Kuongeza Kipato Chako Mara Mbili Inawezekana. Vitu Vitano Ambavyo Unapaswa Kuzingatia


Rafiki yangu wa ukweli salaam, hongera sana kwa siku hii nyingine ya kipekee sana. Siku ya leo ningependa kukushirikisha namna ambavyo unaweza kuongeza kipato chako mara mbili. Hiki ni kitu ambacho kinawezekana.

Ili uweze kunielewa vizuri. Naomba nianze kwa kukwambia kwamba kama unaingiza shilingi elfu moja kwa siku, jua wazi kuwa unaweza kuingiza elfu kumi.

Na kama unaingiza elfu kumi kwa siku, jua wazi kuwa unaweza kuingiza kipato kama hicho au zaidi kwa mwezi.

Ukweli ni kuwa kiwango cha kipato ambacho unaingiza kwa sasa hivi, unaweza kuikiongeza. Inawezekana vizuri sana.

Sasa utakuwa unajiuliza, inawezekanaje. Yafuatayo ni mambo ya muhimu sana ambayo unatakiwa kuzingatia.

Kwanza, kuwa na lengo ambalo unataka kufikia. Ndiyo, namaanisha lengo ambalo unalifanyia kazi na ungependa kulifikia. Hiki ni kitu cha kwanza kabisa, kwa sababu bila ya kuwa na lengo, ni wazi kuwa utakwama na utashindwa kufanyia kazi lengo lako mpaka likatimia.

Pili, heshimu hicho kiasi kidogo ambacho unaingiza sasa hivi. Kuna watu wengi wanaona kwamba kiasi wanachoingiza kwa sasa kama hakifai vile. Hapana, unapaswa kuheshimu kiasi ambacho unaingiza kwa sasa hivi, kwa maana hicho kiasi kidogo ndiyo kitakupelekea kwenye kuingiza kiasi kikubwa zaidi.

Tatu, kutoka kwenye kiasi unachoingiza sasa hivi, anza kuweka akiba. Akiba hii unayoiweka sasa hivi, ndiyo itakusaidia baadaye wewe kuweza kuanzisha biashara au kitu unachopenda kufanya.

Nne, kama hauna biashara, anzisha biashara. Kisha isimamie vizuri hii biashara kwa kuhakikisha kwamba mara zote unafuata misingi sahihi ya kuendesha biashara yako.

Tano, kama tayari una biashara au ujuzi fulani au kipaji. Ongeza thamani kwenye kitu unachofanya, ili kiwe cha thamani kubwa zaidi. Kamwe usikubali chochote kile unachofanya kukifanya katika namna ya ukawaida. Badala yake hakikisha kwamba kazi yoyote ile ambayo unaifanya, unaifanya kwa viwango vikubwa haswa.

Sita, mara zote jifunze. Kujifunza ni tiketi ya wewe kuendeleza ujuzi ulio nao. Kujifunza, kutakupelekea wewe kujitofautisha mwenyewe. Kufanya mambo ya tofauti na kukuza kitu unachofanya ili kiweze kwenda kwenye viwango vikubwa zaidi.

Saba, Usikimbizane na kila fursa ambayo inakuja mbele yako. Badala yake pambana kwanza na kitu kimoja ambacho unafanyia kazi sasa hivi, maana hiki ndiyo kitakuja kuwa tiketi ya wewe kufanya makubwa zaidi hapo baadaye.

Nane, tengeneza mtandao mzuri wa kifedha. Lakini pia hakikisha kwamba unakuwa na nidhamu ya fedha ambayo inaingia kwenye kitu unachofanya. Ukiongeza kipato chako, kamwe usikimbilie, kukitumia na kukifuja chote, badala yake juhudi kubwa zaidi ziendelee kuwekwa kwenye kuongeza kipato zaidi na zaidi.

Rafiki yangu, anza kutumia haya niliyokwambia hapa siku ya leo. Kitu kikubwa unachopaswa kuondoka nacho hapa ni kwamba unapaswa kuanza kufanyia kazi haya uliyojifunza hapa.

Usipoyafanyia kazi haya, hutapata matokeo yoyote.

Halafu nina programu nzuri sana ambayo itakusaidia wewe kuongeza kipato chako mara mbili zaidi ya sasa. Programu hii unaweza kuipata kwa shilingi 50,000/- tu. Lipia sasa kwa 0684 408 755.

Pia, usisahau tutakuwa na semina. Maelekezo ya semina haya hapa

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X