Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Mfuko wa FAIDA (FAIDA FUND): Unawekeza au Huwekezi?

    Watumishi Housing Investment (WHI) wameanzisha mfuko wa uwekezaji wa pamoja ambao wanauita MFUKO WA FAIDA au kama unaielewa vizuri lugha ya kigeni basi unasema FAIDA FUND. Mfuko wao ni mfuko ulio wazi (open-endend). Kama bado hujasoma kitabu changu cha maajabu ya kuwekeza kwenye hisa, hatifunagni na vipande lazima tu utakuwa unajiuliza mfuko ulio wazi maana yake ni nini?

    Mfuko ulio wazi ni mfuko ambao pale unapotaka kununua vipande meneja wa mfuko anakutengenezea vipande vyako. Na pale unapotaka kuuza vipande meneja wa mfuko ananunua vipande vyako.

    Yaani, tuchukilie mfano, mimi naanzisha mfuko wa uwekezaji wa pamoja. Na watu mnakusanyika kununua vipande, labda kipande kimoja ni shilingi mia moja. na watu wa kwanza, mnanunua vipande elfu moja (1000). Mfuko hapo hapo utakuwa na vipande elfu moja. Labda baada ya siku kumi za kununua vipande anatokea mmoja ambaye anataka kuuza vipande vyake 200. Anauza vipande na mimi meneja wa mfuko nanunua hivyo vipande na kumpa hela yake. Mfuko unabaki na vipande 800. Wakati kesho yake anatokea mwingine ambaye anataka kunununua vipande mia tano. Na huyo anaunua vipande na hivyo vipande vya mfuko sasa vinakuwa 1300/-.

    Kwa hiyo, mfuko ulio wazi huwa una sifa ya kuongezeka kwa vipande pale wanunuaji wanaponunua na kupungua kwa bei pale wauzaji wanapouza.

    Mfuko ulio wazi (open ended) ni tofauti kabisa na mfuko uliofungwa (closed ended) ambao wenyewe huwa una idadi ya kamili ya vipande, na idadi hiyo huwa haiongezeki wala kupungua. Kama mfuko una vipande 1000. Vinabaki kuwa hivyo hivyo tu miaka yote. Ili ununue vipande kwenye mfuko uliofungwa, lazima awepo mtu anayeuza. Na ili uuze, lazime kuwepo anayenunua. Utagundua kitu hiki ni tofauti na mfuko ulio wazi ambao meneja wa mfuko ndiye ananunua au kukuuzia vipande. Kama huelewi, hakikisha unapata kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE kwa 20,000 tu, nakala ngumu, na 10,000 tu nakala laini (softcopy).  Kipate kitabu hiki kwa ajili ya kuongeza maarifa zaidi pia kuhusu eneo hili la uwekezaji.

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Kitabu hiki kinapatikana kwa 20,000/- tu

    Mimi niache niendelee mbele kuuongelea mfuko wa FAIDA ulioanzishwa na WHC.

    Mfuko upo chini ya WHI ambao wamesajiliwa na kisheria chini ya soko la mitaji (CMSA).

    Madhumuni ya mfuko

    •   Mfuko huu   ni    mpango    ulio    wazi unaotoa fursa nyingine ya uwekezaji kwa Watanzania hasa wa kipato cha kati na cha chini kupitia uwekezaji katika vipande ili kupata mapato shindani kupitia ukuaji wa mitaji.

    • Kuwajengea watanzania utamaduni wa kuwekeza katika Masoko ya Fedha na Mitaji na kuweka akiba.

    Anayestahili kuwekeza kwenye huu mfuko

    Mfuko huu unatoa mwanaya wa mtu yeyote, (ambaye ni mtanzania au wa nje ya nchi) kuwekeza kwenye mfuko huu. Lakini pia taasisi kama benki, mifuko ya pension, taasisi za kiserikali,  taasisi zisizo za kiserikali, taasisi za kijeshi, makampuni n.k.

    Kiwango cha chini cha kuwekeza kwenye mfuko huu

    Kiwango cha chini cha kuwekeza kwenye huu mfuko ni elfu kumi, pale unapofungua akaunti mara ya kwanza. Baada ya kufungua akaunti, unaweza kuendelea kuwekeza zaidi kwenye huu mfuko kwa kuongeza kiwancho cha chini kabisa cha shilingi elfu tano.

    Kiwango cha juu cha kuwekeza

    Hakuna kiwango cha juu cha kuwekeza. Kwa hiyo, kama una mabilioni ya kuwekeza, unaweza kuyawekeza bila shida yoyote kwenye huu mfuko. Lakini bado kama huna mabilioni makubwa sana, unaweza kuendelea na utaratibu wako wa kuwekeza kwenye huu mfuko kadiri utakavyojiwekea, kwa kuweka kiwango cha chini kabisa cha elfu tano (5,000/-) kila utakapohitaji kuwekeza.

    Gharama za kujiunga na mfuko (Entry load)

    Kwa kawaida huwa ukitaka kununua hisa, huwa kuna gharama ambayo mtu unalipia ili kununua hisa. Na pale unapotaka kuuza hisa zako, kuna gharama ambazo unakatwa. Hizi gharama kwa Kiswahili tunaweza kuziita tozo za kiujiunga (entry load) au tozo za kujitoa (exit load).

    Wakati wa kujiunga na mfuko huu au wakati wa kujitoa kwenye huu mfuko, hakuna gharama yoyote ile ya kujiunga au kujitoa.

    Thamani ya kipande

    Thamani ya mwanzo ya kipande ni Tsh 100/=. Hii itatumika wakati wa mauzo ya awali na baada ya hapo kipande kitauzwa kulingana na thamani halisi.

    Ambapo kipande kitapanda au kushuka kulingana na mwenendo wa soko kwa wakati husika.

    NB: Mpaka sasa hivi mfuko upo kwenye hatua za awali za kuuza vipande vyake. Hivy, kama unasoma ujumbe huu kabla ya tarehe 31 Disemba, unaweza kununua vipande kwa bei ya awali ya vipande.

    Ukwasi

    Uuzaji wa vipande utafanyika kila siku baada ya mienzi mitatu tangu kumalizika kipindi cha mauzo ya awali. Mfuko utatuma malipo ya mauzo ya vipande ndani ya siku tatu za kazi baada ya kupokea maombi katika Makao Makuu ya Watumishi Housing Investments. Fedha za mauzo zitatumwa moja kwa moja katika akaunti ya benki ya mwekezaji au simu ya mkononi iliyosajiliwa.

    Sera za uwekezaji kwenye mfuko

    Mfuko utawekeza katika masoko ya fedha kwa asilimia 100%. Kiwango cha uwekezaji katika masoko ya fedha na Dhamana kitalenga kupata mapato makubwa katika soko.

    Muda wa kuendesha mfuko

    Mfuko huu ni wa kudumu kwa mujibu wa Waraka wa Makubaliano.

    Faida za kikodi

    Kwa mujibu wa sheria za nchi,mgawanyo wa mapato ya Mfuko yamesamehewa kodi ya mapato kwa wawekezaji.

    Hayo ni baadhi ya mambo ambayo nimekuandalia kuhusu  mfuko huu.

    NB: 1. Kabla hujachukua hatua ya kuwekeza kwenye huu mfuko, nashauri uhakikishe umesoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE ili uweze kuelewa zaidi dhana ya uwekezaji.

    2. Mwandishi wa makala hii hauhusiki kwa vyovyote vile na faida au hasara utakayopata kutokana na uwekezaji utakaoufanya kwenye huu mfuko. Ni muhimu kuhakikisha kwamba umepata ushauri wa watalaam kabla ya kufanya uwekezaji.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • SEMINA YA KUFUNGUA MWAKA: Karibu kwenye Semina ya kufungua mwaka 2023

    Kila mwanzo mwa mwaka na katikati mwa mwaka huwa Kuna semina ambayo huwa naiendesha.

    Mwakani wakati wa kufungua  mwaka mpya tunatarajia kuwa na semina ya kufungua mwaka ambayo itafanyika kuanzia tarehe 15.

