Rafiki yangu wa ukweli, salaam. Hongera sana kwa siku hii njema ya leo.
Kwenye biashara kuna kitu kimoja tu ambacho watu huwa wanakosea. Na kitu hiki huwa ni kuhesabu vifaranga kabla havijatotolewa. Yaani, kuhesabu kwamba wameuza wakati bado kabisa hawajauza.
Unakuta mtu anahesabu kwamba ameuza pale anapoahidiwa na mteja kwamba atakuja.
Au anahesabu kwamba ameuza pale mteja anapokuja kwenye biashara yake na kupita, huku akisema kwamba atarudi kununua.
Ukweli ni kuwa hivi vitu vyote havikufanyi kuuza.
Hata kama mteja amechukua mzigo na kuondoka nao, ila kama bado hajakupa hela, fedha, au kama hajaweka fedha hii kwenye akaunti yako. BADO UNAKUWA HUJAUZA.
Hata kama mteja amekuahidi sana kwamba lazima atakuja tu kulipia. Unahesabu umeuza pale unapokuwa umepokea fedha mfukoni au kwenye akaunti ya biashara.
Huu ndiyo muda pekee wa wewe kuhesabu umeuza.
Kabla ya hapo inakuwa bado.
Sasa leo, nataka ujiulize ni mara ngapi umekuwa ukijidanganya kwamba umeuza kwenye biashara yako wakati hujauza?
Kazi yako kubwa ya kufanya siku ya leo ni kuhakikisha kwamba unaanza kuhesabu mauzo ambayo umefanya kwa kupokea fedha na siyo kuhesabu mauzo ya kudhania ambayo hujapokea fedha yake.
Kama bado ulikuwa hujapata nakala ya kitabu hiki cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BISHARA hakikisha kwamba umepata nakala yako siku ya leo. Kupata nakala ya kitabu hiki ni rahisi sana. Wasiliana na nami kwa +255 684 408 755 sasa kupata nakala yako.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com