Usiogope kukosea


Vitu vingi ambavyo huwa tunafanya kwenye maisha huwa vinahusisha makosa. Ni vigumu kuanza kufanya kitu kwa ufanisi wa asilimia 100 hasa unapofanya mara ya kwanza.

Mtoto anapoanza kutembea, haanzi kutembea huku akiwa anatembea kwa usahihi asilimia 100. Anaanza kwa kuanguka, ila ni kupitia huku kuanguka ndiyo baadaye anaweza kutembea vizuri bila wasiwawasi wowote. Baadaye tunakuja kumwona huyo mtoto akikimbia mbio za marathon n.k

Unaikumbuka siku yako ya kwanza kazini?

Mara nyingi siku ya kwanza ya kufanya kitu huwa siyo bora sana. Ila kadiri unavyokuwa unafanya ndivyo unakuwa unazidi kuwa bora zaidi.

Huwezi kusema kwamba mimi nasubiri kuw amkamilifu ili nianze. Hakuna kitu ambacho huw akinaanz akikiw ana ukamilifu wa asilimia 100.

Simu za kwanza hazikuwa kamilifu.

Ndege za kwanza hazikuwa kamilifu.

Ukamilifu kwenye hii dunia haupo. Ndiyo maana utagundua kwamba kompyuta huwa zinakuja katika matoleo. Kuna toleo la kwanza, kuna toleo la pili na kuendelea.

Hii haimaanishi kwamba uanze kutoa kazi ambazo hazina ubora, badala yake kila kazi ambayo utaweka mkono wako, hakikisha kwamba ndiyo kazi bora kuliko zote kwa wakati huo. Kama badaye kutatokea kwamba kunahitajika marejekebisho, au kuna vitu unatakiwa kuboresha basi utaboresha.

Lakini pia, unapotoa kazi yako, kuna watu wanatoa mapendekezo yao ya nana gani uweze kuboresha kazi yako. Ni vitu gani zaidi ambavyo unaweza kuongeza ili kuifanya kuwa bora zaidi. Haya maoni, haya siyo ya kupuuza. Yafanyie kazi. Boresha kazi na ifanye kuwa bora zaidi.

Baada ya kusema hayo,naomba nikutakie kila la kheriii.

SOMA ZAIDI: Usiogope Kuuliza

Makala  hii imeandikwa name rafiki yako

Godius Rweyongeza

0755 848 391

Morogoro-Tz

Tuwasiliane kwa godiusrweyongeza1@gmail.com


One response to “Usiogope kukosea”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X