    Na itadumu kwa siku 15 mfululizo. Semina hii ya kipekee ambayo itafanyika kwa njia ya mtandao, inalenga kukupa maelezo ya kina yatakayokusaidia kuuanza mwaka mpya kwa mtazamo sahihi na kuuweza kuufanikisha kwa viwango vikubwa sana. Semina hii inaitwa JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO 2023.
    Kwenye Semina hii utajifunza Mambo
    1. Namna ya kuongeza thamani yako
    2. Namna ya kuongeza kipato chako mara mbili mpaka mara kumi zaidi
    3. Njia za kuweka malengo na kuyafanyia kazi kwa usahihi ndani ya mwaka 2023.
    3. Nguvu ya vitu vidogo kwenye kuongeza thamani yako binafsi na mengine mengi

    Hii Ni semina ya siku 15 mfululizo ambayo imeshiba mambo ya msingi sana yanayokufaa wewe na yatakayokusaidia wewe kuuanza mwaka kwa usahihi na kupiga hatua na kufika mbali.

    Katika siku hizi 15 utapata masomo 15 yaliyoandaliwa kwa kina na ambayo yatakusaidia wewe kuanza KUONGEZA THAMANI YAKO ndani ya mwaka 2022.

    Ni matarajio yangu kuwa baadaa ya semina hii, utakuwa na mbinu za kukusaidia wewe kuongeza thamani yako binafsi na kipato chako walau Mara mbili zaidi

    Hakikisha kwamba haukosi Semina hii, ya kipekee sana

    Semina itafanyika lini?
    Itaanza tarehe 15 Januari na itadumu kwa siku 15

    Semina itafanyika wapi?
    Semina itafanyika mtandaoni (WhatsApp) kwenye kundi maalumu la WhatsApp.

    Je, Kuna ada ya kujiunga na Semina.
    Ndiyo ada ipo. Ada ya semina ni 15,000/- tu. Kwa kila mshiriki kwa siku zote za semina.
    Mwisho wa kulipia ni tarehe 10 Januari.

    Njoo uuanze mwaka wako kwa kiusahihi na kwa kupata mwongozo utakaokusaidia kuufanyia kazi mwaka mpya kutokea kwenye nafasi nzuri.

    Kuthibitisha ushiriki wako. Tuma malipo yako kwenye Namba ya simu 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Karibu sana

    Whatsap group la semina: https://chat.whatsapp.com/FbzmwEVkObKIuqeR4pIZmu

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
    Unaweza kusoma makala na mafunzo yake zaidi kwenye blog yake ya SONGAMBELE (www.songambele.co.tz)

  • Maisha ndiyo hayahaya rafiki yangu

    KIPAJI NI DHAHABU
    Rafiki yangu, nimeandika kitabu. Kinaitwa KIPAJI NI DHAHABU. Ili kupata kitabu hiki, wasialiana na mi kwa 0755848391 sasa

    Rafiki yangu wa ukweli, moja ya kitu ambacho watu huwa wanafanya kwenye maisha yao ni kusubiri kila kitu kiwe sawa ili waweze kufanyia kazi malengo na ndoto zao. Ila ninachotaka kukwambia rafiki yangu ni kwamba, hakuna hata siku moja ambayo kila kitu kitakaa sawa kwa ajili ya kukusubiri wewe ufanyie kazi malengo yako. Maisha ni haya haya, hivyo, unachopaswa kufanyia malengo na ndoto zako sasa hivi katika hali hii hii unayopitia. Ukweli ni kwamba rafiki yangu ukiendelea kusubiri kila kitu kikae sawa, hiyo siku haitakuja kufika.

    Fanyia kazi malengo yako katika hali hiyohiyo.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Bei kisiwe kigezo cha wewe kuuza

    Moja ya dhana ambayo watu huwa wanatumia kwenye kuuza ni kuuza kwa bei ya chini. rafiki yangu, nataka kukwambia kitu kimoja muhimu sana, kwamba mara zote usishindane kwa bei. Maana kadiri unavyopunguza bei, mara zote utakuta kwamba kuna mtu anawezakupunguza bei zaidi yako.

    Hivyo, bei kisiwe ndiyo kigezo pekee cha wewe kuuza.

  • Wafanyakazi na mfumuko wa Bei

    hisa na nguvu ya vitu vidogo  kuelekea mfanikio makubwa
    hisa na nguvu ya vitu vidogo kuelekea mfanikio makubwa

    Kila tarehe 1 mwezi Mei. Macho na masikio yote ya wafanyakazi huwa yapo kwa kiongozi mkuu wa nchi kuona kama atawaongezea mshahara.

    Unajua kwa nini huwa wanataka ongezeko la mshahara? Ni kwa sababu kile kipato wanachokuwa nacho mwanzoni kinakuwa hakitoshi kuwafanya wamudu mahitaji ya kila siku. Hivyo, ongezeko la mshahara likiwepo kweli, linaweza kuwa suluhisho, japo kwa kiasi fulani. Lakini kesi hii haiishii hapo, hii kesi ni kubwa na mahakama haitoshi, ndio maana tunaendelea mbele mpaka tupate suluhisho😋😋

    Utakumbuka kwenye makala ya jana tuliongelea juu ya suala zima la mfumuko wa bei. Lakini mwisho wa siku tuliona ni kwa namna gani unaweza kuukwepa mfumuko huu wa bei kwa kufanya uwekezaji.

    Sasa siku ya leo nataka tuone uhusiano uliopo Kati ya mshahara na mfumuko wa bei na kwa nini kila mwaka wafanyazi huwa wanaomba ongezeko la mshahara. Lakini kama  kawaida yangu, sitakuacha hivihivi, maana lengo langu siyo tu kuliongelea tatizo pekee, bali kukupa suluhisho.

    Kabla sijaenda mbali zaidi. Naomba niwashukuru wale wote wanaosoma makala zangu na kunipa mrejesho. Na hasa wanaoenda mbali zaidi na kusapoti kazi zangu kwa kununua. Nyie ndio mnawezesha ujio wa makala nyingine zaidi kama hizi. Asante sana

    Sasa ili tuweze kuelewa kwa kina zaidi kwa nini wafanyakazi wanakuwa wanahitaji ongezeko la mshahara, inabidi uelewe kwa kina dhana ya mfumuko wa bei kama nilivyoieleza jana.

    Mfumuko wa bei huwa unatokea kila mwaka, na serikali kupitia benki kuu ya Tanzania (BoT) huwa inatangaza mfumuko wa bei kwa mwaka huo umekuwa ni kiasi gani. Ila mshahara huwa hauongezeki kila mwaka, kumbe basi kama mfumuko wa bei unaongezeka kila mwaka na mashahara hauongezeki kila mwaka, basi hapo Kuna shida sehemu……..

    Jana nilisema kwamba mfumuko wa bei ni pale Ambapo uwezo wa fedha kufanya manunuzi unapungua japo fedha inabaki ileile.
    Mfano kama ulikuwa na elfu moja mwanzoni mwa miaka 2000 ulikuwa na uwezo wa kununua nguo za kutokelezea mtaani. Ila leo hii elfu  huwezi kununua nguo ya kudamshi kwa elfu moja hiyohiyo😂😂.

    Elfu moja imebaki ileile, Ila uwezo wake wa kufanya manunuzi umepungua.

    Tuchukulie unalipwa mshahara wa laki moja. Na mwaka huu mfumuko wa bei ni asilimia 4.4 kama ulivyoripotiwa. Tazama jedwali hapo chini

    Kama mwwka huu  mfumuko wa Bei ni 4.4 na wewe mshahara wako ni laki moja. Maana yake mshahara utapokea uleule Ila utakuwa umepungua uwezo wa kufanya manunuzi kwa asilimia 4.4.

    Asilimia 4.4 ya mshahara wa laki moja ni 4400.

    Kumbe basi, Kama mwaka jana mshahara wako wa laki moja ulikuwa unakutosha kuishi vizuri.
    Mwaka huu hautakutosha kwa sababu ya mfumuko wa bei. Mshahara wako utabaki uleule ila utakuwa umepungua uwezo wa kufanya manunuzi kwa asilimia 4.4 sawa na shilingi 4400/-

    Kumbe basi ndio maana wafanyakazi wanakuwa wanahitaji ongezeko la mshahara.  Ili walau like ongezeko la mshahara lifidie kile kilichopungua kutokana na mfumuko wa bei.

    Kama mfanyakazi ana matumizi sawa na mshahara wake. Na mfumuko wa bei ni asilimia 4.4. anahitaji, ongezeko la mashara linaoendana na mfumuko wa bei ili asiingie kwenye mikopo ili kukidhi mahitaji yake. lakini endapo, hakutakuwa na ongezeko la mshahara, maana yake huyu mfanyakazi, atapaswa kukopa kiasi cha walau shilingi 4400/- ili kuongezea kufidia mfumuko wa bei uliotokea. Na hapo atakuwa ameanza kuingia kwenye madeni.

