JINSI YA KUEPUKA TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO -2


Nilisemaje, mwezi huu; naam, mwezi huu nitakuwa naeleza kwa undani Zaidi kuhusu tabi aya kughairisha na namna ambavyo unaweza kuondokana tabia hii. Tayari niliandika Makala ya utangulizi siku ya juzi. Kama ulikuw abado hujasoma hii Makala, basi ni muda wako wa kuhakikisha kwamba umeisoma hapa.

Sasa siku ya leo; ninaenda kukushirikisha nguvu ya kauli unazojiambia zilivyo na uwezo wa kukufanya uwe mtu wa kughairisha mambo au kukusaidia uepuke hilo. Wahenga wetu walikuwa  ni watu makini sana tokea enzi na enzi. Ndiyo maana walikuwa aksema kuwa maneno huumba. Na ukweli ni kuwa maneno yanaumba. Unachotakiwa kufanya ni kuyatumia maneno yako vizuri.

Kwa hiyo, badala ya kujiambia kwamba nitafanya kesho.

Badala ya kusema kwamba hili siwezi kulifanya, jiambie maneno na kauli chanya.

Mfano unaweza kuwa umechoka; badala ya kusema kwamba nitfanya kesho. Unaweza kusema kwamba japo nimechoka, ngoja nianze kufanya kidogo.

Maneno unayojiambia y anaumba. Badala ya kujiambia maneno hasi.

Badala ya kusema kwamba leo hili haliwzekani kufanyika; sema kwamba  ninaenda kuanza kufanyia kazi lengo langu hata kama ni kidogo. Nitapata motisha Zaidi kaditi ambavyo nitakuwa nazidi kufanyia kazi lengo langu.

Ni kwa namna gani kujiambia maneno hasi kumekuwa kunachangia kwako kwenye kushindwa kufanikisha mnalengo yako?

Ni hatua gania ambazo unaenda kuchukua sasa hivi ili uondokane na hili?

Soma sehemu ya kwanza hapa: NJIA ZA KUEPUKA KUGHAIRISHA MAMBO 2024


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X