-
Unapokosea Wewe Ni Hapa
Kwenye makala ya Jana nilisema kwamba kabla hujamchagua kiongozi yeyote mwaka huu, JICHAGUE MWENYEWE kwanza. Una dira ya miaka mitano ijayo, kama huna iweke Kisha JICHAGUE na kila siku ukiamka kwa miaka mitano itekeleze.
Sasa Moja ya KITU ambacho Watu wanajiambia ni kuwa nikifa je? Ni bora nisiweke mipango ya miaka mitano maana naweza kufa.
Ukweli ni kuwa
Ukweli wa kwanza: wanaoweka mipango siyo kwamba hawafi na hatuweki mipango kwa sababu hatuji kufa.
Ukweli wa pili: kutokuweka mipango kunakuweka kwenye nafasi ya kufa haraka kweli. Unaweza kudhani kujiambia ajuaye kesho ni Mungu ni njia nzuri ya kuishi, ila ukweli ni kuwa unajiua. Iko hivi, unapokuwa na mipango maana yake unaenda kuwa bize muda wote. Unaepuka vishawishi, unaepuka vitu ambavyo vinaweza kukuingiza matatani, ila unapokuwa huna malengo, kila kitu kinakuwa lengo kwako. Kuna wakati unaweza kujikuta unajadili mambo ya watu, si unajua akili tupu ni karakarana ya shetani.
Iko hivi, kama huna mipango, maana yake huna Kusudi la kufanyia kazi na watu ambao hawana Kusudi hufa mapema. Hivyo, kutokupanga ni kupanga kujiua.
Ukweli wa tatu: unambebesha Mungu mzigo ambao sio wake.
Kuna watu kila kitu wanasema Mungu anajua, yaani mpaka wanamfanya Mungu anajuta kuwaumba. Hawawezi kufanya maamuzi yoyote, hawawezi kuchukua hatua pale wanapotakiwa kufanya maamuzi, wanachofanya ni kwamba wanasubiri tu Mungu afanye.Ninachotaka wewe ufahamu ni kuwa ni kweli Mungu anafanya pale na wewe unapofanya. Usimbebeshe Mungu mzigo ambao unapaswa kuufanya wewe. kazi ya kuweka malengo na mipango ni ya kwako. Hiyo usimbebeshe Mungu, ibebe wewe mwenyewe. Kazi ya kuibadili kesho yako na kutengeneza kesho bora ni ya kwako. Ni jukumu lako kuhakikisha kwamba unalipambania hili suala.
Kesho inayong’aa inatengenezwa sasa hivi.SOMA ZAIDI: AMSHA UUNGU ULIO NDANI YAKO: Sifa 3 Za Kimungu Unazopaswa Kuzitumia Kuanzia Leo
Imeandikwa nami rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz -
Mchague Huyu Mtu. KURA YAKO UTAKUWA UMEITUMIA VIZURI SANA
Mwaka 2025 kwa hapa kwetu Tanzania ni mwaka wa UCHAGUZI. Na tayari hivi ninavyoandika hapa kampeni zimeanza nchi nzima. Wagombea wote wanajinanadi uwachague waende kukuwakilisha kwa miaka mitano ijayo.
Mtu yeyote anayekuja kwako kuomba kuchaguliwa lazima tu atakuja sera. Atakuuzia wewe sera, ukiona zinafaa maana yake utanunua hizo sera kwa kumpigia kura.
Unapomchagua mtu yeyote, maana yake unampa mamlaka ya kwenda kutekeleza sera hizo kwa kipindi cha miaka mitano. UCHAGUZI Huwa ni KILA BAADA YA MIAKA MITANO.
Kwa nini miaka mitano?
Iko hivi, miaka mitano ni kipimo ambacho tunaenda kuona kama mtu alichoahidi amekifanyia kazi au la. Hii ndiyo kusema kwamba yeyote anayechaguliwa anapewa MUDA wa kutosha kufanilisha jambo lake kwa sababu MAFANIKIO ni mchakato. Si KITU Cha siku Moja au mbili.MALENGO+MUDA=MAFANIKIO
Ndiyo maana malengo yanahitaji muda, na wanaochaguliwa wanapewa muda wa kutekeleza sera zao.