    Hiki kitu ndicho huwa kinawafanya wafanyakazi waombe ongezeko la mshahara zaidi.

    sasa mfanyakazi anaweza kufanyaje ili kuondokana na hali hii?

    Kwanza ni kuhakikisha kwamba anapata elimu sahihi, kuhusu mfumuko wa bei.

    Pili ni kuanza kufanya uwekezaji. maana njia pekee ya kuukwepa mfumuko wa bei ni kuwekeza sehemu ambayo inaweza kukupa mrejesho mkubwa kuliko mfumuko wa bei wenyewe.

    na kwenye hili nimekua nakushauri walau kuwekeza UTT, kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja. Unajiuliza, mfuko wa pamoja ni nini? UTT ni kitu gani? Naanzaje kuwekeza kwenye UTT na maswali mengine kama hayo? basi, tuwasiliane kwa 0755848391 ili uweze kupata nakala ya kitabu chako. Karibu sana.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • USIFANYE kosa hili unapotaka kufanya uwekezaji

    Rafiki yangu, bila shaka uko vizuri. Leo nataka nikwambie kosa moja unalopaswa kuepuka unalofanya uwekezaji. Na kosa hili ni kuwekeza kwa sababu rafiki zako wanawekeza.

    Ni muhimu Sana kabla wewe hujawekeza, uhakikishe kwamba unefanya ufuatiliaji wa kina, Kisha uwekeze. Rafiki yangu, USIFANYE kosa la kuwekeza kwa mkumbo.

  • Mfumuko wa bei ni nini?

    Kila mwaka serikali kupitia benki kuu ya Tanzania huwa inatoa takwimu za mfumuko wa bei. Unakuta ripoti inasema kwamba mwaka huu mfumuko wa bei ni asilimia 4, 5,au 3.5,7 au vyovyote vile kulingana na ripoti inavyokuwa inasema.

    mfumuko wa Bei kwa miaka Saba iliyopita.

    Wengi huwa hawajui mfumuko wa bei ni kitu gani na una madhara gani kwao.

     Leo hii ningependa kukueleza mfumuko huu wa bei kwa lugha rahisi sana kiasi kwamba ukishasoma hapa uweze kumweleza mwanao wa miaka 6, aweze kukuelewa.

    Mfumuko wa bei ni pale ambapo fedha inapoteza uwezo wake wa kununua vitu.

    Tukichukulia mfano wa shilingi mia tano. Mwanzoni mwa miaka ya 2000, kama ulikuwa na shilingi mia tano,ungeweza kununua kipande cha sabuni, kiberit na chumvi na bado ukabaki na chenji. Ila leo hii, kwa shilingi mia tano hiyo hiyo, huwezi kununu hata kipande kimoja cha sabuni. Hii ndio kusema kwamba fedha imepoteza uwezo wake wa kufanya manunuzi.

    Shilingi mia tano imebaki kuwa ileile, ila uwezo wa kununua vitu kama ilivyokuwa mwaka 2000 siyo kama ulivyo sasa hivi.

    Serikali ikitangaza kwamba mwaka huu mfumuko wa bei ni asilimia 4. Maana yake uwezo wa fedha kufanya manunuzi umepungua kwa asilimia 4.

    Hii ndio kusema kwamba kama una shilingi elfu moja kama akiba haiwezi tena kufanya manunuzi kama iliyokuwa inafanya mwaka jana.

    Kama mwaka jana shilingi elfu moja ilikuwa inaweza kununua

    • Sabuni kipande kimoja (500)
    • Kiberiti (100)
    • Kalamu kwa ajili ya mwanao 200/-
    • Na ukabaki na chenji 200

    Mwaka huu hutaweza kufanya manunuzi hayohayo na hela yako hiyohiyo. Elfu moja itabaki kama elfu moja. kama ni noti itakabaki kama elfu moja noti, ila uwezo wake wa kufanya manunuzi utapungua kwa shilingi 40. Kumbuka mfumuko wabei ni asilimia 4.

    Kwa hiyo kwa mwaka huu maana yake vitu vitapanda bei kidogo. na hivyo chenji uliyobaki nayo mwaka jana itapungua au pengine hutakuwa na chenji tena!

    Sasa unafanyaje ili kuukwepa mfumuko wa bei.

    Njia pekee ya kuukwepa mfumko wa bei ni kufanya uwekezaji. Ambao unaweza kukupa mrejesho ambao ni mkubwa kuliko uwekezaji.

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Pata nakala ngumu (hardcocopy) kwa shilingi 20,000/- tu. Utatumiwa popote ulipo. Nakala laini Ni 10,000/-

    Ndio maana nimekuwa nashauri watu kuwekeza UTT. UTT wamekuwa wanatoa mrejesho mkubwa ulio juu ya mfumuko wa bei.

    Ili uniewe vizuri angalia kwanza chati hii hapa chini.

    Jedwali hapo juu linaonesha mrejesho ambao umekuwa unatolewa na mfuko wa UTT yangu kuanzishwa.

    Mrejesho wa wastani tangu kuanzishwa mei 2005 ni asilimia 15.7

    Hii ndio kusema kwamba kama uliweka shilingi elfu moja kwenye mfuko wa UTT mwaka 2005, mpaka leo hii hiyo shilingi elfu moja tu uliyoweka, imekuwa inapata ongezeko la wastani wa asilimia 15.7 kila mwaka.

    Hii ndio kusema kwamba kila mwaka elfu moja yako, imekuwa inapata ongezeko la asilimia 157 kwenye UTT ukitoa mfumuko wa Bei bado unakuwa juu.

    Mfano kwa mwaka huu ambao mfumuko wa Bei ni asilimia 4.4 Kama tukivyoona hapo juu, maana yake.
    Kama hiyo elfu moja yako uneiweka UTT, ukapata mrejesho wa 15.7 Ni sawa na ongezeko la shilingi 157.

    Ukitoa kiasi kikichotokana na mfumuko wa bei. Yaani, shilingi 44 maana yake utakuwa na (157-44=113).

    NB. Wastani wa mrejesho wa 15.7 Ni wa jumla kwa yangu mfuko wa UMOJA uanzishwe mwaka 2005 mpaka 2022 Juni 31.

    Ili lunielewe vizuri naomba nitolee mfumuko wa bei kwa mwaka mmoja uliopita.

    Tuchukulie mfano tuna watu wawili

    Bwana CHACHA NA BW. MWASHA

    Bwana Chacha ana shilingi elfu moja, ambayo ameiweka akiba chini ya godoro mwaka 2021 julai mosi. Mwaka mmoja baadaye, tarehe 31 Juni 2022, serikali kupitia benki kuu ya Tanzania (BoT) inatangaza kuwa mfumuko wa bei ulikuwa ni asilimia 4.4 kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini

    Hii ndio kusema kwamba thamani ya fedha ya bw. Chacha, itakuwa imepungua uwezo wa kufanya manunuzi kwa shilingi 44/- tu. Elfu moja yake aliyoiweka akiba,  itabaki kama elfu moja. ila itakuwa imepungua uwezo wa kununua kwa shilingi 44 tu.

    Yaani, kama bw. Chacha alikuwa anaweza anaweza kununua

    • Karanga (kwa shilingi 100)
    • Pipi kifua (shilingi 50)
    • Andazi (shilingi 100)
    • Sabuni 500
    • Kitunguu 100
    • Majani ya chai  (shilingi 100)
    • Na kubaki na chenji ya shilingi 50

    Kwa mfumuko wa bei wa mwaka huu, ambao ni asilimia 4.4, maana yake akienda dukani kununua vitu. Ile chenji yake ya shilingi 44. Haitabaki, badala yake itabaki shilingi 6 tu. kama mwenye duka ana shilingi 6, basi atampa hiyo shilingi 6.

    Mfumuko wa bei umemeza shilingi 44. Maana yake vitu alivyokuwa ananunua hapo zamani kwa elfu moja na kubaki na chenji sasa hivi vimepanda bei.

    ILA KWA UPANDE MWINGINE

    Bwana Mwasha naye ana shilingi elfu moja, ambayo ameiweka UTT mwaka 2021 julai mosi. Mwaka mmoja baadaye, tarehe 31 Juni, serikali kupitia benki kuu ya taifa inatangaza kuwa mfumuko wa bei ulikuwa ni asilimia 4.4 . lakini wakati huohuo, mfuko wa UTT, ukatangaza ongezeko la thamani la asilimia 11.7 kama inavyoonekana hapo chini.

    Hii ni tawkimu halisi ya mwaka huu.

