Kila sehemu ina kanuni zake maalum ambazo kila mmoja anapaswa kuzifuata. Na kanuni huwa zikifuatwa, mara zote huwa zinaleta matokeo chanya, ila zikikiukwa au kupuuzwa, huwa unakuta kwamba unapata matokeo hasi.
Mfano wa wazi kabisa kwenye hili ni kwenye kuendesha gari barabarani. Ukifuata kanuni za kuedesha gari barabaani, ni wazi kwamba utaweza kufika salama kule ambapo unaelekea, ila kwa upande mwingine ukiedesha gari kwa namna unavyotaka mwenyewe. Badala ya kupita kushoto ukapita kulia, sehemu yenye mataa ambayo yanayokuonesha kwamba unapaswa kutulia kwanza, wewe ukapitiliza tu moja kwa moja.
Sehemu unapopaswa kwenda kwa mwendo wa 50 wewe ukaenda kwa 120
Ni wazi kuwa huwezi kufika salama. Unaweza kufanikiwa kubahatisha mara moja, ila huwezi kufanya hivyo mara zote kwa mafanikio makubwa.
Sasa tunapoongelea biashara. Ina kanuni zake pia.
Ukizifuata unatoboa, ila usipozifuata, ni wazi kuwa amambo mengi yanaenda kuwa magumu kwa upande wa wako.
Unapoanzisha biashara, kuna mambo 55 ambayo unatakiwa kuzingatia kama ambavyo nimeyaeleza kwenye kitabu MABO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA. Nakushauri uweze kupata nakala yako na ujisomee, utanishukuru sana kwa siku zijazo.
Ila kwa leo ningepnda kuongelea kitu kimoja tu. kitu hiki ni muda wa kufungua na kufunga biashara yako.
Unapoanzisha biashara yako, hakikisha kwamba unakuwa na muda maalum ambao unakuwa umefungua na muda maalum wa kufunga biashara yako. Hiki ni kitu kidogo sana lakini chenye nguvu kubwa sana.
Kiufupi ni kwamba unapoanzisha biashara yako unapaswa kuanza kuiwekea misingi sahihi. Bila ya kuwa na misingi sahihi, huwezi kujenga biashara ya maana. Misingi sahihi ndiyo ambayo itakufanya uiendeshe biashhara yako bila stress hata kidogo.
Na moja ya msingi muhimu ambao unapaswa kuuweka ni msingi wa kufungua na kufunga biashara yako.
Ijulikane kabisa kwamba, muda wa kuingia kazini ni saa fulani na muda wa kutoka ni muda fulani. Kuwa na utaratibu kama huu hata kama kwenye biashara yako kwa sasa hivi uko peke yako.
Kumbuka kwamba lengo la biashara yako siyo wewe kuendelea kufanya kila kitu peke yako. Badala yake ni kwamba lengo lako kubwa ni kuhakikisha kwamba hii biashara inakua na unakuwa na matawi pamoja na watu wengine ambao wanakusaidia kwenye kufanya na kutekeleza baadhi ya majukumu. Sasa haya majukumu huwezi kuyatekeleza kwa ufanisi bila ya kuwa na mpango wa muda maalum wa kuingia na kutoka.
Ushauri wangu kwako kabla hujaenda kuweka muda wa kuingia na kutokia kazini kuwa saa tatu. Maana niliwahi kuongea na rafiki yangu mmoja akaniambia mimi muda wa kuingi na kutoka kazini ni saa tatu naingia, na saa kumi na moja nafunga.
Ni kweli kwa upande wa benki kuna mengi ya kujifunza kutoka kwao, ila kwa upande wa muda naom,ba unisikilize.uKIWAIGA BENKI UTAPASAUKA MSAMBA.
Unajua kwa nini nakwambia hivi, ni kiwa sababu benki huwa zinafanya kazi saa 24 siku saba za wiki. Kuna ATM za kutoa pesa benki, ambazo zinafanya kazi saa 24. Wewe biashara yako ina ATM kama hii. Ni kitu gani kwenye biashara yako ambacho kinafanya kazi saa 24 bila ya kuacha. JE, NI BLOGU AU TOVUTI?
Najua unaijua vizuri biahsara yako, sihitaji nikuhubirie kwenye hilo, ila lifahamu. Na umakini wako wote uweke kwenye kuijenga vizuri kuanzia mwanzo,
Sasa hivi benki zinakuja na ATM za kuweka pesa. Maana yake utakuwa na uwezo wa kuweka na kutoa benki muda wowote.
Wewe unapoanza biashara yako, kuwa na utaratibu huu wa kuingia na kutoka na hasa muda wako uwe mapema.
Mapema ikiwezekana saa 12, hiki kitu kitakusaidia wewe kuwa unawapata wateja wa asubuhi na mapema na wateja wa jioni baada ya wengine kuwa wamefunga. Katika ulimwengu ambao dunia inafanya kazi saa 24.
Wewe pia unapaswa kuwa na muda mrefu ambao biashara yako itakuwa imefunguliwa kwa kuanzia. Na tunapoelekea, biashara yako inaweza kuwa imefunguliwa muda wote saa 24.
Kwa leo nitaishia hapa, ila ukiendelea kufuatilia makala na mafunzo mengine ambayo ninatoa hapa kila siku, utazidi kujifunza zaidi hasa kuhusu biashara na namna ambavyo unaweza kuboresha kile unachofanya.
Kujifunza zaidi soma makala hizi
- Njia Tano Za kuwa na Ukuaji Kwenye Maisha, Biashara na Kila kitu unachofanya
- Ni muda Upi Sahihi Kuajiri Wafanyakazi kwenye Biashara?
- Sababu mbili Kwa Nini kila anayetaka kuwekeza anapaswa kuwa na biashara pia
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755
For Consultation only: +255 755 848 391