Tunahitaji tuchague Watu wazuri wa kutuongoza na hapa nataka nikwambie mtu mmoja ambaye unapaswa kumchagua kwa uhakika. Mtu huyu atakufaa sana.
Unajua ni nani huyu?
Nisikilize kwa haya kwanza.
Iko hivi, unapomchagua diwani, mbunge au rais maana yake unakuwa umempa kazi. Kwamba KILA siku ukiamka fikiria kuhusu haya unayoniambia, na kila siku ukienda kulala, fikiria kuhusu hayahaya.
Yaani, kazi yake ni hiyo. Anapaswa kuachana na mengine yote na kuweka NGUVU kubwa kwenye sera au ilani aliyotoa.
Sasa twende kwa mtu unayepaswa kumchagua. Mtu huyu si mwingine Bali ni wewe. Unapaswa kujichagua KWANZA. JICHAGUE MWENYEWE 2025
Kivipi? Pengine unajiuliza yaani Mimi najichaguaje? Mbona Sina sera wala ilani yoyote?
Na hapa ndipo narudia tena kwa kusema kwamba JICHAGUE MWENYEWE. Ni mambo yapi ambayo kila siku kwa miaka mitano ijayo, kila utakapokuwa unaenda kulala utakuwa ukiyafikiria, na ni mambo yapi kwa miaka mitano ijayo kila ukiamka utakuwa ukiyafikiria. Hizi ndizo sera zako
Kabla hujaenda kumpigia kura diwani yoyote. Kabla hujaenda kumpigia kura mbunge wala rais, JICHAGUE. Unajichagua vipi?
Kuwa na sera au ilani? Yaani MALENGO Yako unayoenda kuyafanyia kazi usiku na mchana kwa miaka mitano ijayo. Ikumbukwe tokea mwanzo ninesema kwamba unapomchagua kiongozi maana yake KWA miaka mitano ijayo KILA akiamka anakuwa anafanyia kazi sera au ilani zake Ili zitimie.
Sasa swali langu kwako siku ya Leo ni kwamba SERA ZAKO ZA MIAKA MITANO IJAYO NI ZIPI? MALENGO YAKO AMBAYO YATAKUAMSHA KILA SIKU UKIENDA KUYAPAMBANIA NI YAPI?
Kama huna haya, hii miaka mitano inaenda kupiga, utakuwa hujafanya chochote Cha maana, na kama kulalamika utakuwa unalalamika maisha magumu. Ukweli mchungu ni kwamba bila kujali ni kiongozi Gani ynaenda kumchagua, kama wewe mwenyewe huna MALENGO Yako ya kutoboa, huyu kiongozi hata kufanya utoboe. Ni mpaka pale utakapokuwa na malengo Yako.
Bahati wanakutana nayo walio kwenye mwendo na siyo wale waliotulia.Unapoweka MALENGO maana yake umeamua kuwa kwenye mwendo.
Sasa hata kama huna MALENGO basi kwa miaka mitano ijayo, hakikisha unafanyia kazi haya MALENGO
MOJA, KUAMKA MAPEMA. Niwekee utaratibu wa kuamka walau saa 11 kwa miaka mitano ijayo na siyo zaidi ya saa 12 KASORO.
MBILI, KUSOMA VITABU, kwa miaka mitano ijayo soma walau kurasa kumi za kitabu KILA siku. Hii itakusaidia
TATU, KUWEKA AKIBA, kwa miaka mitano ijayo weka akiba walau ya sh elfu Moja tu KILA siku.
NNE, KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI Au VIPANDE. Kwa miaka mitano ijayo, chagua KUWEKEZA pia. Anza na Uwekezaji kwenye HISA na siku hizi unaweza kununua hisa kiganjani mwako kupitia app ya DSE KIGANJANI.
