Naomba kuanzia leo hii uanze kumfuatilia mtu huyu, hutajutia…


Naomba kuanzia leo hii uanze kumfuatila mtu huyu, hutajutia…

Moja ya kitu ambacho watu wengi wanakosea ni kufuatilia maisha ya watu wengine kuliko wanavyojifuatilia maisha yao binafsi. Ninachotaka ufanyie kazi rafiki yangu kuanzia leo ni kuanza kujifuatilia maisha yako mwenyewe.

Inawezekana moja ya kitu kinachokufanya wewe ufuatilie maisha ya watu wengine ni kwa sababu haujijui.

Hauju ni kitu gani unapaswa kufanya.

Haujui ni kipaji gani ulichonacho.

Hiki kitu kinakupelekea wewe kufuartilia maisha ya watu wengine., unafuatilia wengine wanaishije, unafuatilia wengine wanakula nini na mengine mengi.

Huyo hapaswi kuwa wewe.

Leo jipe kazi moja tu. Kazi ya kujifuatilia wewe mwenyewe. Kwamba wewe ni nani, kwa nini uko hapa duniani na nini haswa ambacho unapaswa kuwa unafanyia kazi? Jipe hili jukumu rafiki yangu, nina uhakika kwa kujifahamu mwenyewe utaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Hakuna ukuaji wowote utakaoupata kwa kufuatilia maisha ya watu wengine. Lakini utaweza kupata ukuaji mkubwa kwa kitendo cha kujifuatilia mwenyewe tu. Hivyo, jifuatilie mwenyewe kwanza.

SOMA ZAIDI: Mfuatilie huyu jamaa kwa mwezi mmoja tu, wewe mwenyewe utaniambia utakachoona

Umekuwa name rafiki yakow a ukweli

Godius Rweyongeza

Nifuatilie youtube kupitia hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X