KHERI YA MWEZI SEPTEMBA: MWAKA 2025 HAUJAISHA MPAKA UISHE


Leo ni tarehe 1.9.2025, ni siku ya 244 tangu tuuanze mwaka huu wa kipekee, inawezekana mwaka huu uliuanza kwa mbwembwe nyingi, lakini sasa tunapokaribia mwishoni mwa mwaka huu ukijitafakari unajiona wapi? Ni hatua zipi ambazo umeweza kupiga mpaka sasa, ni wapi unaelekea.

Ukweli ni kuwa hata kama mwaka huu unaonekana kwenda, hii haimaanishi kwamba huwezi kufanya kitu kwa siku hizi ambazo zimebaki. Bado unaweza kufanya kitu kikubwa sana rafiki yangu. Kikubwa zingatiai yafuatayo.

MOJAJ, MWAKA HAUJAISHA MPAKA UISHE

Kwenye mpira wa miguu, mpira huwa hauhesabiki kuwa umeisha mpaka pale kipenga cha mwisho kinapokuwa kimepulizwa. Hivyo hivyo kwenye mwaka huu, hatuwezi kusema kwamba mwaka huu umeisha, mpaka pale tutakapokuwa tumeuanza mwaka mwingine. Hivyo basi, ni muhimu kwako kufahamu kuwa kila siku inayokuja mbele yako inapaswa kuhesabiwa kwa ushindi mkubwa na kamwe usibaki nyuma, bali ipambanie kila siku ijayo mbele yako kuanzia sasa nakuendelea.

MBILI,  UJUE WAPI UNAENDA NA KW ANINI UNAENDA HUKO.

Hakuna kitu kinasikitisha kama mtu kuwa unaenda safari, ili hali safri hiyo siyo safari sahihi kwako. Yaani, unazunguka tu huku na kule bila ya kuwa na mwelekeo wa maana, ukweli ni kuwa kwa kuwa zimebaki siku chache kuelekea mwisho wa mwaka, basi zitumie siku hizi vizuri kwa kuhakikisha kwamba, unafanya yale ambayo umepanga. Kamwe usifanye vitu ambavyo siyo sahihi ndani ya hizi siku ambazo zimebaki kuelekea mwisho wa mwaka. Kuwa na malengo na yafanyie kazi bila kusita wala kurudi nyuma. Kumbuka, mwaka huu bado haujaisha mpaka utakapokuwa umeisha.

SOMA ZAIDI: Nini Cha kufanya unapokutana na changamoto.

TATU, PANGILIA KILA WIKI YAKO KIPROFESHONO

Huuu ni muda mzuri wa wewe kupangilia kila wiki yako kiprofoshono. Yaani, kila wiki inayokuja mbele yako unahakikisha kwamba umeweza kufanya makubwa. Kamwe usikubali wiki yoyote ile ipite mbele yako bila ya wewe kufanya jambo ambalo ni la maana sana. Kila wiki ni kipekee na itumie hivyo.

NNE, AMUA KUWEKA KAZI MBELE

Ni kazi pekee ambayo inaweza kukupa ushindi wa kweli na unaodumu. Amua kwamba kwa muda na kwa kipindi hiki unaenda kuweka kazi mbele na kazi pekee ndiyo inaenda kuwa kipaumbele kwako mara zote.

SOMA ZAIDI: Kazi ni nini?

TANO, JICHAGUE MWENYEWE KWANZA

Kipindi cha miezi mitatu ijayo ni kipindi ambacho pia ndani yake tutakuwa na siasa nyingi, muda huu ni muda wa kujichagua mwenyewe pia kwa sera zako utakazoweka. Sera zako za maisha yako ni zipi. Jiwekee sera nzuri utakazoenda kuishi nazo kwa miaka mitano inayokuja.

SOMA ZAIDI: KONA YAA SONGA MBELE; IKO WAPI MOTISHA YA JANUARI MOSI?.🤷🏽‍♂🤷🏽‍♂

Rafiki yangu, haya ni mambo ya msingi sana ambayo unatakiwa kuzingatia kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Karibu sana.

Ni mimi rafiki yako wa ukweli

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tanzania

Jipatie vitabu vya Godius Rweyongeza kwa kuchagua HAPA.

Wasiliana nami wasap hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X