NJE YA KUMI NA NANE: fikiri, Hoji Na Uliza Maswali Katika Ulimwengu Ambao Hautaki Uwe Hivyo.


Rafiki yangu, kama kwenye maisha yako bado hujafikia hatua ambapo wewe unaweza kufikiri nakuhoji na kuuliza maswali vitu. Basi bado hujaianza safari yako ya maisha. Hii ni hatua muhimu sana ambayo unapaswa kuifikia.

Tuli[pokuwa wadogo tulikuwa tunapenda sana kuuliza maswali. Kuanzia maswali ya Mungu ni nani? Mpaka maswali ya watoto wanatoka wapi? Ila baada ya kukua inaonekana kuna ustaarabu ambao unakuja ghafla. Na ile shauku ya kujua vitu ambayo unakuwa nayo tangu utotoni inapotea. Leo hii nipo hapa kukwambia kuwa unapaswa kuendelea

Kufikiri

Kuuliza maswali

Kuhoji

Na kufanya maamuzi yako mwenyewe.

Hakuna mtu ambaye anaweza kufikiri kwa niaba yako. Usimwongope yeyote.

Watu wengi, viongozi wengi hawapendi kabisa uulize maswali au uhoji au ufikiri kwa namna yako. Ukionekana unafikiri, unahoji na kuuliza maswali na kufanya maamuzi yako mwenyewe unaonekana wewe ni tishio kwao na kwa uongozi wao!

Ndiyo maana hata mfumo wa elimu ulipokuja hapa barani kwetu Afrika uliletwa katika mfumo huuhuu. Kwamba wapokeaji wa elimu wasiwe watu wa kufikiri, bali wawe watu wa kupokea maagizo na kuyafanyia kazi.

Unaweza kudhani ni utani, unaweza kusema haka ka jamaa kanapata wapi ujasiri wa kusema haya, kama huniamini mimi basi iamini hata hii barua aliyoiandika Mfalme Leopord wa Pili kwa ajili ya wamisionari waliokuwa wanaeneza injili Afrika.

Kwenye barua yake ameandika hivi; wafundishe hawa watu kusoma lakini siyo kufikiri.

Hii dhana ya kufikiri, kuhoji na kuuliza maswali inaleta utata miongoni mwa watu wengi.

Kwenye dini ukionekana unauliza maswali sana, watakwambia kwamba umeanza kuasi. Hivyo ili usionekane kama mtukutu unapaswa kufuata kila kitu kinachoelezwa au unachoambiwa. Kama una swali kafie nalo mbele huko…

Kwenye elimu mpaka vyuo vikuu hivyohivyo, ukionekana unauliza sana, inaonekana unataka kuwa *challenge* maprofesa. Wanaweza mpaka wakakufelisha hivihivi..

Wanafunzi wenzako wakiona unauliza sana maswali, wataanza kudhani ni utukutu tu au unajionesha.

Sasa nataka nikwambie kitu kimoja tu, hoji kila kitu kwenye maisha yako. Uliza kila kitu, hata hili andiko unaruhusiwa kulihoji  na kuuliza. Ni kwa jinsi hii ndiyo utaweza kuupata ukweli kamili wa kile ambacho kineongelewa au ambacho unaanmbiwa. Na hivyo utaishi maisha yenye uhuru sana.

NB: Hiyo barua ya mfalme Leopord wa pili wa wabeljiji unaweza kuipata mtandaoni. Andika, King Leopords letter to African Missionaries.

Utakachosoma huko siri yako.

Uwe na siku njema sana

SOMA ZAIDI: Vitu viwili vinavyokufanya ushindwe kufikia ndoto zao

Makala ya hii imeandikwa na Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X