    Hii ndio  kusema kwamba mfumuko wa bei wa asilimia 4.4 ni sawa na shilingi 44 na

    Ongezeko la thamani la asilimia 11.7 lilitolewa UTT ni sawa na shilingi 117. Hivyo basi, kwenye ile elfu moja yetu. Tutaongeza shilingi 117 ambayo UTT wametoa kama ongezeko la Thamani, hivyo ile elfu moja ya Bw. Mwasha aliyokuwa nayo mwanzoni mwa mwaka 2021 itakuwa tena siyo elfu moja bali itakuwa ni shilingi 1117. Tukitoa kiwango cha mfumuko wa bei ambayo ni shilingi 44 tutabaki na  1073.

    Kwa hiyo bwana Mwasha akifanya manunuzi baada ya mfumuko wa bei bado atabaki na shilingi 73 ya chenji.

    Bw. Chacha atakuwa ameupiga mfumuko wa bei na kuukwepa.

    Kumbe basi, njia pekee ya mtu yeyote yule kuukwepa mfumuko wa bei, ni kuhakikisha kwamba anafanya uwekezaji, na eneo la kuanzia ni kwenye Hisa, hatifungani na vipande.

    Ndio maana nashauri wewe rafiki yangu uweze kujipatia nakala ya kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

    Kitabu hiki cha kipekee gharama yake ni 20,000/- tu. na utaletewa popote pale utakapokuwa. Nakala laini Ni 10,000/-

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Kitabu hiki kinapatikana nakala ngumu ni 20,000/- na nakala laini kwa elfu kumi tu (sotfcopy)

    Kwenye hiki kitabu nimeeleza kwa kina dhana nzima ya mfumuko wa Bei. Na mengine mengi yako kwenye kitabu

    Tuwasiliane sasa kwa 0755848391 ili uweze kupata nakala yako.

    Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

    Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

    Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

  • Aina tano za uwekezaji ambazo kila kila kijana anapaswa kufanya

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)

    Habari ya siku hii ya kipekee rafiki yangu. Bila shaka unaendelea vyema kabisa,
    Siku ya leo ningependa nikwambie Aina Tano za uwekezaji ambao unapaswa kuhakikisha umezifanya.

    Huu ni uwekezaji ambao ukiufanya sasa hivi ukiwa kijana. Kadiri siku zinavyoenda wewe utavuna matokeo yake tu. Hakikisha unazitumia aina zote hizi za uwekezaji ukiwa bado kijana, maana ujana ni muda mzuri wa wewe kutumia kwa vitendo haya unayojifunza hapa ili umri ukisogea uanze kufurahia matunda ya haya tunayojifunza.

    Kwanza ni uwekezaji kwako mwenyewe.
    Yaani, hapa wekeza kwenye kujifunza na kupata maarifa sahihi ambayo yatakusaidia kusonga mbele.

    Kuna vyanzo vingi ambavyo Kama kijana unaweza kutumia kupata haya maarifa, ila Mimi nakushauri sana uweze kutumia vifuatavyo.
    Kwanza tumia VITABU. Penda kusoma VITABU maana humu kuna mengi utakayonugaika nayo.
    Pili, jifunzee kupitia kozi mbalimbali za mitandaoni, ana kwa ana au vyuoni.
    Jifunze kwa waliokutangulia na wazee. Mazuri yao yafanye zaidi. Majuto Yao yaepuke.

    chagua mwalimu mmoja kwenye mtandao wa youtube kisha endelea kukjifunza kutoka kwa huyu mwalimu kila mara. Siku hizi kuna walimu wengi kwenye mtandao huu kiasi kwamba huwezi walau kukosa mwalimu mmoja ambaye unaweza kujifunza kwake.

    Pili, wekeza kwenye kuanzisha na kukuza iashara Yako.
    Hiki Ni kitu KINGINE muhimu ambacho kama kijana unapaswa kuhakikisha umekifanya.
    Tunaishi kwenye ulimwengu wa pekee Sana tofauti na miaka mingine mingi ya nyuma. Leo hii Ni rahisi Sana kuanzisha Biashara tofauti na vile ilivyokuwa hapo zamani za kale.

    Na hii fursa ambayo kila kijana anapaswa kuhakikisha kwamba anaitumia vizuri. Hata Kama umeajiriwa Sasa hivi, Anza kufikiria NAMNA ya kuanzisha na kuendesha Biashara yako.

    Biashara itakupa kipato ambacho hakina ukomo. Maeneo mengine Yana ukomo wa kipato. Ongezeko la mshahara linategemea kudra za bosi, na hata haliongezeki kila mara. ila kwenye biashara kuna uwezekano wa wewe kutengeneza kipato chako bila ukomo. maana kadiri utakavyokuwa unaongeza mauzo kwenye biashara yako ndivyo ambavyo utakuwa unaongeza mauzo zaidi. kwa hiyo basi, nashauri uhakikishe unaanzisha biashara yako ambayo utaanza kuisimamia hata kama umeajiriwa rafiki yangu.

    tatu, wekeza kwenye vipande vya utt

    Mtu yeyote ambaye huwa ananitafuta na kuniambia kuwa ana hela na angependa kuanza kufanya uwekezaji, basi eneo la kwanza kabisa ambalo huwa namwambia wekeza hela yako ni Utt.. hii ni kutokana ukweli kuwa ni rahisi sana kuwekeza UTT kuliko lilivyo eneo jingine.

    Ni rahisi pia kufuatilia mwenenedo wa mifuko ya UTT kuliko ilivyo rahisi kufuatilia mwenendo wa uwekezaji mwingine. Kwa hiyo, basi kama kuna uwekezaji ambao unapaswa kuufanya rafiki yangu, basi ni kuhakikisha kwamba unaanza kuwekeza UTT.

    Nne, wekeza kwenye hisa

    hili ni eneo moja la muhimu sana ambalo watu wengi wamekuwa hawaelewi. Soko la hisa kwa Tanzania limekuwa kwa miaka zaidi ya 20 sasa. lakini cha kushangza ni kwamba watu wengi wamekuwa hawalielewi na hivyo, kila mara kujikuta kwaba wanajiingiza kwenye uwekezaji ambao siyo sawa huku wakishindwa kufanya uwekezaji mzuri kama huu wa hisa.

    Kama wewe huelewi uwekezaji wa aina hii, basi nashauri uweze kupata kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. hiki ni kitabu cha kipekee sana ambacho kitakusaidia wewe kuanza kufanya uwekezaji kwenye soko la hisa. lakini siyo tu kwamba utalijua soko la hisa, bali utajifunza pia kwa kina suala zima la vipande na hatifungani.

    Nakala ngumu ni 20,000/- tu. karibu sana uweze kujipatia nakala yako sasa hivi.

    Tano, wekeza kwenye kuandaa kizazi kijacho

    Moja ya kosa kubwa ambalo watu wengi wamekuwa wanafanya ni kupambana kwa nguvu zao zote kutafuta mafanikio ila huwa hawaweki nguvu kwenye kuandaa kizazi kijacho. hiki ni kitu ambacho rafiki yangu unapaswa kukifanyia kazi pia.

    wakati unapambana kutafuta fedha na kuwekeza. unapaswa kuwafundisha wanao pia ili wajue kila kitu unachofanya. kwa jinsi hii utakuwa umefanya uamuzi mzuri sana wa kuandaa kizazi kijacho.

    Rafiki yangu, anza kuandaa kizazi kijacho sasa.

    Hakikisha umepata nakala ya kitabu cha MAAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Nakala ngumu ni 20,000/. Nakala laini 10,000/- tu. Karibu sana.

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)

  • Kiashiria kuwa uwekezaji uliolfanya Siyo sawa

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)

    Juzi Kuna mtu alinipigia simu na kuniambia kuwa Kuna uwekezaji ameufanya. Ila hawezi kuniambia uwekezaji huo kwenye simu mpaka tuonane.

    Nilipomuuliza kwa Nini, alisema hataki watu wawepo maana uwekezaji wenyewe ni siri.

    Rafiki yangu, kama uwekezaji uliofanya wewe mwenyewe unaogopa kuusema mbele ya watu basi jua tayari umeshaliwa😂😂.

    Simaanishi kwamba ufanye uwekezaji halafu uende mbele ya watu na kuanza kujigamba. Hapana.

    Lakini ninachotaka ujue kwa uwekezaji wako wowote ule utakaoufanya, kama unaogopa kuusema mbele ya watu ujue uwekezaji wako una shida sehemu.
    Uwekezaji unaofahamika
    Ni kwenye hisa.
    Hatifungani
    Vipande
    Ardhi (real estate)
    Vito vya thamani…..
    Fedha za kigeni…

    Sasa je, wewe uwekezaji wako unaweza kuutaja kwa watu hadharani bila kuogopa mtu?

