Kosa Kubwa Ambalo Watu Hufanya Tunapozungumzia Kuhusu Kuweka Akiba


Salaam, tunapoongelea kuhusu kuweka akiba naona kuna kosa kubwa ambalo watu huwa wanafanya.

Wengi wanafikiri kwamba akiba wanayoweka leo hii inapaswa kuja kutumika baadaye kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Hili ni kosa kubwa sana.

Akiba siyo kwa ajili ya matumizi. Naomba uambatane nami sasa mwanzo mpaka mwisho ili nikueleweshe akiba ni kwa ajili ya nini.

Akiba ni mbegu

ili tuweze kuelewana vizuri kwenye hili, tuanze kuiona akiba kama mbegu, ambayo unaipanda leo hii siyo kwa ajili ya manufaa ya leo tu, bali hata kwa manufaa ya siku zijazo

Mbegu wewe unaipanda leo hii, baada ya miaka kadhaa itaanza kutoa matunda. hayo matunda yenyewe yatakuwa na uwezo wa kutoa mbegu, ambazo zikipandwa zitatoa miti mingine zaidi ambayo itatupa matunda.

Ukweli ni kwamba unapokula mbegu moja leo hii, unakuwa umekula matunda mengi ya siku zijazo.

Mbegu tunaweka kuziweka kwenye vizazi.

Kuna kizazi cha kwanza cha mbegu.

Unapokweka akiba ni kizazi cha kwanza cha mbegu.

lakini ukila akiba hiyo kabla haijakuzalishia, maana yake unakuwa umekula kizazi cha kwanza hata kabla hakijazaa matunda yoyote.

Unachotakiwa kufanya wewe ni kuhakikisha kwamba hauli kamwe kizazi chako cha kwanza cha mbegu. ile mbegu unapaswa kuipanda ili baadaye ije ikuzalishie zaidi na zaidi. Wewe utaanza kula kizazi cha tatu cha mbegu, huku kila kizazi kikiendelea kuleta matunda zaidi.

nimeona niliongelee hili kwa sababu inaonekana watu wengi hawajui sababu ya kuweka akiba, nimekuwa nikiongea na watu wengi kuhusiana na suala zima la kuweka akiba.

Unakuta baada ya kuwa umeongea nao kwa kina kuhusiana na suala zima la kuweka akiba, mwisho wa siku, wanakuja kusema kwamba,

Nikikosa pesa ya kula , naitumia ya akiba. Inanisaidia kwa sababu hata hivyo hiyo ndiyo kazi yake.

Siyo hivyo, unapofanya hivyo, maana yake unakuwa umekula mbegu kabla mbegu hizo hujapata nafasi ya kuzipanda ili zikuzalishie zaidi.

Kama wewe ni mkulima mzuri, utakuwa unafahamu kuwa mkulima makini, analazimika hata kulala njaa akiwa na mbegu yake ndani. Anajua wazi kuwa siku akila mbegu, maana yake mwakani hatakuwa na kitu cha kupanda, hivyo suluhisho ni kuhakikisha kwamba anatafuta njia mbadala ya kupata chakula, lakini mbegu inaendelea kuwa mbegu.

Hii ni akili ya kikulima ambayo mimi na wewe tunahitaji kuitumia kwenye maisha yetu ya kila siku. kwa hiyo usitumie akiba yako kama hela ya kula.

Chukulia akiba unayoweka kama fedha mbayo umeiweka sehemu na hutakaa uipate tena

kILA MARA MIMI NA WEW ETUNAFANYA MANUNUZI MENGI. Kuna wakati ambapo unalipia usafiri.

wakati mwingine unalipia nguo.

na wakati mwingine unalipia chakula.

Huwezi kwa mfano kuwa umelipia chakula, halafu ukarudi nyumbani ukakuta umeme umekatika, ukarudi kwa bodaboda na kumwambia akurudishie hela yako kwa sababu nyumbani hakuna umeme. Hiyo hela ukishampa bodaboda, hiyo hele ukishamlipa mtu wa chakula ndiyo inakuwa imeenda, haina kurudi nyuma hiyo. Hata kama ukikutana na dharula kubwa kiasi gani.

Hivyo hivyo, akiba yako ifanye hivyo mara zote. ICHUKULIE KAMA HELA AMBAYO UMEITUMIA KWA MATUMIZI AMBAYO HAYATAWEZA KUIREJESHA.

Unajiuliza sasa ikitokea dharula?

Kabla sijakujibu kwa undani kuhusiana na hili ningependa tufahamu hizi dharula unazoongelea hapa ni dharula gani? Lazima dharula ziwe zinafahamika kuwa ni zipi ni dharula na zipi siyo dharula. Usipokuwa na mpangilio mzuri kama huu, mwisho wa siku utajikuta kwamba kila kinachokuja kwenye maisha yako kinakuwa dhrula na mwisho wa siku utajikuta kwamba unaitoa na kuitumia akiba yako kila mara. HIKI KITU kitakukwamsiha kwa sababu kila mara utakuwa unapiga hatu amoja mbele na kisha unarudi nyuma

Kwa vile umeshaamua kusongambele na kuweka akiba bila ya kurudi nyuma, unapaswa kuhakikisha kwamba haurudi nyuma hata kidogo, badala yake unapaswa kuendele akuapmabana kila wakati ili usirudi nyuma

Ikitokea umekutana na dharula, jiulize nitatumia mbinu gani kupata pesa?

Ukiweka akiba chukulia kama hiyo pesa ya akiba haipo kabisa. Ni wazi kuwa ukiwa hauna hiyo hela, kwa vyovyote vile, ukiishiwa na pesa utakuwa hauna sehemu ya kutoa pesa ya kutumia . Hivyo utafikirisha kichwa na kuona ni wapi ambapo unaweza kupata fedha zaidi ambazo utatumia.

NA WEWE SASA UNAPASWA KUFIKIRISHA AKILI YAKO BILA YA KURUDI NYUMA.

Sasa akiba ITUMIKE KUFANYA NINI?

Kama ambavyo tumeshaongelea mwanzoni, akiba iwekezwe ili ije ikupe matunda mengi zaidi hapo baadaye. Akiba ipandwe.

Nashauri ujipatie nakala ya kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE, pamoja na kitabu cha MAAJABU YA KUWEKA AKIBA

Hivi ni vitabu ambavyo ni muhimu sana uweze kuvipata.

Wasiliana nami kwa ++255 684 408 755

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X