TANO KUFANYA KAZI KWA BIDII, kwa miaka mitano ijayo, chagua kuwa kazi ndiyo kitu pekee ambacho kinaenda kukutambulisha. Kazi huwa haidanyanyi na kamwe usifeli kwenye hilo.
Nakuhakikishia BAADA ya miaka mitano utakuwa mmoja wa Watu watakaokuwa wanamiliki uchumi wao wa maana.
Rafiki yangu, tunayo miaka mitano ya uhakika mbele yetu. Ni au uchague kuitumia vizuri au la unaenda kuipoteza. Chagua kuitumia vizuri Sasa.
Imeandikwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza
Karibu sana.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
Jipatie vitabu vya Godius Rweyongeza kwa kuchagua HAPA.
Hakikisha umepata kitabu cha RASILIMALI ZA WATU WENGINE, ni kitabu kizuri kwa ajili yako. wasiliana na 0755848391 au 0745848395 sasa
Makala ya kesho itawekwa kwenye blogu ya SONGAMBELE ambayo unaweza kuifikia kupitia www.songambele.co.tz na itawekwa kwenye channel ya telegram pia ambayo unaweza kuifikia kwa KUBONYEZA HAPA
-
KHERI YA MWEZI SEPTEMBA: MWAKA 2025 HAUJAISHA MPAKA UISHE
Leo ni tarehe 1.9.2025, ni siku ya 244 tangu tuuanze mwaka huu wa kipekee, inawezekana mwaka huu uliuanza kwa mbwembwe nyingi, lakini sasa tunapokaribia mwishoni mwa mwaka huu ukijitafakari unajiona wapi? Ni hatua zipi ambazo umeweza kupiga mpaka sasa, ni wapi unaelekea.
Ukweli ni kuwa hata kama mwaka huu unaonekana kwenda, hii haimaanishi kwamba huwezi kufanya kitu kwa siku hizi ambazo zimebaki. Bado unaweza kufanya kitu kikubwa sana rafiki yangu. Kikubwa zingatiai yafuatayo.
MOJAJ, MWAKA HAUJAISHA MPAKA UISHE
Kwenye mpira wa miguu, mpira huwa hauhesabiki kuwa umeisha mpaka pale kipenga cha mwisho kinapokuwa kimepulizwa. Hivyo hivyo kwenye mwaka huu, hatuwezi kusema kwamba mwaka huu umeisha, mpaka pale tutakapokuwa tumeuanza mwaka mwingine. Hivyo basi, ni muhimu kwako kufahamu kuwa kila siku inayokuja mbele yako inapaswa kuhesabiwa kwa ushindi mkubwa na kamwe usibaki nyuma, bali ipambanie kila siku ijayo mbele yako kuanzia sasa nakuendelea.
MBILI, UJUE WAPI UNAENDA NA KW ANINI UNAENDA HUKO.
Hakuna kitu kinasikitisha kama mtu kuwa unaenda safari, ili hali safri hiyo siyo safari sahihi kwako. Yaani, unazunguka tu huku na kule bila ya kuwa na mwelekeo wa maana, ukweli ni kuwa kwa kuwa zimebaki siku chache kuelekea mwisho wa mwaka, basi zitumie siku hizi vizuri kwa kuhakikisha kwamba, unafanya yale ambayo umepanga. Kamwe usifanye vitu ambavyo siyo sahihi ndani ya hizi siku ambazo zimebaki kuelekea mwisho wa mwaka. Kuwa na malengo na yafanyie kazi bila kusita wala kurudi nyuma. Kumbuka, mwaka huu bado haujaisha mpaka utakapokuwa umeisha.
SOMA ZAIDI: Nini Cha kufanya unapokutana na changamoto.
TATU, PANGILIA KILA WIKI YAKO KIPROFESHONO
Huuu ni muda mzuri wa wewe kupangilia kila wiki yako kiprofoshono. Yaani, kila wiki inayokuja mbele yako unahakikisha kwamba umeweza kufanya makubwa. Kamwe usikubali wiki yoyote ile ipite mbele yako bila ya wewe kufanya jambo ambalo ni la maana sana. Kila wiki ni kipekee na itumie hivyo.
