KIPAJI NI DHAHABU: Ila hapa kuna vitu vitano ambavyo kila mwenye kipaji anapaswa kufahamu


Juzi kuna mtu alinifuata kikashani kwangu whatsap na kuniuliza, mbona kijana yule mwenye kipaji ameshindwa kusaidiwa? 

Nilimwuliza kijana yupi? baadaye kidogo alinitumia picha za yule kijana pamoja na kazi alizofanya. 

Nilitakafari hili kidogo, ila nikaja kugundua kwamba watu wenye vipaji kuna vitu vitabo muhimu ambavyo hawafahamu.

Ningependa na wewe ufahamu hivi vitu, kuanzia leo hii, nina uhakika vitakuwa vitu vyenye manufaa makubwa sana kwako.

  1. kipaji ni dhahabu, ila ni ukweli kuwa kipaji hakitageuka kuwa dhahabu bila ya wewe kukifanyia kazi
  2. Usitegemee kamba kipaji chako kitaanza kukulipa siku hiyohiyo. Kinachukua muda.
  3. Ikitokea kipaji chako hakijakulipa, usikate tamaa na kuacha kukifanyia kazi. Kumbuka kwamba kila kitu huwa kina majira yake.
  4. Ni muhimu sana kufahamu misingi sahihi ya kutengeneza fedha kwa kutumia kipaji chako badala ya kuanza kusubiri watu waje wakufadhili, wakudhamini. Ukweli ni kuwa ukisubiri watu wa namna hii waje, unaweza kujikuta kwamba unakata tamaa na hata unashindwa kufanyia kazi kipaji chako kwa uhakika kabisa.
  5. inapotokea majibu uliyokuwa unategemea yaje haraka hayajatokea, usikate tamaa wala kuishia njiani. Endelea kupambania kipaji chako bila ya  kurudi nyuma. Kipambanie mpaka kieleweke

hayo ni mambo matano tu ambayo nilitaka uyajue kuhusu kipaji siku ya leo.

KIPAJI NI DHAHABU
Rafiki yangu, nimeandika kitabu. Kinaitwa KIPAJI NI DHAHABU. Ili kupata kitabu hiki, wasialiana na mi kwa +255684408755 sasa

Hakikisha umepata kitabu changu cha KIPAJI NI DHAHABU: Ni moja ya kitabu kizuri sana ambacho unapaswa kusoma. Kimeeleza kila kitu kuhusu kipaji na jinsi unavyoweza kutumia kipaji chako kwa manufaa.

Kupata nakala ya kitabu hiki hakikisha umewasiliana na 0684 408 755 sasa

SOMA ZAIDI:

  1. Sababu 15 kwa nini haupaswi kuwa na plan B
  2. Sababu Kumi Kwa Nini Haupaswi Kuongea Sana


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X