Iko hivyo. Vitu ambavyo watu wanakwambia kinyume chake na nini chakufanya kuanzia leo hii


Nakumbuka kwenye hesabu za kidato cha tatu kulikuwa na hesabu fulani za maumbo, ambapo ulikuwa unatafuta ukubwa wa pembe fulani au urefu fulani.

Sehemu ya kwanza kabisa ulipokuwa unaanzia ilikuwa ni kutumia zile pembe ambazo zinafanana.

Mfano ungeweza kusema kwamba pembe ABC ni sawa na pembe EFG kwa sababu iko hivyo (its given). Kama yangekuwa maandiko matakatifu basi tungesema imeandikwa.

Sasa leo, nataka nikwambie vitu ambavyo vipo hivyo (given). Havibadiliki, hata ufanyeje.

Lengo la makala hii ni kukwambia ukweli na kukufungua ili uweze kupambania malengo na ndoto zako, bila kurudi nyuma.

Lengo la makala hii ni kukupa hasira, nakwambia bila hasira hii, hutatoboa.

kitu cha kwanza ni ambacho kiko hivyo, ni kwamba wanyonge wanayongwa na haki yao hawapewi.

kama hili ulikuwa hulijui ndiyo nataka ulijue. Kama wewe unaendelea kujiita mnyonge mpaka leo hii, utanyongwa kweli mpaka ufe. Na hapa usije ukaanza kusema kwamba mbona huyu anaandika vitu ambavyo sio kweli na havipo.

Hivi vitu siyo kwamba hata nimevigundua mimi, bali vimekuwepo kwa miaka mingi. Miaka mingi iliyopita Darwin aliwahi kusema kwamba, vitu vinyonge ndiyo vinatoweka kwanza kabla ya vyenye nguvu.

Vinyonge vinakosa chakula.

Vinyonge vinakosa ushawishi

Vinyonge vinakosa hoja

Vinyonge vinakanywagwa.

Ni vivyonge. Na vinanyongwa kwelikweli.

Unachotakiwa kufanya ni kubadili mtazamo. Toka kwenye mtazamo wa kuwa mnyonge, badala yake kuwa mpambanaji. Nimeandaa kabisa Mwongozo Wa Wapambanaji ambao na wewe unaweza kuupata. Mwongozo huu unapatikana kirahisi tu, wasiliana na 0684 408 755 sasa kupata mwongozo wako.

Kamwe usikubali kuwa mnyonge. Kuwa mpambanaji na mara zote pambania melengo na ndoto zako kubwa.

Kitu cha pili ambacho kiko hivyo ni kwamba, watu wote siyo sawa.

Ninavyoandika makala hii siyo kwamba nataka kuwa mbaguzi. hapana, ila nataka nikwambie tu ukweli.

Na hapa nitaeleza hasa kwenye eneo moja ambalo nalifahamu vizuri

Mfano kazini. Au ofisini, siyo wote ni sawa.

Ndiyo maana unakuta bosi anamlipa mtu fulani kiasi kikubwa cha fedha na mwingine kiasi cha kawaida, japo wote wanafanya kazi muda uleule. Kungekuwepo na usawa basi watu wote wangefanya kazi na kulipwa kwa usawa.

Kwenye timu ya mpira wa miguu kuna wachezaji kumi na moja, lakini malipo yao ni tofauti. Japo wote wanacheza dakika 90, ila kuna wanaolipwa zaidi na wale ambao wanalipwa kidogo. Hii ni kwa sababu hakuna usawa na usawa huu hauwezi kulazimishwa kuwepo, isipokuwa tu wewe unaweza kubadili mtazamo wako na kujiweka kwenye nafasi ya wale wanaopokea kikubwa badala ya wale wanyonge wanaongwa na kupokea kidogo.

wale wenye vipaji na upekee kwenye kucheza mpira wanalipwa zaidi.

Hivyo hivyo kwenye kazi

Mnaweza kuanza kazi sehemu mkiwa wawili. Mmoja baada ya muda akaongezewa mshahara, na pengine akapandishwa hata cheo, wakati mwingine akiwa bado anabung’aa. au pengine hata mwingine akafukuzwa.

Ukweli ni kuwa hakuna meneja ambaye huwa anafukuza mtu anayefanya vizuri. Meneja atafanya chochote kile anachoweza kuhakikisha kwamba mtu anayefanya vizuri anaendelea kubaki naye. Kama ni mshahara atamwongezea, kama ni bonus zaidi atamongezea.

Nakumbuka kuna siku nilisoma wasifu wa Strive Masiyiwa akawa anasema kwamba, aliwahi kumwachia mfanyakazi ambaye alikuwa anamfukuzia gari. Na yeye akatembea kwa mguu, hii ni kwa sababu alikuwa anamhitaji afanye kazi. Lakini tunaposema kwamba huyu mfanyakazi alimwachia gari, kuna watu ambao baada ya kuongea nao, alitamani asionane nao tena kwa sababu walikuwa hawafai.

Mtu ambaye hafanyi vizuri (mnyonge) ananyongwa haraka (kama ni kazini anaondolewa haraka) na ndiyo maana nilikwambia mapema kabisa kwamba kamwe kwenye maisha yako usikubali kuwa mnyonge maana watakunyonga na haki yako hutapewa.

Unachotakiw kuafanya ni kuhakikisha kwamba unakuwa mtu mwenye thamani kubwa. Ongeza thamani yako zaidi, na ukiwa mtu mwenye thamani, hakuna mtu atakayekupuuza. Kila mtu atahitaji kukaa karibu na wewe.

Unakuwa kama moto. Tunaupenda, kukiwa na baridi, tuna uhakika wa kupata joto. kukiwa chakula tuna uhakika wa kupika chakula chetu kwa wakati

Kwa kumalizia makala ya leo nipende kukusisitiza vitu viwili ambavyo nimeongelea siku ya leo. Kitu cha kwanz ani kwamba usikubali kuwa mnyonge la sivyo utanyongwa na haki yako hutapewa. Kitu cha pili ni kwamba usikubali kuwa mtu kawaida kwa kisingizio kwamba watu wote ni sawa. Huo usawa upo kwenye karatasi tu, ila kwenye uhalisia usawa haupo. Jitofautishe, kuwa mtu mwenye thamani kubwa, ni uhakika kwamba ukifikia hivi viwango watu hawataweza kukupuuza hata kidogo.

Utaweza kulipwa kwa namna unavyotaka. Na utaweza kupata chochote unachotaka hata hao wanaotoa hicho kitu watakuwa tayari kuwakosesha wengine.

watakuwa tayari kuwapunguzia wengine mishahara ili usiache kazi.

watakuwa tayari kukulipa mara mbili mpaka mara tatu zaidi ya wengine kwa sababu upekee wako.

watakuwa tayari kufanya lolote kwa niba yako

Utakula na wafalme.

mimi nakupenda


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X