Epuka Makosa Haya Matano (05) Kwenye Biashara Yako


Rafiki yangu mfanyabiashara, Leo nataka nikuainishie MAKOSA matano ambayo wafanyabiashara Wengi hufanya. Tafadhali hakikisha kwamba unayaeouka Haya MAKOSA Kwa manufaa ya biashara Yako ya Sasa na baadaye

Kosa la kwanza: kutioipa biashara Yako jina.

Labda nianze Kwa kukuuliza jina biashara Yako ni lipi? Kama biashara Yako Haina jina unakosea sana.
Mtoto akizaliwa anapewa jina
Wewe pia una jina.
Mpaka mbwa na paka Wana majina.
Sasa wewe unashindwaje kuipa jina biashara Yako.

Ni Muhimu biashara kuwa na jina, maana kikawaida biashara Huwa inachukuliiwa kama kiumbe hai. Na hii itakusaidia wewe kujitofautisha wewe na biashara Yako.

Hivyo, kazi Yako kubwa ya Leo ni kuhakikisha biashara Yako Ina jina

Kama ungependa kupata mwongozo Kamili wa kupata jina zuri la biashara, basi, pata nakala ya kitabu Cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA. Kitabu kina mwongozo Kamili, wa kupata jina zuri Kwa ajili ya biashara Yako, unaweza kupata mwongozo huu Kwa kuwasiliana na +255 684 408 755. Kitabu softcopy ni 10,000/- na hardcopy ni 15,000/- (usafiri ni juu Yako mwenyewe).

Kuna mambo 55 ya kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara, mambo haya yote yameelezwa kwenye hiki kitabu. Kupata nakala yako, wasiliana na +255 684 408 755
Hakikisha unajipatia nakala ya kitabu hiki. Tumia namba ya simu +255 684 408 755

Kosa la pili ni kutoipa kipaumbele biashara yako.

Biashara yako unapaswa kuipa kipaumbele kikubwa sana kuliko kitu kingine chochote. Kama huipi biashara yako kipaumbele unaiua mwenyewe.

Kama umeajiriwa, hakikisha unakuwa na ratiba yako umeigawa mara mbili. Muda wa kazi za mwajiri na muda wa biasahra yako. Usifanye hilo kosa ambalo wengine huwa wanafanya.

SOMA ZAIDI: Kitu Muhimu Unachopaswa Kufahamu Kabla ya Kuvuna Mafanikio yoyote

Kosa la tatu: usikubali ujinga kwenye biashara Yako

Ndiyo usikubali ujinga wowote aidha Kutoka Kwa watu unaofanya nao kazi, washirika, au hata wateja. Kuwepo na misingi ambayo inasimamiwa kwenye biashara yako. Kwenye ubora, kwenye huduma, kwenye viwango ambavyo wafanyakazi wanapaswa kufikia na kamwe usikubali ujinga.

Kosa la nne: usikubali huduma mbovu zitolewe Kwa wateja.
Kwa mteja wako yeyote ambaye anapata huduma kwenye biashara Yako, usikubali apate huduma mbovu. Kama Sasa hivi huduma hazijakaa vizuri Anza kurekebisha Hilo. Ili uwe na huduma ambazo ni bora, huduma za viwango vya juu.

Kosa la tano: usikubali kuwa na siku ambayo hujaipangilia.

Kama mfanyabiashara kosa kubwa unaloweza kufanya ni kutokuwa na ratiba. Hakikisha unakuwa na ratiba ambayo utakifanyia kazi ndani ya siku Yako. Usifanye kitu chochote ambacho hakipo kwenye ratiba yako.

SOMA ZAIDI: Uchambuzi wa Kitabu: The Leader Who Had no Title (Kiongozi Asiye na Cheo); Mambo 200 Niliyojifunza katika kitabu hiki.

Kosa la sita: Usikubali kuendesha biashara Yako bila kutunza kumbukumbu.

Kumbukumbu za PESA. Kumbukumbu za Kila mteja ambaye amenunua. Kumbukumbu zote ziwekwe sawa, maana kesho na keshokutwa hizi kumbukumbu zitakuwa na maana Kwa biashara Yako.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X