    Kama unaogopa kuutaja aidha kwa kuhofia polisi au kitu kingine basi jua huo siyo Uwekezaji.

    Ndio maana nashauri ujifunze kwa kina uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Maana utakufaa sana. Hakikisha umepata nakala ya kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Kitabu hiki unaweza kukipata kwa 5,000/- tu. Nakala laini.
    Nakala ngumu 20,000/-

    Karibu Sana

    Kupata nakala yako. Tuna fedha kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Utatumiwa nakala yako popote pale ulipo bila kuchelewa.

    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Uchambuzi wa Kitabu: Atomic Habits; Tiny Changes, Remarkable Results

    Mwandishi: James Clear

    Mchambuzi: Hillary Mrosso

    Simu: +255 683 862 481

    UTANGULIZI

    Tabia hujenga maisha tuliyonayo, tabia huamua mafanikio kwenye maisha yetu. Ubora wa maisha yetu ya sasa na ya baadaye yanategemea sana tabia tunazoziishi kila siku. Mara zote tumejikuta kwenye jamii ambayo inaishi na kuamini kwenye tabia fulani ambazo kwa kiasi kikubwa ndio tabia tunazoziishi na ndio zimetuletea maisha tuliyo nayo.

    Mandishi James Clear kupitia kitabu chake cha ATOMIC HABITS, ametuonyesha namna inavyowezekana kujenga tena tabia tunazozipenda, pia ametuonyesha kupitia kitabu hiki namna ya kuvunja tabia tusizozipenda. Kupitia uchambuzi huu, nimekuandalia mambo 130, niliyojifunza ndani ya kitabu hiki bora kuhusu tabia. Naweza kuungana na watu wengine kusema hiki ndio kitabu bora sana kuhusu tabia. Karibu sana katika uchambuzi wa kitabu hiki.

    1. Wote tunakutana na changamoto kwenye maisha lakini baada ya muda ubora wa maisha yetu huamuliwa na ubora wa tabia zetu. Kila tabia ina matokeo yake, ukiwa na tabia nzuri utaleta matokeo mazuri ukiwa na tabia mbaya utaleta matokeo mabaya.

    2. Mjasiriamali na mwekezaji, Naval Ravikant aliwahi kusema, ili uandike kitabu bora, unahitaji kwanza kuwa kitabu. Maana yake kabla ya uandishi wa kitabu hiki kilichoandikwa na James Clear aliishi na kuyafanyia kazi mambo yote yanayohusu tabia aliyoyaandika katika kitabu hiki.

    3. Hakuna njia moja nzuri ya kujenga tabia bora, lakini kupitia kitabu hiki mwandishi amejaribu kutumia njia za ufasaha na zilizohakikishwa katika utengenezaji wa tabia bora, haijalishi upo kona gani ya dunia, unaweza kutumia mafunzo ya kitabu hiki na ukajenga tabia bora sana kwenye maisha yako.

    4. Kila ushindi kidogo unaoupata, au vikwazo vidogo unavyovipata vinaweza kuzalisha matokeo makubwa sana endapo vitaendelea kutokea bila kukoma. Maana yake ni kwamba hata kama unataka kuanzisha tabia unayoiona ni ndogo na inaweza kuwa haina sana mchango, ukweli ni kwamba mkusanyiko wa vitu vidogo vidogo huleta matokeo makubwa hapo baadaye.

    5. Tabia ni mkusanyiko wa juhudi binafsi zinazochukuliwa kila siku ili kujiboresha. Kama vile fedha inavyoweza kuongezeka kwa njia ya riba kutokana na mkusanyiko wa siku nyingi hivyo ndivyo ilivyo kwa tabia pia.

    6. Mafanikio yako kimaisha ni matokeo ya tabia ulizoziishi kwenye maisha yako, mafanikio yako kifedha ni matokeo ya tabia bora za kifedha unazoziishi, uzito na afya uliyonayo ni matokeo ya tabia za ulaji unazoziishi kwenye maisha yako, ufahamu na maarifa uliyonayo ni matokoe ya tabia za kujifunza unazoziishi kwenye maisha yako. Mara zote huwa tunapata kila tunachokifanya na kukirudia rudia kwenye maisha yetu.

    7. Tabia ni kama upangwa wa pande mbili, unaweza kuutumia kukusaidia na pia unaweza ukatumika kukuharibu. Maana yake tabia zinaweza kukuletea mafanikio na pia tabia zinaweza kukukwamisha kufikia mafanikio yako. Tabia ni hatari sana, hivyo jua namna ya kuzitumia tabia zikusaidie kwenye maisha yako.

    8. Mafanikio ni matokeo ya mkusanyiko wa juhudi na hatua ulizokuwa unachukua siku za nyuma bila kuacha, na ndio hujikusanya na kukufanya uonekane umefanikiwa sana ndani ya kipindi fulani. Maana yake hakuna kinachofanyika bila kuwa na mchakato wa muda mrefu, mfano ugonjwa wa kansa, unaweza kutumia zaidi ya 80% ndani ya mwili wako bila kugundulika, lakini siku ya kuja kuonekana ni majanga makubwa sana ndani ya mwezi mmoja.

    9. Mara nyingi sana ni ngumu kutengeneza tabia bora zinazodumu, kwasababu hatua ndogo ndogo tunazochukua kila siku zinaweza zisiwe na matokeo ya haraka, na wakati mwingine matokeo yake hayaonekani na huchukua muda mefu kuonekena, jambo hili ndio husababisha wengi kuishia njiani na kukata tamaa, hivyo kushindwa kuunda tabia wanazozitaka.

    10. Kama unajikuta unashindwa kujenga tabia nzuri kwenye maisha yako, au umeshindwa kuivunja tabia mbaya, sio kwasababu huna uwezo wa kuivunja tabia hiyo, bali ni kwasababu kuna ukanda umeshindwa kuuvuka.

    11. Kazi ya kuondoa tabia mbaya kwenye maisha yetu ni kama kuungoa mti mkubwa wa mkuyu wenye mizizi mirefu na imara, lakini pia kazi ya kujenga tabia mpya na nzuri kwenye maisha yetu ni kama kupalilia na kutunza uwa zuri na laini ili lisivyauke kila siku.

    12. Muhimu kwenye maisha sio kuwa na malengo, bali ni kuwa na mfumo mzuri utakaokufanya uufuate mara zote ili ukuletee matokeo na kutimiza malengo yako.

    13. Jenga mfumo mzuri na imara ambao hautakuwa mgumu kuufuata, jenga mfumo ambao utafanya iwe rahisi kutimiza malengo ya maisha yako.

    14. Muhimu kwenye maisha sio kubadilisha matokeo, muhimu ni kubadilisha mfumo au system iliyoleta matokeo hayo.

    15. Ili tupate suluhisho la kudumu ni muhimu kutatua matatizo yetu kwa ngazi ya kimfumo na sio ngazi ya kimatokeo.

    16. Changamoto iliyopo kwa wanaoweka malengo ni kuahirisha furaha au baadhi ya mambo muhimu kwenye maisha, mfano kuna watu wanasema wakifanikiwa kutimiza malego fulani au wakifikia mafanikio fulani ndio watakuwa na furaha, watafanya jambo fulani nk.

    17. Kama utaendesha maisha yako kwa misingi ya kimfumo hutakuwa na muda wa kusubiria matokeo ndio ufurahi au uwe na amani, utakuwa na amani na utafurahia mchakato utakao kupeleka kwenye matokeo, hutahitaji ruhusu au wakati fulani maalumu ili uwe na furaha.

    18. Mafanikio makubwa kwenye maisha yanategemea kujitoa kwa kiwango kikubwa kubakia katika mchakato wa kufikia mafanikio yako, uwezo wako wa kubakia katika mchakato wa kufikia mafanikio yako unatakiwa kuwa mkubwa na wenye uvumilivu mkubwa.

    19. Tabia mbaya unazotaka ziondoke kwenye maisha yako huwa zinatabia ya kujirudia rudia kila mara hata bila ya wewe kujua; hii ni kwasababu kuna mfumo wa maisha unaouishi unaifanya tabia hiyo mbaya kuwa na nguvu ya kuendelea kutokea kwenye maisha yako.

    20. Jambo muhimu katika kubadili tabia mbaya uliyo nayo ni kubadili mfumo mbaya ulio nao. Ukiwa na mfumo mzuri utakuletea matokeo mazuri, na mfumo mbaya unaleta tabia mbaya.