NNE, AMUA KUWEKA KAZI MBELE
Ni kazi pekee ambayo inaweza kukupa ushindi wa kweli na unaodumu. Amua kwamba kwa muda na kwa kipindi hiki unaenda kuweka kazi mbele na kazi pekee ndiyo inaenda kuwa kipaumbele kwako mara zote.
SOMA ZAIDI: Kazi ni nini?
TANO, JICHAGUE MWENYEWE KWANZA
Kipindi cha miezi mitatu ijayo ni kipindi ambacho pia ndani yake tutakuwa na siasa nyingi, muda huu ni muda wa kujichagua mwenyewe pia kwa sera zako utakazoweka. Sera zako za maisha yako ni zipi. Jiwekee sera nzuri utakazoenda kuishi nazo kwa miaka mitano inayokuja.
SOMA ZAIDI: KONA YAA SONGA MBELE; IKO WAPI MOTISHA YA JANUARI MOSI?.🤷🏽♂🤷🏽♂
Rafiki yangu, haya ni mambo ya msingi sana ambayo unatakiwa kuzingatia kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Karibu sana.
Ni mimi rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tanzania
Jipatie vitabu vya Godius Rweyongeza kwa kuchagua HAPA.
-
Kuandika ni Kutunza Kumbukumbu
Marcus Aurelius alikuwa na utaratibu wa kuandika kwenye notebook (tuiite hivyo) kila siku. Kila siku aliandika kitu alichojifunza, iwe ni kitabuni au kutoka kwa watu aliokutana au katika vyanzo vingine.
Kile ambacho mwanzoni alikuwa anaandika kwa ajili yake, baadaye kilikuja kuonekana ni cha msaada mkubwa, mpaka maandiko yake yakakusanywa kwenye kitabu kimoja ambacho leo hii kinafahamika Kama Meditations.Huwa napenda kuwaambia watu kuwa kwenye maisha haya kila mmoja ana jambo lake anaweza kuandika kwa ajili yake mwenyewe, familia, au hata kwa ajili ya wengine.
Naomba unisikilize rafiki yangu. Huhitaji kuwa Reginald Mengi ili uandike kitabu chako.
Inawezekana watoto wako tu kuna vitu hawajui kuhusu wewe. Sasa itakuwaje,
Hilo mimi nina uhakika nalo.
UNAPOANDIKA KITABU, unatoa nafasi ya mambo yako na historia kuendelea kujulikana kwa urahisi hata kwa miaka mingi ijayo.
Mimi nina uhakika, sambamba na mali zote utakazoacha, moja ya kitu ambacho wajukuu wako watajivunia, ni kitabu utakachokuwa umeandika. Mfano, kama mimi babu yangu angekuwa ameandika kitabu. Ningekuwa naringa sana hapa mjini. Kwanza historia yake ambayo huwa nasimuliwa nusunusu kila siku, ningeipata kwa ukamilifu bila chenga. Hili lingekuwa ni jambo zuri sana kwangu.
Mfano mdogo tu, tuchukulie historia yako. Kuna watu huwa wanafikiria kwamba ili aandike historia ya maisha yake anapaswa kuwa maarufu sana. Wengi hutolea mfano wa Mengi au Mkapa na kuonesha kwamba wanapaswa kuwa kwenye viwango hivyo ili waandike vitabu.
Wewe pia itakuwa hivyo endapo hutaandika kitabu. Wajukuu wako watakuwa wanahadithiwa historia kidogo kidogo. Vistori ambavyo havina kichwa wala miguu na hivyo hawataweza kujua historia yako kamili. Ila kama utakuwa umeiandika, wataiona kwa uzuri.
Hivyo, fikiria kuhusu kuandika kitabu cha historia ya maisha yako mara moja.
Sasa kama ungependa kupata mwongozo wa kuandika kitabu
Usimamizi
au hata kuandikiwa kitabu chako
Nitumie namba yako ya simu sasa hivi ili tuweze kuwasiliana.
