Changamoto kubwa ambayo imekuwa inawakumba wafanyabiashara wengi ni kuchanganya pesa zao na pesa za biashara. Makala ya leo, inaenda kuwa mwarobaini wa hili.
Sikiliza uhusiano mkubwa uliopo kati yako wewe na biashara yako ni kwamba wewe ni mmiliki wa biashara, lakini fedha za biashara haupaswi kujimilikisha na kuzifanya kuwa za kwako. Fedha za biashara ni za biashara. wewe unapaswa kupata pesa kutoka kwenye biashara yako kwa njia mbili tu.
Njia ya kwanza ni kama mshahara, wewe kama mfanyakazi kwenye biashara yako basi unastahili kupata mshahara. na njia ya pili ya wewe kupata pesa kutoka kwenye biashara yako ni gawio au faida.
Nje na hapo fedha ya biashara ni ya biashara na fedha ya kwako ni ya kwako.
lakini si tunaanzisha biashara ili tupate fedha?
Najua unajiambia hivyo, ndio. ni kweli. ila sikiliza. Biashara yako ni kama kiumbe hai, inahitaji kula, inahitaji kupumua na inahitaji kukua. Endapo haitapata vitu muhimu kwa ajili ya biashara yako kukua, ukweli ni kwamba biashara hii haitakua.
Hivyo, usiibemende biashara yako kwa kuchukua hela za biashara ya kujimilikisha. Ziache fedha za biashara ziendelee kuwa za biashara
Tena biashara inapaswa kuwa na akaunti yake benki. Na wewe unapaswa kuwa na akaunti yako pia.
Hela yako ikae kwenye akaunti, na helaya biashara iwe kwenye akaunti yake. Usizichanganye.
Hapa najua unajiuliza mbona lakini muda mwingine huwa naongeza hela kwenye biashara, hili nalo limekaaje?
Ndiyo, kama unaongeza hela kwenye biashara maana yake kuna kitu umeona kwamba kikipata nguvu utakuja kupata faida zaidi hapo baadaye. Kama kwa sasa faida ulikuwa unapata milioni kwa wiki, maana yake unatazamia utapata milioni na nusu. Kitendo cha wewe kuongeza fedha kwenye biashara hakikupi wewe uhuru wowote wa kuifanya hela ya biashara kuwa ya kwako.
Najua unajiuliza swali jingine, kuwa je, kwa mfano, nikipata shida wakati hela ya biashara ipo nifanyeje?
Jibu langu ni kwamba, ukipata shida, tumia mshahara wako. Kama mshahara unaupata kutoka kwenye biashara yako haukutoshi, ongeza bidii ili mshahara huo uweze kupanda.
Ninaposema ongeza bidii maana yake, weka mkazo kwenye mauzo,ili uweze kuuza zaidi na hatimaye uweze kupata mshahara mkubwa zaidi kutoka kwenye biashara yako.
Sasa swali jingine unalojiuliza, ni je, nijilipe shilingi ngapi kutoka kwenye biashara yangu?
Jibu lake ni kwamba, kuna aina mbili za malipo ambayo unaweza kupata kutoka kwenye biashara yako.
Aina ya kwanza ni malipo ya mshahara ambao uko fixed. Yaani, unajiwekea kiwango maalumu cha mshahara ambacho utakuwa unapokea kila wiki au kila mwezi.
Ni muhimu kuhakikisha kwamba unakuwa na kiwango ambacho kitakuwezesha kukidhi mahitaji yako ya kila siku, ili usije ukajikuta umechukua hela ya biashara katikati ya wiki au mwezi.
aina ya pili ya kujilipa kwenye biashara, ni kwa kamisheni.
Hii ni njia nzuri kama utakuwa tayari kupambana na kuweka kazi zaidi. Hii itakupa changamoto ya kuisukuma biashara yako iende viwango vya juu mara zote. kama upo tayari kwa ajili ya hii changamoto, basi hii ndiyo njia bora kwako ambayo itakufaa kujilipa.
Kwa njia hii ni kwamba, unaweka kiwango cha mshahara wako kuwa asilimia ya mauzo unayokuw aumefanya. mfano unaweza kuweka asilimia tano au kumi. Hii inamaanisha kwamba kwa kila mauzo utakayofanya, utapata asilimia tano tu. Mfano ukifanya mauzo ya milioni moja, unapata kamisheni yako ya ya asilimia tano ambayo ni sawa na shilingi elfu hamsini. Ukijisukuma zaidi, maana yake utapata kamisheni kubwa zaidi na hivyo kuwa na mshahara zaidi.
najilipaje hiyo hela nachukua tu pale ninapopaswa kuchukua au inakuwaje yani?
Utaratibu wa kujilipa jilipe kama ambavyo ungekuwa unawalipwa wafanyakazi wengine. Jilipe hela kupitia akaunti ya benki. Toa kwenye akaunti ya benki kwenda akwenye akaunti yako, na matumizi yawe ni mshahara au kamisheni.
Una swali la ziada kuhusu hii mada ya leo. Kama lipo inawezekana swali lako limejibiwa kwenye kitabu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA. Hakikisha umepata kitabu hiki kizuri sana kwa kuwasiliana na +255 684 408 755. Fanya hivyo sasa hivi ili uweze kupata nakala yako,
La sivyo, mimi nakushukuru sana kwa muda wako siku ya leo. HAKIKISHA UMEJIUNGA NA WATU WANAOPOKEA MAKALA MAALUM KUTOKA KWANGU kila siku. Kujiunga, jaza taarifa zako hapa chini
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com