    21. Atomic habit ni vitabia vidogo kama atomi ambavyo vinakuwa sehemu ya mfumo sahaihi ambao unaleta matokeo makubwa, kama vile ilivyo kwa atomi ni chembe ndogo sana ambayo huungana na kutengeneza kitu kikubwa sana.

    22. Mara nyingi ni ngumu kubadili tabia ambayo ni matokeo ya mapokeo na imani za tamaduni fulani, tabia ambazo zimetokana na mambo ya imani ni ngumu sana kuzibadili, maana ukitaka kuzibadili tabia hizi inabidi ubadili kwanza namna mtu anavyoamini kuhusu tabia hiyo.

    23. Kama kuna ufahari unaupata kutokana na jinsi ulivyo, au jinsi watu wanavyokutambua, ndio inaongeza hamasa ya kuendelea kuidhihirisha tabia hiyo.

    24. Tabia zinazobeba utambulisho wa mtu ni ngumu sana kuzivunja na pia ni rahisi kuunda tabia ambazo zinahusianisha utambulisho wa mtu.

    25. Kama unaona fahari ya nyele za kichwa chako jinsi zilivyo, lazima utatengeneza aina ya tabia ambazo zitakuasidia katika utunzaji wa nywele zako ili ziendelee kuonekana vizuri kila siku.

    26. Kama unaona ufahari juu ya mwili wako kuonekana imara na wenye afya, lazima utajenga tabia za kila siku za kuendelea kuutunza mwili wako na kufanya mazoezi ili uonekane kuwa imara mar azote.

    27. Mwandishi wa kitabu hiki James Clear anasema, unaweza kujenga tabia kwasababu umepata hamasa ya kujenga tabia hiyo, lakini ili uendelee kuwa na tabia ulioijenga ni muhimu tabia hiyo ikahusisha utu wako au ikawa sehemu muhimu ya utambulisho wako.

    28. Mfano, lengo lisiwe kusoma tu kitabu, lengo kubwa linatakiwa kuwa msomaji wa vitabu. Lengo lisiwe tu kukimbia, bali iwe kuwa mkimbiaji, lengo lisiwe kuwa mpiga vyomba bali liwe kuwa mwanamziki. Endapo utafikiri kwa namna hii katika kufanya mambo yako, utajenga tabia za kudumu ili uendelee kuwa msomaji, mkimbiaji na mwanamuziki mkubwa.

    29. Ni rahisi kufanya kama mtu ambaye unatamani kuwa. Na ujenzi wa tabia unakua rahisi endapo tabia zitahusisha kuwa mtu bora unayemtamani kuwa.

    30. Katika ujenzi wa tabia mpya, unaweza kuzalisha tabia bora na zikakusaidia kufikia ndoto zako, kwa upande mwingine unaweza kuzalisha tabia hatarishi ambazo zitakwamisha maisha yako. Chagua kwa usahihi ujenzi wa tabia muhimu kwenye maisha yako.

    31. Utambulisho wako au utu wako unatokana na tabia zako; hukuzaliwa na mapokeo na imani ulizo nazo na unazozijua kuhusu wewe mwenyewe, kila unachokiamini ulijifunza au umekutana nacho kwenye mazingira uliyoyazoea.

    32. Mazoea na uzoefu yamechangia sana kukupa mitazamo na imani ulizo nazo, ndio maana tabia nyingi hujengwa na kusitawi kupitia mazingira yanayotuzunguka.

    33. Jinsi unavyokoaa kwenye mazingira fulani kwa muda mrefu, mazingira hayo yanamchango mkubwa sana wa kukufanya uwe na tabia ambazo unazirudia rudia kila mara bila hata wewe kujua.

    34. Tabia ndio zinakujengea utambulisho wako, mfano, kama una tabia ya kuandika kila siku, utaishia kuwa mwandishi, kama una tabia ya kuimba kila siku utaishia kuwa mwimbaji, kama una tabia ya kupika kila siku utaishia kuwa mpishi, kama una tabia za kufundisha kila siku utaishia kuwa mwalimu.

    35. Kila hatua unazochukua kila siku ni kura yako unajipikia ili kufikia mtu unayetamani kuwa, hakuna ambalo unalifanya lisiwe na matokeo yake.

    36. Kila siku chagua aina ya mtu unayetaka kuwa, kisha thibitisha hilo kwa kuchukua hatua ndogo ndogo zinazokupa ushindi. Wewe sio jiwe, tabia yako sio jiwe kwamba haibadiliki, kila kitu kinaweza kubadilika endapo kitaandaliwa mfumo sahihi wa kubadilika.

    37. Mwandishi anasema, kuna aina 3 za mabadiliko, mabadiliko ya matokeo, mabadiliko ya mchakato na mabadiliko ya utu au utambulisho wako. Fikiria mtu bora unayetamani kuwa, kiasha jenga tabia za kufanya kila siku ili kufikia mtu huyo bora unayemtamani.

    38. Mwandishi James anaeama, tabia ni njia fupi ulizojifunza na kuzitumia kipindi cha nyuma ili kutatua changamoto ulizokutana nazo.

    39. Mazingira yale yale yakijirudia utatumia tabia ile ile kutatua changamoto ulizokutana nazo. Mazingira sahihi yanatukumbusha kuchukua hatua fulani zilizofanya kazi kipindi cha nyuma ili kutatua changamoto zinazotokea kwenye maisha.

    40. Usipokuwa na udhibiti mzuri wa tabia zako, zinaweza kuwa kikwazo kikubwa sana kwako, zinaweza kukunyima uhuru mkubwa sana.

    SOMA ZAIDI: Uchambuzi Wa Kitabu Cha The 5Am Club: (Mambo 304 niliyojifunza kutoka kwenye hiki kitabu)

    41. Siku zote fahamu zetu zinaangalia mazingira yote ya ndani na nje ili kujua ni sehemu gani zawadi zilipo. Kunakuwaga na msukumo mkubwa sana wa kufanya jambo fulani endapo jambo hilo limeambatana na zawadi baada ya kulifanya.

    42. Fahamu zetu zinaangalia sehemu ambazo tunaweza kupata matamanio yetu na ambapo tunaweza kupata utoshelevu na raha.

    43. Hisia za raha na karaha ni sehemu ya mchakato wa mrejesho wa taarifa ambao husaidia ubongo wetu kutofautisha kati ya matendo ya muhimu na yale yasiyo ya muhimu.

    44. Lengo la kila tabia ni kutatua changamoto zinazotokea kwenye maisha yetu kwa nguvu kidogo kwa kadri inavyowezekana. Mfano, kila siku unapovaa viatu au unapofunga kamba za viatu vyako, unatumia gharama na nguvu gani kufanhya hayo, ukiangalia utaona unatumia nguvu kidogo sana.

    45. Kuna kanuni na sheria za kubadili tabia yoyote ile, sheria hizo ni fanya tabia hiyo kuwa wazi, pili ifanye tabia hiyo kuwa ya mvuto, tatu ni kuifanya tabia hiyo kuwa rahisi na nne ni kufanya tabia hiyo kuwa na utoshelevu.

    46. Kuna vitu vinatokea kwenye maisha yetu bila hata sisi kufikiria vinatokeaje, mfano jinsi nywele zetu zinavyoota, jinsi mapigo ya moyo yanavyodunda, jinsi tunavyopumua, jinsi tumbo letu linavyomengenya chakula. Mambo haya yanafanyika katika miili yetu bila hata ya sisi kufikiri namna yanavyofanyika, sisi ni zaidi ya fahamu zetu.

    47. Mwanasaikolojia maarufu Carl Jung aliwahi kusema, inabidi tuyadhanie yale tusiyoyadhaia, bila kufanya hiyo mambo hayo yanaweza yakayaendesha maisha yetu hadi tukaishia kuona ni kama sehemu ya hatima yetu.

    48. Tunatakiwa kuzielewa kwa undani tabia zinazoendesha maisha yetu, ili ujue kama zinaweza kuleta majanga au hatari kwenye maisha, usipofanya tathimini ya tabia, unaweza kudhani baadhi ya tabia ulizo nazo ni haki yako na huwezi kuzibadili.

    49. Mwandishi wa kitabu hiki anasema, hakuna tabia nzuri wala tabia mbaya, tabia zote zina manufaa kwa namna moja au nyingine kwa mtu anayezitumia. Tabia zote huwa kuna tatizo zinatatua ndio maana watu wanaendelea nazo, tabia mbaya kuna namna zinawasaidia watu hata kama ni kwa muda mfupi.