Tuma namba yako ya simu kwa kujibu email hii. Asante sana -
Mafanikio Katika Biashara
Ili uweze kufanikiwa katika biashara yako kuna mbinu na hatua za kufuata. Ndani ya ebook hii kuna mbinu na hatua madhubuti za kuzingatia katika mafanikio ya biashara yako. Soma kupitia hapa
Zingatia mambo yafuatayo
soma zaidi; Kitu Kinachofanya Mabadiliko Kuwa Magumu Kwenye Biashara Yako
-
Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuongez Kujiamini
Rafiki yangu mpendwa, watu wengi wamekuwa wanahangaika sana na kujiamini. wengi huwa wanakosa kujiamini hasa wanapokuwa mbele ya watu. Kwa kulifahamu hilo, nimeandaa ebook fupi yenye suluhisho juu ya hili tatizo ambalo limekuwa linawakumba watu wengi. Ebook hii unaweza kuipata kirahisi sana kupitia link hii hapa
BONYEZA HAPA KUPATA EBOOK yako
Asante sana
-
Ushauri wa Bilionea Pavel Durov Kuhusu Kozi Ya Kusoma Chuo
Pavel Durov ambaye ni bilionea na mwanzilishi wa telegram kwenye channel yake ya telegram ametoa ushauri kwa wanafunzi ambao wanatafuta kitu gani cha kusoma.
Anasema hivi,
Ikiwa wewe ni mwanafunzi unayechagua nini ubobee, basi chagua HESABU. Itakufundisha kutegemea akili yako mwenyewe bila kuchoka, kufikiri kwa mantiki, kugawa matatizo vipande vipande, na kuyatatua hatua kwa hatua kwa mpangilio sahihi. Huo ndiyo ujuzi wa msingi utakaohitaji kujenga kampuni na kusimamia miradi.
Huu ni moja ya ushauri muhimu sana hasa ukizingatia bilionea huyu ni mwanzilishi wa kampuni kubwa na kabla ya hii aliwahi kuanzisha kampuni nyingine.
Bilionea huyuhuyu siku za nyuma aliwa kusema kwamba wachina wanafanya vizuri kwenye sekta nyingi kwa sababu hesabu wamezipa kipaumbele kwenye mfumo wao wa elimu na hivyo akawa anashauri nchi mbalimbali kuiga mfumo wa elimu wa china
WEWE UNA MAONI KUHUSIANA NA HIKI ANACHOSEMA DUROV?
-
Jinsi Ya Kuandika Kitabu Kirahisi Hata Kama Uko Bize
Kuandika kitabu ni ndoto ya watu wengi, lakini mara nyingi hukwamishwa na sababu moja kubwa: “Sina muda.” Lakini je, kweli muda ni kikwazo au ni kukosa mbinu sahihi za kutumia muda tulio nao? Siku za nyuma nimewahi kuandaa video YouTube yenye kichwa cha “Jinsi ya kuandika kitabu kirahisi hata kama uko bize”, kama hujawahi kuiangalie itazame tena hapa. Ila kwa Leo ningependa nikushirikishe haya.
- Una dhamira ya kuandika kitabu?
Kabla hujashika kalamu au kufungua kompyuta, jiulize: Kwa nini ninaandika kitabu hiki? Je, ni kushirikisha uzoefu, kufundisha, au kujenga chapa binafsi? Dhamira hii itakusaidia kusimama imara hata pale unapokuwa umechoka au ratiba imekuwa ngumu.
2. Tumia Muhtasari (Outline) Kama Ramani
Unapokuwa bize, huwezi kuanza kila siku na wazo jipya. Njia bora ni kuandika muhtasari wa sura zako kabla hujaanza kuandika. Hii ni kama ramani ya safari. Inakuokoa muda na inakusaidia kujua ni wapi pa kuanzia kila siku.
Mfano:
- Sura ya 1: Historia yangu
- Sura ya 2: Changamoto kubwa niliyokutana nazo
- Sura ya 3: Mafanikio yangu ya kwanza
Na kuendelea…
unaweza kupata msaada zaidi wa hili kwa kusoma kitabu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. Kupata nakala Yako, wasiliana NAMI Sasa kwa 0655848392. Karibu sana.
