INAUMIZA SANA! Kosa Kubwa Unalofanya Linaloathiri Ubongo Wako Na Namna yako Ya Kufikiri (Ukikabiliana na hili kosa, utabadili maisha yako kiujumla)


Nimekuwa mkulima tangu nimezaliwa mpaka leo hii. Kiuhalisia nimekuwa nikiwaambia watu kuwa kitu ambacho kitanipa ubilionea ni kilimo. Na huu ndiyo ukweli, na kuthibisha hilo chuoni nilibobea kwenye kilimo, nikiwa najua kabisa Kilimo tu lazima kitanitoa siku moja.

Moja ya kitu ambacho huwa tunakilinda sana kwenye kilimo ni bustani yako au shamba. Ukweli ni kuwa kwenye shamba langu mimi siwezi kukubali mtu yeyote aingie tu hovyohovyo na kufanya chochote. Lina ulinzi, na nikigundua mtu kaingia, inaweza kuwa kesi kubwa.

Hiki kitu siyo kwangu tu, ila ni kwa wakulima wengi. Hakuna mkulima yeyote kwa mfano ambaye anaweza kuruhusu mtu aingie shambani kwake na kuweka sumu, au uchafu wa namna yoyote ile ambao hautakiwi. Kama wewe unaweza kumruhusu mtu afanye hivyo kwenye shamba lako nadhani unaweza kuandika maoni yako hapo chini, ili tujue.

 

Sasa ebu pata picha ya shamba, ni kitu ambacho tunakilinda kwa nguvu zote. Ila cha kushangaza ni kwamba tunasahau kitu kimoja muhimu sana ambacho tunapaswa kukilinda kwa nguvu zetu zote. na kitu hiki siyo kingine bali ni uboongo wetu.

Ubongo wako wewe ndiyo. 

yaani, inashangaza kuona kwamba unalinda sana bustani, ila linapokuja suala zima la ubongo wako unabugi. Unaacha watu wanaweka sumu na kiila aina ya uchafu.

Mpaka hapo unaweza kuwa unajiuliza, kuwa hili linawezekanaje? Ukweli ni kuwa hili linawezekana kwa kile unachokuwa unaruhusu kuingiza kwenye ubongo wako.

Pale unaporuhusu habari hasi ziingie kwenye akili yako, maana yake unakuwa umeamua kuweka sumu kwenye ubongo wako.

Pale unaporuhusu habari za kukatisha tamaa, umbea na vingine vyote vinavyoenana na hivyo, maana yake unakuwa umeamua wewe mwenyewe kwa ridhaa yako mwenyewe kuingiza habari hasi kwenye ubongo wako.

Kitu kama hiki siyo kitu ambach ounapaswa kuruhusu kiendelee kwenye ubongo wako. Hapana, badala yake ni kwamba unapaswa kulinda ubongo wako na kila kitu kinachoingia kwenye ubongo wako kwa nguvu zako zote.

Uko ulivyo kwa sababu ya kile unachoingiza kwenye ubongo wako. Hii ndiyo kusema kwamba kama unataka kupata matokeo ya tofauti, sharti, uwe tayari, kuingiza vitu ambavyo vitakupelekea wewe kupata hayo matokeo.

NA VITU MUHIMU AMBA YO UNAPASWA KUANZA KUINGIZA KWENYE AKILI YAKO KUANZIA LEO 

  1. Maarifa chanya. Yaani maarifa ambayo yanakusukuma wewe kusongambele na siyo kurudi nyuma.
  2. maarifa haya unaweza kuyapata kupitia vitabu, soma vitabu vingi kadiri uwezavyo. Unaweza kuanza na kitabu changu ambacho nakitoa bure kabisa. KIPATE HAPA CHINI, KINATUMWA KWENYE EMAIL, hviyo jaza email yako ili uweze kukipata.

3. Maarifa haya pia unaweza pia kuyapata kupitia kujifunza kwenye semina, mafunzo mbali mbali kama makala nk.

4. Maarifa haya unaweza pia kuyapata kupitia makala mbalimbali kama hii hapa

 

Ikumbukwe kuwa, jukumu la kutunza bustani ya akili yako ni jukumu lako. hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kufanya hili jukumu kwa niaba yako. Jukumu hili kama kupiga push up, hakuna mtu ambaye anaweza kupiga pushup kwa niaba yako hata siku moja. Unapaswa kulifanya wewe mwenyewe

SOMA ZAIDI: Vitu 13 ambavyo hakuna mtu anaweza kufanya Kwa niaba Yako

Hivyo ni wajibu wako kuhakikisha kwamba umelifanyia kazi hilo jukumu bila ya kurudi nyuma.

Kwa leo naomba niishie hapa

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755

 

For Consultation only: +255 755 848 391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X