Hii ndiyo Aina Ya Watu Ambao Siwapendi


Rafiki yangu wa ukweli.hongera sana kwa kazi na kwa siku hii ya kipekee. leo ni siku nyingine bora sana ambapo wewe unatakiwa kwenye kufanya kazi na kuzipambania ndoto zako kubwa pamoja na malengo yako makubwa. Ukweli ni kuwa, vile unaishi kwenye hii dunia, hauna kitu chochote kile ambacho kinapaswa kukukwamisha wewe kufanyia kazi malengo na ndoto zako kubwa. Mara zote unapaswa kuwa unaendelea kupambania malengo na ndoto zako kubwa bila ya kurudi nyuma.

Lakini pia unapaswa kuwa mtu mwenye fikra za kuona na kufikiri mbali.

Binafsi siwapendi sana watu ambao hawafikiri mbali. 

Napenda nijihusishe na watu wenye fikra za kufikiri na kuona mbali. Watu ambao wanaona kwamba wanaweza kufanyia kazi jambo fulani na wakalifanikisha, watu ambao wanafikiri kwa ukubwa na wanachukua hatua kufanyia kazi kile ambacho wanafikiri kwa ukubwa.

Ukweli ni kuwa hawa ndiyo napenda wanizunguke na hawa ndiyo napenda wawe marafiki zangu.

Ukiwa karibu na watu wa namna hii fikra zao, mitazamo yao na namna wanavyochukua hatua ni tofauti kabisa na watu wa kawaida.

Hawa wanaona uwezekano hata sehemu ambapo wewe unaona kwamba hakuna uwekezano. Hawa wanachukua hatua kubwa hata sehemu ambapo wengine wanaogopa kuchukua hatua.

Ushauri wangu kwako ni mmoja tu. Jihusishe na watu wenye fikra kubwa, watu ambao wanaona mbali na watu ambao wanafikiri kwa ukubwa. Na wala siyo watu ambao wanarudi nyuma au kufikiri kwa udogo.

Mara zote fikiri kwa ukubwa.

Mara zote zungukwa na watu wanaofikiri kwa ukubwa.

Ni haki yako kufikiri kwa ukuba

na wala hakukugharimu kitu chochote kile.

Nina kitabu kizuri sana ambacho kinaitwa NGUVU YA KUFIKIRI KWA UKUBWA.

Kama ulikuwa bado hujajipatia nakala ya kitabu hiki cha NGUVU YA KUFIKIRI KWA UKUBWA basi huu ndiyo muda wa wewe kufikiri kwa ukubwa rafiki yangu.

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X