3. Andika Kidogo Kidogo Lakini Kila Siku
Uandishi wa kitabu si lazima uwe kazi ya siku nzima. Unaweza kuandika maneno 200–500 kila siku, hata ukiwa unasubiri foleni au mapumziko kazini. Ukiandika maneno 300 kwa siku, kwa wiki utakuwa na zaidi ya maneno 2,000. Hiyo ni karibu sura moja!
Mbinu nzuri:
- Chagua saa moja maalum kwa siku (mfano, kabla ya kulala au asubuhi kabisa)
- Weka alama ya “niliandika leo” kwenye kalenda yako
4. Andaa ‘Draft ya Kwanza’ Isiyo Kamili
Unapokuwa bize, jaribu kujizuia kutaka ukamilifu kwenye awamu ya kwanza. Lengo la awali ni kuandika maudhui Yako. Suala Zima la kurekebisha na kusahihisha ni kazi ya baadaye. Hivyo basi, Kuwa mwepesi kuandika, mzito kuhukumu.
5. Tumia Teknolojia Kukusaidia
Siku hizi kuna zana nyingi zinazoweza kusaidia watu walio bize:
- Voice-to-text apps (zungumza badala ya kuandika)
- Note-taking apps kama Google Keep, Simplenote na notes
- Kuandika kwenye simu wakati unasafiri au unasubiri huduma
6. Kumbuka: Huwezi Kumaliza Kitu Usichoanza
Usisubiri hadi uwe na muda mwingi. Hakuna wakati “kamili” wa kuanza kuandika. Wakati ni sasa. Uandishi ni safari inayohitaji hatua moja kila siku.
Ukiwa bize haina maana huwezi kuandika kitabu. Unachohitaji ni mbinu, dhamira, na nidhamu. Kwa kuandika kila siku hata kidogo, kwa kutumia muhtasari, na kwa kuweka akilini kwamba ukamilifu huja baadaye, unaweza kuandika kitabu kizima ndani ya miezi michache tu.
Je, umekuwa ukiota siku moja kuandika kitabu? Usingoje tena. Anza leo hata kama ni kwa aya moja tu. Kwa msaada zaidi sisi Songambele Consultants tunaweza kukushauri kwenye mchakato mzima WA kuandika kuhariri na kuchapa kitabu chako
Tuwasiliane kwa kutumia simu 0755848392
Tazama video kamili hapa:
📺 Jinsi ya Kuandika Kitabu Kirahisi Hata Kama Uko BizeImeandikwa na GODIUS RWEYONGEZA
-
Nini Cha kufanya unapokutana na changamoto.
Hongera sana kwa kuendelea kupambana rafiki yangu.
Kwenye MAISHA Kuna wakati mambo yanakuwa yanaenda ndivyo sivyo. Mipango Yako unaenda kinyume na matarajio Yako.
Leo ningependa nikwambie tu, inapotokea mipango Yako umependa kinyume, fahamu kuwa
1. Unapaswa kukaa chini na kujitafakari upya. Kushindwa au kuanguka si KITU kibaya, ubaya ni pale unapokataa kukaa chini na kujifuñza kutokana na kushindwa huko. Hivyo Kaa chini ujitafakari, umeshindwa wapi? Kwa Nini umeshindwa? Ni KITU Gani unaweza kufanya ili utoke hapo na kwenda HATUA ya ziada? Tumejifunza Nini?
2. Panga upya. Kila unapojitafakari, panga upya, uone ni HATUA Gani zaidi utachukua baada ya hapo? Ni nini unaenda kufanya baada ya hapa?
3. Chukua HATUA kimkakati zaidi? Baada ya kuwa umeanguka, tayari umeshajua wapi umekosea, kinachofuata ni wewe kuanza kufanyia kazi malengo Yako kimkakati zaidi?