    50. Namna ya kujenga tabia mpya ni kuisema kuisema angalau kila siku kwa nguvu, hii itatasidia kufanya tabia hiyo kuwa wazi sana kwako, lakini pia itakupa ufahamu wa uwepo wa tabia hiyo.

    51. Mfano, kama unataka kuacha tabia ya kula vyakula vyenye sukari, unapaswa kusema kwanguvu leo nataka kula chipsi mayai na soda, lakini nikila chipsi mayai sio nzuri kwa afya yangu maana zitaniongezea uzito na kisukari kwenye mwili.

    52. Unapoamua kujijengea tabia mpya kwenye maisha yako, itakuwa ngumu katika siku za mwanzo, lakini ukiendelea kuifanyia kazi kila siku, itafikia hatua itajiendesha yenyewe bila wewe hata kutumia nguvu. Na hapo inahitaji muda na uvumilivu mwingi.

    53. Kabla ya kuibadili tabia yoyote kwenye maisha yako, unahitaji kuifahamu vizuri tabia hiyo, ielewe tabia hiyo illivyo na namna inavyokufanya ukose furaha kila inapojitokeza.

    54. Kama unaweza kuiona na kuitaja tabia unayotaka kuibadilisha inatakufanya upate nguvu ya kuchukua maamuzi ya kuibadili tabia hiyo, mwandishi anasema kuitaja na kuisema kwa sauti tabia unayotaka kuibadili unajipa nguvu zaidi na ushawishi mkubwa wa kuibadili.

    55. Wengi wetu tunapenda kusema nitafanya hiki au nitafanya kile, au nitabadili hiki au kile, lakini hatusemi tutafanya lini, na wapi na kwa muda gani. Tunaishia kusema tu nitafanya nitafanya, lakini hatuweki maelezo ya kutosha kwenye ufanyaji wa jambo tunalotaka.

    SOMA ZAIDI: Uchambuzi wa Kitabu: The Leader Who Had no Title (Kiongozi Asiye na Cheo); Mambo 200 Niliyojifunza katika kitabu hiki.

    56. Ili kuongeza ushawishi wa kuchukua hatua kujenga tabia bora ni lazima tuweke bayana kabisa tabia ambayo utaifanya, muda ambao utaifanya, eneo ambalo utaifanya tabia hiyo. Mfano, saa tano asubuhi nitaenda ofisini kwa ajili ya kuandika makala kwa muda wa saa moja. Hapo umeiweka kabisa wazi hivyo inakupa nguvu ya kuchukua hatua na kufanya.

    57. Kuna watu wanakaa wakisubiri maisha yako yote ili muda uwe upande wao ndio waanze kufanyia kazi malengo na ndoto zao. Mwandishi wa kitabu hiki anasema, huna muda wa kusubiria kama unavyofikiri, chukua hatua mara moja.

    58. Wengi tunafikiri tumekosa hamasa ya kufanya mambo, mwandishi James anasema, hatujakosa hamasa, tumekosa uwazi, au ubayana kwenye yale tunayoyafanya. Mfano hutuweki bayana ni lini, na wapi, utafanya jambo lako, hivyo kusema tu utafanya haikupi ushawishi wa kutosha kuchukua hatua.

    59. Tunatakiwa kuwa na nia ya utekelezaji ambayo tumeiweka bayana kabisa, ili ikifikia wakati uliopanga kufanya jambo fulani kila kitu kiwe tayari, isiwe umefika wakati wa kufanya jambo lako unaanza kuwaza waza, na kuangalia mambo mengine, ambayo kwa kiasi kikubwa yanaweza kukutoa kwenye malengo na mipango yako uliyoipanga.

    60. Weka mazingira yote yawe bora kabisa kiasi cha kukuvutia uendelee kutekeleza tabia mpya, ainisha na weka bayana kabisa unachotaka ili ukipate. Usikubali mambo mengi yakufanye ushindwa kujenga tabia bora unayoitamani kwenye maisha yako.

    61. Mwandishi James Clear anasema, muda mzuri wa kuanza tabia mpya ni siku ya kwanza ya wiki, mfano siku ya jumatatu, mwandishi anasema, siku hii unakuwa na nguvu na hamasa na matumaini makubwa sana, hivyo ni rahisi kuanza jambo lolote siku ya jumatatu.

    62. Sehemu yenye matumaini inakupa sababu ya kuendelea kuchukua hatua, chagua kuwa na nyakati nyingi nzuri na zilizojaa matumaini ili upate sababu nyingi za kuendelea kufanyia kazi mabadiliko unayoyataka kwenye maisha yako.

    63. Ipe tabia yako mpya muda na nafasi ya kutokea na kuchanua hapa duniani, kila tabia bora unayotamani kuwa nayo kwenye maisha yako inawezekana kuitengeneza na kuipa mazingira yote wezeshi ili ichanue na kukuletea kila ulichokitamani na kukufanya kuwa mtu uliyemtamani.

    64. Jitamanishe tabia mpya unayoijenga kwenye maisha yako, jione ukiwa bora kwa kuiishi tabia hiyo, jenga shauku itakayokusukumba kuishi tabia hiyo kila siku mpaka iwe sehemu muhimu ya maisha yako ya kila siku.

    65. Hakuna tabia inayojijenga katika upweke, kuna uhusiano mkubwa sana endapo utajenga tabia mpya na nzuri, utaendelea kujenga tabia nyingine nyingi mpya na nzuri zinazoendana na tabia mpya uliyoijenga. Kanuni ya uhusiano huu inaitwa Diderot effect.

    66. Kanuni ya Diderot inasema unaponunua kitu kimoja inachochea kununua kingingine kinachoendana na hicho. Mfano, ukinunua nguo, utatamani ununue na viatu vinavyoendana na hiyo nguo, saa inayoendana na hiyo nguo nk. Kanuni hii inaweza kutumika vizuri kwenye uanzishwaji wa tabia mpya ambao utakufanya uanzishe tabia nyingine nzuri zinazoendana na tabia uliyoanzisha.

    67. Mwandishi James anasema njia nyingine ya kujenga tabia mpya ni kuijua tabia unayoiishi kila siku na kisha kuipachika tabia yako mpya juu ya tabia ya zamani. Mfano, kufanya tahajudi kwa dakika moja baada ya kuweka kahawa kwenye kikombe changu wakati wa asuhuhi.

    68. Pia unaweza kuongeza tabia ya kushukuru kila baada ya kukaa mezani wakati wa kula chakula cha jioni na familia yako; unaweza kufanya mazoezi kila utakapofika nyumbani na kubadili nguo za kazi na kuvaa za mazoezi wakati wa jioni ukitoka kazini.

    69. Hata kama wewe ni wa kipekee kiasi gani? Kuna tabia zinaweza kuibuka kwenye maisha yako kutegemea na mazingira yalivyo. Mazingira yana mchango mkubwa sana wa kujenga tabia na kuzikuza baadhi ya tabia nyingine. Kwenye kila mazingira utakayoishi au kukutana nayo, yatumie mazingira hayo kwa faida yako ili yawe sehemu ya kuimarasha tabia zako bora na kujenga nyingine bora zaidi.

    70. Mazingira yanaweza kukufanya ukaamua vingine kabisa na ulivyopanga au ulivyotarajia. Mfano, ukienda kwenye maduka ya nguo au bidhaa za fasheni utaona zile nguo au bidhaa zinye gharama na faida kubwa zinawekwa mbele kabisa ili zionekane vizuri na kila mtu, lakini zile bidhaa dhaifu na zisizo na faida kubwa zinawekwa mbali kwenye kona za maduka. Hapo ujue wanakulenga wewe ili ujichanganye ununue zenye faida kubwa kwao.

    71. Watafiti wanaonyesha kuwa, tunategemea sana vitu tunavyoviona kuliko hata milango mingine ya fahamu. Vitu tunavyoviona vina nguvu sana ya kugeuza mitazamo na misimamo yetu. Vingi tunavyoviona ndio vinatufanya kuamua mambo mengi kwenye maisha yetu. Ndio maana ukitaka kufanya biashara yenye mafanikio makubwa lazima uzingatie bidhaa zenye mvuto zaidi mbele ya macho.

    72. Kwenye kutengeneza tabia mpya, lazima uzingatie mazingira yenye mvuto, ifanye tabia mpya unayoipenda kuwa ya mvuto na inayokuvutia sana, kiasi kwamba utapenda kuifanya kila mara, hii inaenda sambamba na mazingra yenye mvuto sana katika kuikuza tabia hiyo.

