Hivi Ndivyo Vitu Ambavyo Vinakukwamisha Wewe Na Nini Cha Kufanya


UNAENDELEAJE RAFIKI YANGU WA UKWELI, Karibu Tena kwenye blogu yetu kwa ajili ya mafunzo mengine mazuri ambayo nimeandaa kwa ajili yako. Siku ya leo  nina ujumbe mfupi tu kwa ajili yako. na ujumbe huu siyo mwingine bali ninataka kukwambia kuwa;

Asilimia kubwa ya vitu ambvyo vinakuzuia wewe kufanikiwa ni vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wako. Ukiweza kuvuka hivi vikwazo ambavyo vipo ndani ya uwezo wako. Utaweza kufanya makubwa sana.

Vikwazo hivi ambavyo vipo ndani ya uwezo wako ni pamoja na

  1. Uzembe. Ukiachana na uzembe na kuchapa kazi, utaweza kufanikisha makubwa
  2. Kutokuwa na ratiba. Hiki ni kitu kingine ambacho ndani ya uwezo wako. Ukianza kuipangilia ratiba yako, itakusaidia sana kufanya makubwa bila kusukumwa na mtu yeyote. Ratiba yako inapaswa kuwa imebana muda wote, kiasi kwamba upatikanaji wako uwe ni mgumu mara zote.
  3. Kutokufanya maamuzi. Muda mwingine kutokufanya maamuzi kunakukwamisha sana wewe kupiga hatua. Inawezekana ni kuchelewa kufanya maamuzi, au kutofanya maamuzi kabisa. Unachotakiwa kufahamu ni kuwa maamuzi ni sehemu ya maisha yako. hakuna namna ambavyo unaenda kuyaepuka. Kitu kikubwa ni kwamba unapaswa kuyafanya kwenye maisha yako ya kila siku. Usiogope kufanya maamuzi hata kama muda mwingine yanakuogopesha.
  4. Kutaka kufanya kila kitu mwenyewe. Hiki ni kitu kingine ambacho kinakwamisha watu wengi. Ukweli ni kuwa huwezi kufanya kila kitu mwenyewe. Ni lazima uwe tayari baadhi ya vitu vingine kuwapa wengine wafanye. Maisha ni kusaidiana, ukitaka kupambana na kila kitu, ukweli ni kuwa hutaaweza. na kama utaweza basi itakuwa ni kwenye ngazi za chini kabisa. Unachohitaji wewe kufanya vitu katika ngazi za juu, na ili uweze kufanya vitu katika ngazi hizi za juu, unahitaji watu. Usemi wa kiafrika unasema kwamba ukitaka, kufika haraka tembea peke yako, ila ukitaka kufika mbali, nenda na watu. Sasa swali langu kwako ni je, unataka kwenda haraka au unataka kufika mbali?
  5. Kutokufanya kazi kwa viwango vikubwa. Hiki ni kitu kingine ambacho kipo ndani ya uwezo wako.

Ukweli ni kuwa kazi yoyoote ile ambayo wewe unashika, unapaswa kuifanya kwa viwango vikubwa kiasi kwamba uwashangaze watu watu watakaoshika kazi hiiyo. Je, umekuwa unafanya hivi. Au watu wamekuwa wanashika kazi hiyo na kuona kwamba wewe unashangaza kwa kutofanya kazi kwa ubora. Kama ni hivyo, basi unapaswa kurekebisha ambacho umekuwa unafanya, ili uweze kufanya kazi zako kwa viwango vikubwa na vya hali ya juu.

Rafiki yangu Hivyo Ndivyo Vitu Ambavyo Vinakukwamisha Wewe Na hizo ndizo hatua unazopaswa kuchukua. na hatua hizi unapaswa kuzichukua leo hii.

Nakutakia siku njema.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Unaweza kujifunza zaidi kwa kufuatilia makala za Godius Rweyongeza kwenye youtube channel yake ambayo unaweza kuipata kwa kubonyeza hapa

mafunzo mengine zaidi huwa anayotoa kupitia email. unaweza kujaza taarifa zako hapa ili mmoja wa wale ambao wananufaika na mafunzo yake kwa email

Kila la kheri

Godius Rweyongeza

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X