Aina Tano (05) ya watu ambao kila mfanyabiashara anapaswa kujenga nao urafiki wa karibu


Rafiki yangu wa ukweli salaam. Hongera sana kwa siku hii nyingine ya leo. Leo nataka kukwambia aina tano ya watu ambao kama mfanyabishara unapaswa kuanza kujenga nao urafiki mapema.

Unapaswa kuanza kujenga urafiki wa namna hii mapema sana bila kujali biashara yako ni ndogo au kubwa.

#1. ni wanasheria.

Hawa ni watu muhimu sana kwenye ulimwengu wa biashara. wanaweza kukushauri mambo mengi, kuanzia kwenye mikataba (ukweli ni kwamba kama mfanyabiashara kuna mikataba mingi ambayo utaingia, na wafanyakazi, na washirika, wasambazaji n.k), mpaka kwenye maamuzi fulani ya kisheria ambayo utatakiw akufanya kwenye safari yako ya biashara.

watakushauri mengi kuanzia kwenye mikataba ya wafanyakazi na hata namna bora ya kuondoa wafanyakazi bila mkono wa sheria kukupitia. Na mengine mengi.

hivyo, moja ya kipaumbele chako kiwe ni kujernga uhusiano wa karibu na wanasheria. Kama kwenye mzunguko wako hauna mwanasheria, basi ni muda muafaka wa kufanya hivyo.

 

#2. Washauri wa kodi

hawa ni watu muhimu sana. Wanajua mengi kuhusu kulipa kodi ambayo hujui, wanajua namna ya kukusaidia kulipa kodi sahihi kwa wakati sahihi. Ukiw ana hawa watu watakusaidia sana kulipa kodi inayoendana na kile unachotakiwa kulipa

 

#3. Wahabibu

Hawa ni watu wengine muhimu sana ambao unapaswa kujenga nao ukaribu. Hawa watakusaidia sana kwenye kutunza hesabu za biashara yako vizuri.

 

#3. Watu wa masoko

Ni wazi kuwa biashara yako itakuwa na kitengo cha masoko. Hivyo, unahitaji pia kuhakikisha kwamba unakuwa na watu wa namna hii. Watu hawa wa masoko watakusaidia kwenye kutangaza bidhaa zako unazouza na kulifikia soko lako vizuri.

 

#4. graphic designers

Hawa watakusaidia kudizaini kazi zako na hasa katika mfumo wa video na picha. Kummbuka picha moja inaongea maneno milioni.

 

#5. kocha

Unahitaji kuwa na kocha ambaye atakushikiria hasa kwenye kufuatilia malengo na ndoto zako ili uweze kuzifanyia kazi kama ulivyoziweka. Bila ya kuwa na mtu wa namna hii, utajikuta kwamba unaweka malengo ila huyafanyii kazi. Au unaanza kuyafanyia kazi ila hayatimii.

 

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X