4. Jifanyie tathimini Kila mara. Kila mara jifanyie tathmini kuona mwenendo wako. Uko wapi, unaelelea wapi na Nini zaidi tunafanya.Imeandikwa na Godius Rweyongeza
0755848391
-
Salaam za semina na pongezi kutoka kwa washiriki wote wa semina wa biashara na Uwekezaji 2025
Rafiki yangu mpendwa, salaam. Leo ningependa tu kukutaarifu kuwa semina yetu ya biashara na Uwekezaji imeweza kufanyika kwa kishindo kikubwa sana.
Semina hii ya pekee imefanyika tarehe 28 na 29 kwenye ukumbi wa KINGSWAY HOTEL MOROGORO MJINI
Washiriki wametoka pande mbalimbali za Dunia kuja hapa Morogoro kujifuñza maarifa sahihi ya biashara na Kila KITU kimekwenda kama kilivyokusudiwa.
Kwa Leo ningependa nikudokeze VITU 10 tu kuhusiana na semina hii
- Tumejifunza kuhusu Kuweka malengo binafsi na ya biashara na njia Bora ya kuyafanyia kazi. Huku tukiona kwamba njia ya kufanyiia kazi malengo kwa wiki 12 badala ya miezi 12 ni Bora zaidi.
- Tumejifunza kuhusu masuala yote yanayohusiana na kampuni, HATUA zote za usajili, Faida na hasara za kuwa na kampuni. Na mengine mengi mazuri kuhusu kampuni
- Tumejifunza kuhusu elimu ya Kodi. Hii ni elimu adimu ambayo siyo rahisi kuipata, ila sisi tumeipata. Masuala yote yanahohusiana na ulipaji wa Kodi, sasa tunayafahamu vizuri sana.
- Tukaona isiwe kesi, tukaendelea mbele zaidi kujifuñza namna ya KUANZISHA BIASHARA ya pamoja kama wenza. Hivi hiki kitu kinawezekana, na kama kinawezekana kivipi? Kwa maarifa tuliyoondoka nayo, tuna uhakika wa KUANZISHA BIASHARA kama wenza bila wasiwasi wowote.
- Tumebadilishana mawazo, tumekonekti, tumeshauriana, tumeelekezana Nini Cha kufanya kwenye biashara zetu. Kila mmoja sasa ameondoka na mwongozo kamili wa kufanyia kazi. Na Bado tutakuwa wote kwa kipindi Cha mwaka mmoja ujao tukizidi kupambana zaidi kuelekea kwenye malengo yetu.
- Tumejifunza kuhusu masuala ya benki, tumepata konekisheni za kibenki kutoka kwa watalaam.
- Lakini sote tunajua wazi kuwa wakati tunaendelea kupambana na mambo MAKUBWA na biashara ni vizuri pia kuwaandaa watoto kwa ajili ya hiyo baadaye. Tulichokifanya ni kwamba tumejifunza pia namna ya kuwaandaa.
- Biashara Zina misingi yake, namna ya kuziendesha, Kuweka MIFUMO imara na kujenga timu Bora. Hivi ni VITU vya Msingi sana ambavyo tumeweza kujadiliana kwa kina kwenye semina hii.
- Utt amis wameungana nasi kwenye semina hii kutufundisha Uwekezaji kwenye taasisi hii ya UTT AMIS. Mambo yamekuwa ni moto🔥
- Kuagiza mizigo china, ni KITU ambacho watu wengi wangependa kujifuñza. Tumeona hili kwa undani pia
Kiukweli tunekuwa na siku mbili Bora sana hapa duniani. Tumezitumia vyema
Kujitafakari,
Kujipanga upya
Na sasa tupo tayari kusongambele
NB: Kama hukushushiriki semina na ungependa kuendelea kupata mafunzo haya yote. Habari njema ni kwamba mafunzo haya yote yanapatikana. Tutapata video zote za mafunzo. Utalipia 50,000/- tu BEI YA OFA. Cha kufanya wasiliana NAMI kwa 0755848391 sasa Ili tuweze kuanza kufanyia kazi haya pamoja.