Madebe tupu huvuma


Leo kuna kauli mbili muhimu sana ambazo nataka tuzijadili kwa ufupi tu.

Kauli ya kwanza ni kauli ya wahenga watu wanaosema kwamba, madebe tupu huvuma.

Na kauli ya pili ni kauli inayosema kwamba, an idle mind is a devil’s workshop. ikiwa na maana kuwa akili tupu ni karakakana ya shetani.

hizi kauli zote mbili zinatusisitiza mimi na wewe kitu kimoja kikubwa sana. Na kitu hiki ni kufanya kazi.

Tunaishi katika dunia ambayo vijana na watu wengi hawapendi kufanya kazi. LAKINI WANAPENDA PESA.

Wanapenda kulipwa sana, LAKINI HAWAPENDI KUTOA THAMANI KUBWA.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba baadhi ya vijana unaweza kukuta kwamba wapo vijiweni wamekaa, wakiwa hawafanyi jambo lolote la maana la kuwaongezea aidha wao thamani au kuwaongezea kipato, lakini bado wanadharau kazi.

Ifike hatua ambapo wewe rafiki yangu, utapangilia ratiba yako na kuwa bize muda wote. Kuwa na fikra za kuchapa kazi mara zote.

ili uwe unachapa kazi mara zote, hakikisha mara zote unapangilia ratiba yako. Ratiba yako ndiyo njia pekee ya wewe kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako.

Kamwe rafiki yangu usikubali kuwa debe tupu! Na kamwe usikubali kuwa karakana ya shetani. Lengo la makala hii isiyo kukuhubiria, bali ni kukupa ukweli ambao utaufanyia kazi.

Ukweli ni kuwa kelele nyingi unazosikia kwenye maisha yetu ya kila siku. Iwe ni kwenye mitandao ya kijamii, kwenye vyombo vya habari au sehemu yoyote ile ni kutoka kwa watu ambao hawana kitu cha kufanya. Yaani, madebe tupu.

Kama kila mtu akiwa bize kuanzia leo hii. Tutaifanya hii dunia kuwa bora zaidi kuliko ilivyo sasa hivi.

Na njia bora ya dunia hii kuwa bora zaidi ni kwa mimi na wewe kuanza kutimiza wajibu wetu.

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X