Njia Tatu Za Uhakika Zitakazokusaidia Wewe Kuweka Akiba Bila Ya Kutoa (Namba 3 Ndiyo Yenyewe Haswa!)


Wahenga wanasema kwamba ukiona vyaelea, basi ujue vimeundwa, hivyohivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mji wa Babilon (Babeli) ambao kwa nyakati zake ulikuwa mji tajiri na wenye watu wenye utajiri.

Simulizi zake na busara za nyakati hizo zimebaki vitabuni kwa ajli yetu sisi vijana wa miaka yetu kuzitumia kwa manufaa. Lakini moja ya kitu kimoja na kitu kikubwa ambacho tunajifunza kutoka kwa hawa watu ni kuweka akiba bila kukoma.

Yaani, kila siku kuifanya kuwa siku ya kuweka akiba.

Ukweli ni kuwa, kama una ndoto kubwa na malengo yoyote yale makubwa, ukweli ni kuwa hayo malengo, yatatimia tu kwa wewe kuwa na fedha. Asilimia kubwa ya ndoto ulizonazo zinahitaji fedha, ila cha kushangaza zaidi ni kwamba hizi fedha siyo kwamba unazo kama keshi mkononi mwako leo hii.

na isitoshe kila siku kuna majukumu mapya ambayo yanazidi kujipenyeeza yakiwa yanahitaji fedha zako unazozipokea kila leo.

sasa unafanyaje ili uweke akiba bila kuitumia.

kwa leo ninaenda kukutajia njia tatu tu za uhakika ambazo zitakusaidia wewe kuweka fedha bila kuzitumia,

  1. kwanza ni kuweka fedha yako kwenye akaunti ya simu ambayo wewe mwenyewe hauna neno lake la siri. Hiki kitu kinaweza kuwa kimekuja kwako kama mshangao kidogo. Yaani, iweje niweke fedha kwenye akaunti ambayo mimi sina neno la siri. Ndiyo inawezekana, unachotakiwa kufanya ni hivi, unasajili laini yako. Halafu unamtafuta mtu ambaye unamwamini, mtu ambaye anaweza kukushikilia. Halafu mtu anakuwekea namba ya siri kwenye hii akaunti yako. Halafu unamwahidi kwamba naomba usinitajie namba ya siri mpaka pale nitakapokuwa nimeweza kuweka akiba ya kiasi kadhaa kwenye hii laini. Mfano, unaweza kumwambia kwamba usinitajie neno la siri mpaka pale nitakapokuwa nimeweza kuweka akiba ya milioni mbili kwenye hii laini. Kwa hiyo, laini unakuwa nayo wewe, umeisajili wewe ila kitu pekee ambacho hauna ni namba ya siri. Huyu mtu wako wa karibu anakupa tu namba ya siri unapokuwa umetimiza lengo la awali. na hapo ndipo unapata uwezo wa wewe kwenda kutoa hiyo fedha. Hii ni njia ya kwanza, kama hii ni ngumu kwako. Twende kwenye njia nambari mbili.
  2. Fungua akaunti kwenye benki ambayo hutachukua kadi, hutaiunganisha na njia yoyote ile ya kimtandao, na wala hutachukua checkbook ya kutolea fedha. Yaani, unabaki unajua akaunti ya benki tu. Unaanza kuweka akiba kwenye hii akaunti, hutoi pesa mpaka unapokuwa umeweza kufikia lengo lako.
  3. Weka hela yako Utt moja kwa moja. Tena ngoja kwenye hili nikushauri vizuri kabisa, sajili akaunti yako kwa simu. Hapo chini ninaenda kukuwekea njia sita za kufungua akaunti yako ya utt amis. Ukisajili akaunti ya UTT, usajili wako unakuwa haujakamilika, lakini kwa aina hii ya usajili, unaruhusiwa kuweka pesa na unanufaika na vitu vyote vizuri vinavyopatikana pale UTT AMIS, ila haurusiwi kutoa fedha. Sasa hii ni nzuri kwako, kwa sababu, usajili haujakamilika. Unaweza kuamua kuacha hivihivi siku zote, ukaja kukamilisha usajili wako pale unapokuwa umekamilisha lengo lako. Kwa maoni yangu, hii ndiyo njia bora zaidi kuliko zote. Ni njia bora kwa sababu tu, inakusaidia wewe kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Unaweka akiba huku ukipata faida za kiuwekezaji. Inawezekana hapa unajiuliza, Hivi hii UTT ni nini? Inafanyaje kazi? Na mimi naweza kujiungaje? Nina mwongozo mzuri, kitabu ambacho kitakusaidia wewe kupata maarifa kamili kuhusu uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI na VIPANDE. Unaweza kupata kitabu hiki kwa kuwasiliana na +255 684 408 755. Fanya hivyo sasa hivi.

Kwa leo hizi zinatosha au unasemaje rafiki yangu! Kikubwa ni kwamba uanze kuzifanyia kazi. Kamwe hutapata matokeo bila ya kuzifanyia kazi hizi mbinu. Ni mpaka uanze kuzifanyia kazi ndipo utakuja kupata matokeo ambayo yameelezwa au ambayo unatazamia kupata.

Kitu kikubwa ambacho unapaswa kukifanyia kazi siku ya leo ni kuhakikisha umepata nakala nzuri sana za vitabu. Nakala hizi ni kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE pamoja kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA. Hivi vitabu vina mwongozo kamili hasa kuhusiana na mada ya leo ambayo nimeieleza hapa kwa kina.  Usichelewe kuwasiliana na +255 684 408 755 sasa ili uweze kujipatia nakala zako leo hii. Kila nakala ni 25,000/-. Jipatie nakala zako sasa.

SOMA ZAIDI: Ijue Siri Ya Babiloni Kuwa Mji Tajiri Kuliko Yote Duniani

Sababu 100 kwa nini unapaswa kuweka akiba ya pesa

Rafiki yangu, kwa leo, naomba niishie hapo.

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli,

Godius Rweyongeza

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755

For Consultation only: +255 755 848 391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X