Vitu 13 ambavyo hakuna mtu anaweza kufanya Kwa niaba Yako


Kuna vitu ambavyo unaweza ukawapa watu wengine wavifanye kwenye Maisha yako, lakini pia kuna vitu ambavyo huwezi kuwapa watu wengine wavifanye kwa niaba yako. Ni lazima uingie ulingoni na uvifanye mwenyewe.

Watu wengi wamekuwa wanakosea hasa kwenye hili kwa kuacha kufanyia kazi vile vitu ambavyo wao wanapaswa kufanyia kazi, wanasubiri watu wengine waje wavifanyie kazi wakati hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kufanya hivyo vitu kwa niaba yao. Ukweli ni kuwa kuna vitu ambavyo unaweza kuwapa wengine, lakini wakati huohuo ni ukweli kuwa kuna vitu vingine ambavyo huwezi kuwapa wengine wavifanye kwa niaba yako. Hivyo unapaswa kuvifanya mwenyewe.

Lengo la Makala hii ni kukuonesha wapi haswa kwenye Maisha yako unapaswa kuweka nguvu, huku ukijua wazi kuwa hakutakuwa na mtu yeyote ambaye ataweza kufanya hivyo vitu kwa niaba yako. Badala yake utapaswa kuhakikisha kwamba unavifanya hivyo vitu mwenyewe bila ya kusubiri mtu yeyote ambaye unaweza kuwa unamtegemea aweze kukusaidia wewe kwenye kuvifanyia kazi hivyo vitu ambavyo wewe mwenyewe unafikiria kwamba unaweza kufanyiwa.

Sasa vifuatavyo ni vitu ambavyo huwezi kufanyiw ana mtu yeyote. Ni sharti uingie ulingoini uvifanye mwen ywe. Ni kama

 1. Kujiamini wewe mwenyewe

Hakuna mtu ambaye anaweza kujiamini kwa niaba yako. Kujiamini ni jukumu lako, ni lazima mara zote uhakikishe kwamba unaonesha ujasiri na kujiamjni hata kama unapitia katika hali ngumu. Ukweli ni kuwa hata kama unapitia kwenye hali ngumu, kuna watu wengine ambao wanakuwa wanapitia kwenye hali ngumu zaidi yako. Hivyo, hakikisha kwamba mara zote jiamini, maana hiki kitu hakuna mtu ambaye ataweza kukifanya kwa niaba yako.


 1. Kuwapenda wazazi wako

Kama una wazazi; hakuna mtu ambaye atakusaidia kuwapenda wazazi wako kwa niaba yako. Ni jukumu lako; wapende wazazi wako.


 1. Kumpenda mwenza wako

Kama ilivyo kwa wazazi wako, mwenza wako pia hakuna ambaye anaweza kukusaidia kumpenda. Akikusaidia mwingine kumpenda, anakuwa amekusaidia kweli, hahah. Mpende na hakikisha analijua hilo. Mwambie hivyo mara kwa mara.


 1. Kufanya mazoezi

Hakuna mtu anaweza kufanya mazoezi kwa niaba yako. Yaani, kwamba mtu akimbie kilomita moja kwa niaba yako. Hakuna kitu kama hicho, hili ni jambo ambalo wewe mwenyewe unapaswa kulifanya kwa uhakika. Hivyo, badala ya kusubiri mtu aje akufanyie kmazoezi; anza wewe kufanya mazoezi. Hata kama ni kwa dakika tano tu.


 1. Kula vizuri

Kama ilivyo kwa mazoezi; hakuna mtu ambaye anaweza kula vizuri kwa niaba yako. Ni lazima uwe tayari kula vizuri kwa ajili ya afya yako mwenyewe.


 1. KUWEKA AKIBA NA KUWEKEZA

Hakuna mtu ambaye anaweza kuwekeza fedha kwa niaba yako. Ukibahatika Rafiki yako atakupa zawadi ya kiasi kidogo cha fedha au atampa mwanao zawadi ya uwekezaji kwenye hisa au UTT ila kama unataka kujenga utajiri na uhuru wa kifedha, basi wewe unapaswa kuwa tayari kulifanya mwenyewe hili. Hiki kikombe hakikuepuki. Unapaswa kuwa tayari kunywa maji yake.


 1. Kujifunza na hasa kusoma vitabu

Kama ilivyo kweli kuwa hakuna mtu anayeweza kwenda chuo kikuu kusoma kwa niaba yako; hivyo hivyo hakuna mtu ambaye anaweza kusoma kitab una kupata maarifa kwa ajili yako. Hii ngoma inakuhusu. Ni sharti ufanye mwenyewe.


 1. Kuanzisha biashara

Una wazo la biashara? Sasa unataka nani alifanyei kazi kama siyo wewe. Hakuna mtu ambaye anaweza kuanzisha biashara kwa niaba yako. Ni sharti uanzishe biashara mwenyewe.


 1. Kuwapenda na kuwajali wanao

Kama ilivyo kwa wazazi. Kama ilivyo kwa mwenza wako. Hivyohivyo kwa wanao. Hakuna mtu ambaye anaweza kuwapenda wanao kwa niaba yako


 1. Kupangilia ratiba yako

Ratiba yako ya kila siku, ratiba yako ya wiki, ratiba yako ya mwezi, hakuna mtu ambaye anaweza kuipanga kwa niaba yako. Wewe ndiye unapaswa kuipanga na kuwa makini na ratiba yako ili uweze kuifuata kwa ufanisi ili uweze kupata matokeo makubwa.


 1. Kusamehe

Hiki ni kitu kingine ambacho hakuna mtu anaweza kufanya kwa niaba yako. Samehe SONGAMBELE


 1. KUFANYIA KAZI NDOTO ZAKO.

Kila mtu ana NDOTO zake. NDOTO za jirani Yako siyo za kwako. Ni kweli unaweza kuajiri watu, lakini Kuna nafasi Yako wewe kama wewe…unapaswa kuwaonesha wapi unaelekea na kuwapa mwongozo sahihi wa kufuata. Huwezi TU kubweteka na kumsubiri mtu akufanyie kazi NDOTO ZAKO. Kama angekuwa anajua SI angefanyia TU kazi NDOTO ya kwake.
Unahitaji umpe mwongoZO

Rafiki yangu, hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo hakuna mtu anaweza kufanya kwa niaba yako. Nimeona ni vyema nikudokeze hivi vitu ili uepuke kuingia kwenye mtego wa kukaa kusubiri mtu avifanye kwa niaba yako.

Huu ujumbe naomba uwafikie watu wote ambao wanakaa na kuilaamikia serikali kuwa haijawafanyia kitu Fulani. Ujumbe huu uwafikie wote wanaolalamika kuwa wazazi hawakuwasomesha. Japo una pointi nzuri kuwa wazazi wako hawakukusomesha, ila sasa wakati wa kupambania Maisha yako ni sasa. Hilo limeshapita, unachopaswa kufanya ni kuweka malengo na kuanza kuyafanyia kazi. Hakuna mtu ambaye anaenda kuyafanyia kazi haya malengo kwa niaba yako.

Nadhani orodha hii ni ndefu, naomba mimi niishie.

Kama unamfahamu mtu ambaye huu ujumbe unamhusu, ebu mtumie huu ujumbe aweze kuusoma

Mwambie Godius Rweyongeza nampenda sana kutoka hapa mji kasoro pwani Morogoro mjini

Kwa mawasiliano Zaidi godiusrweyongeza1@gmail.com


One response to “Vitu 13 ambavyo hakuna mtu anaweza kufanya Kwa niaba Yako”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X