Kama Isingekuwa Pesa, Ungekuwa Unafanya Unachofanya sasa


Ndugu Godius Rweyongeza
Ndugu Godius Rweyongeza

Anaandika GODIUS RWEYONGEZA

Wasiliana naye wasap hapa

Mwaka juzi taarifa zilisambaa mtandaoni kwamba mchungaji mmoja huko nchini Uganda ameacha uchungaji baada ya kushinda milioni 100 kupitia kubeti. Kwa maneno yake huyu mchungaji alisema kwamba alikuwa anafanya kazi ya uchungaji kwa sababu hakuwa na fedha.

Hiki kinatafakarisha sana. Kumbe tuna watu wanafanya vitu ambavyo hawapendi, na kila siku wanalazimika kwenda kufanya shughuli wanazofanya ila moyoni mwao hawapendi hivyo vitu.

Je, wewe umo?

Mtu mmoja alisema kwamba biashara za kitanzania ni ngumu sana. Kwa sababu pale biashara zinapoanza kupata faida inayoeleweka, ndipo watu wanataka kupata pesa zao na kuondoka kwenye biashara hizo badala ya kurudisha faida kwenye biashara. Kumbe kitu cha kwanza kilichokuwa kimewapeleka kwenye biashara hiyo si kutoa huduma, siyo kutatua matatizo yanayowakumba watu, bali ni pesa.

Sasa swali llangu kwako siku ya leo ni kwamba kama isingekuwa pesa, je, unachofanya sasa hivi ungekuwa unakifanya? Najua utanza kusema sasa nitaishije bila yakuwa na pesa. Ni ukweli usiopingika kuwa pesa ni muhimu na inahitajika sana.

Ila unatakiwa kupenda unachofanya.

Kupenda unachofanya ni hatua moja mbele ukilinganisha na pale unapofanya usichokipenda.

Kuna siku unaweza kuwa siku hiyo hujisikii kufanya kazi. Ila ukiwunapenda unachofanya utaendelea kupambana.

SOMA ZAIDI: Kauli Yenye Nguvu: Ni bora Ufe Ukiwa unafanya unachopenda…

Sasa kwenye makala ya leo tujadiliane vitu vitano vinavyopaswa kukusukuma kufanya kazi au biashara. Hii siyo kwa sababu hatutambui umuhimu wa fedha. Itambulike umuhimu fedha. lakini kwa hapa tuzungumzie hili. 

sababu ya kwanza ni kutimiza kusudi lako. kila mmoja ana kusudi kubwa ambalo limemfanya awepo hapa duniani. 

  1. Kutimiza kusudi la kuwepo hapa duniani

Kila mtu ameumbwa kwa kusudi fulani. Kazi au biashara unayofanya inapaswa kuwa sehemu ya kutimiza kusudi hilo. Unapofanya kazi kwa kuelewa kwamba unatekeleza wito wa maisha yako, hutachoka kirahisi, wala hutafanya mambo kwa kubahatisha.

2. Kuwahudumia watu na kutatua changamoto

Biashara na kazi yoyote yenye mafanikio makubwa inasimama juu ya msingi wa kutatua matatizo ya watu. Ukizingatia kusaidia na kuhudumia wengine, thamani yako itaongezeka, na kwa hakika pesa zitaingia kama matokeo.

3. Kujenga historia

Kila siku unayofanya kazi au biashara, unajenga hadithi yako ya maisha. Je, utataka watu wakikukumbuka waseme uliishi tu kwa ajili ya kutafuta fedha, au watasema ulileta mabadiliko makubwa? Kufanya kazi kwa lengo la kuacha alama ni nguvu ya pekee ya kukusukuma kila siku.

4. Kukuza vipaji

Kazi na biashara ni shule kubwa zaidi ya maisha. Inakupa nafasi ya kutumia kile kilicho ndani yako na pia kujifunza zaidi. Unapoliona hilo kama msukumo, utathamini kila changamoto na fursa kama nafasi ya kukua na kuwa bora.

 

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza

Jipatie vitabu vya Godius Rweyongeza kwa kuchagua HAPA.

Wasiliana nami wasap hapa

Hakikisha umepata kitabu cha RASILIMALI ZA WATU WENGINE, ni kitabu kizuri kwa ajili yako. wasiliana na 0755848391 au 0745848395 sasa

Makala ya kesho itawekwa kwenye blogu ya SONGAMBELE ambayo unaweza kuifikia kupitia www.songambele.co.tz na itawekwa kwenye channel ya telegram pia ambayo unaweza kuifikia kwa KUBONYEZA HAPA

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X