    73. Wengi tunaishi kwenye dunia iliyoandaliwa na watu wengine, tunaishi kwenye mazingira yaliyoandaliwa na watu wengine kwasababu ya matamanio yao. Kama tunataka kuwa na ufanisi kwenye mambo tunayoyafanya inatakiwa kujitengenezea dunia na mazingira yetu wenyewe ambayo yatakuwa ndio mazingira bora sana kutimiza na kutekeleza jambo lolote kwa ufanisi wa hali ya juu sana.

    74. Mwandishi James Clear anasema, kuwa muundaji na mtengenezaji wa dunia yako, jitengenezee Edeni yako, ambayo kwa kukaa humo utaishi maisha bora, utafanya kazi zako kwa ufanisi na utakuwa mtu wa furaha, na utaifurahia dunia yako mwenyewe.

    75. Siku zote ni rahisi kusimamia na kuongoza kitu ambacho umekiunda na kukianzisha mwenyewe. Unakuwa na uongozi na umiliki wote na yote yaliyomo ndani ya mazingira uliyoyatengeneza.

    76. Tengeneza uhusiano mzuri na mazingira yako ya kazi, uhusiano ambao utakufanya kuchukua hatua zaidi na kufanya makubwa zaidi. Mfano, unaweza kutengeneza mahusiano mazuri na ofisi yako au sehemu unapokaa na kufanya kazi zako, ili ukifika tu eneo hilo hamu na shauku ya kufanya kazi iwe kubwa.

    77. Uwezo wa kufanya kila mazingira yawe yanaleta ufanisi kwako zaidi ni muhimu sana katika ujenzi wa tabia. Mfano, mwingine kochi ni kwa ajili ya kukaa na kuangalia TV, mwingine kochii ni sehemu yake bora ya kukaa na kusoma kwa muda mrefu. Hii ndio namna ya kushirikiana na mazingira yako kwa manufaa makubwa ili kujenga tabia mpya.

    78. Unaweza kubadili mazingira na kwenda sehemu nyingine tofauti ili ujitengenezee mazingira bora kwa ajili ya kupalilia tabia yako mpya. Mfano, unaweza kwenda hotelini, ukachagua kochi au kiti na meza unayoipenda kisha ukaamua kupafanya pakawa ndio sehemu yako bora ambayo ukikaa hapo unaweza kufanya kazi zako kwa ufanisi mkubwa.

    79. James Clear anasema kila tabia inatakiwa kuwa na nyumbani kwake. Usiache tabia ikatanga tanga mitaani bila kuwa na sehemu ambayo itapata utulivu, chakula na kukua ili iwe sehemu ya mafanikio yako kwenye maisha. Tabia zinatakiwa kutusaidia kufanikiwa na sio kutuangusha.

    80. Tengeneza mazingira yanayotabirika, mfano ukifika kitandani ni kulala na sio kufanya mambo mengine kama kuchati, ukifika mezani ni kula, ukifika ofisini ni kufanya kazi na sio jambo jingine. Tabia ili zikue zinahitaji mazingira yanayotabirika.

    81. Wakati mwingine ni rahisi kutengeneza tabia mpya sehemu mpya, au kwenye mazingira mapya, kwa sababu upo kwenye mazingira mapya ambayo hayana upinzani katika kukuza tabia mpya.

    82. Mwandishi anasema, uvumilivu, shauku, na matamanio makuwa ni mambo muhimu katika kufikia matokeo, lakini ili uwe na hayo yote unaweza kudhani unahitaji sana kuwa mtu wa nidhamu kubwa, nidhamu inatakiwa iwe kwenye mazingira ili yakufanya na wewe kuwa na nidhamu.

    83. Njia nzuri ya kuondoa tabia mbaya kwenye maisha yako ni kuondoka na kuondoa mazingira yanayokufanya uifanye tabia hiyo kirahisi, au ondoka na ondoa mazingira yanayofanya tabia hiyo iwepo hapo. Mfano, kama unaona unashindwa kufanya kazi kwasababu upo na simu yako karibu, unatakiwa uiondoe simu sehemu unapofanyia kazi na uiweke chumba kingine ili ufanye kazi zako kwa ufanisi.

    84. Kama kuna namna kwenye maisha yako unajiona hutoshi au hufai na umeachwa nyuma, mwandishi wa kitabu hiki anasema acha kabisa kufuatilia mitandao ya kijamii ambayo inakufanya ujione hutoshi, pia inakufanya uone wivu na ujione hufai.

    85. Kama unapoteza muda mwingi kuangalia TV kwasababu ipo tu sebuleni na unaikuta inawaka na ina vipindi vinavyokuvutia, mwandishi anasema, iondoe hiyo TV na uiweke kwenye chumba kingine ambacho huingii mara kwa mara.

    86. Kwenye ulimwengu tulionao sasa umetengeneza mazingira ya usumbufu mwingi sana, na usipojua unataka nini kwenye maisha yako, utajikuta unatumia muda wako mwingi kufuatilia maisha ya wengine, na kufuatilia vitu vya mitandaoni ambavyo havina tija kwenye maisha yako.

    87. Weka mazingira yawe magumu sana kwenye ufanyaji wa tabia mbaya ambazo huzipendi kwenye maisha yako, na pia weka mazingira rahisi, yenye mvuto kwa utendaji wa tabia nzuri unayotaka kuijenga kwenye maisha yako.

    88. Kama kitu kimekuvutia sana, kama kuna fursa imekuvutia sana, ni rahisi kuunda tabia kwenye vitu unavyovipenda maana vitakupa sababu na hamasa za kuifanya kila mara.

    SOMA ZAIDI: Uchambuzi Wa Kitabu: 25 Hours a Day; Going One More to Get What You Want

    89. Kama tabia unayoijenga inaendana na utamaduni wa jamii yako, mara nyingi inakuwa rahisi na kuvutia unapoifanya maana hutakutana na upinzani mkubwa kwenye utekelezaji wake.

    90. Mara zote huwa tunafuata tabia za tamaduni zetu hata bila kufikiri, wakati mwingine hata bila kuuliza, au bila hata kukumbuka. Hii ni kwasababu kila mtu anaiona ni sawa na kila mtu anaifanya na umezaliwa umekuta watu wanazifanya hiyo wewe kuzifanya haiwi jambo gumu.

    91. Mwandishi wa kitabu hiki anasema, tabia ni rahisi kuzitekeleza kama zinatufanya tuonekane ni sehemu muhimu ya jamii au kundi pale tunapoifanya. Kumbuka mara zote huwa tunaiga au kufuata tabia za makundi 3 muhimu sana kwenye jamii zetu, makundi hayo ni; watu wetu wa karibu sana, wingi wa watu, na wenye nguvu au ushawishi.

    92. Kama unataka kujenga tabia mpya na unayoipenda tafuta watu wanaoishi kwa tabia unayoitamani. Tafuta watu au kundi au jamii ambayo wanaishi tabia unayoitaka kisha jiunge nao, kwa kufanya hivyo utakuwa kwenye mazingira mazuri na rahisi kwa tabia yako kusitawi.

    93. Mfano, ukienda kwenye jamii au kundi la watu ambao kila siku asubuhi wanafanya mazoezi ya kujenga mwili, itakuwa rahisi kwako kujenga tabia ya mazoezi ya mwili kwasababu kuna mazingira mazuri ya kuifanya tabia hiyo ya mazoezi bila upinzani mkubwa.

    94. Mwandishi James anasema ili iwe rahisi kwako kujenga na kukuza tabia unazozipenda, ni vizuri ukazungukwa na watu au mazingira yatakayokufanya uijenge tabia yako kwa urahisi. Kama wewe unapenda muziki wa dansi, zungukwa na watu wanaoimba na kupenda mziki wa dansi.

    95. Makundi, watu wa karibu, na watu wenye nguvu ya kiuchumi huwa wana ushawishi sana, hivyo ukikaa miongoni mwa kundi moja wapo hapo, ni rahisi kujikuta ukifanya kama wao; kama wanapenda kusoma vitabu utajikuta na wewe ukitamani kusoma vitabu, kama wanafanya biashara na kuzungumza biashara, basi itakuwa ni rahisi sana kwako kunzisha biashara maana upo kwenye mazingira sahihi.

    96. Mara nyingi tuona ni bora kukosea tukiwa kwenye kundi kuliko kuwa sahihi sisi wenyewe. Maana yake makundi yana nguvu na ushawishi sana, hata kama kitu sio sashihi, wengi wakikipenda au kukifanya kinaonekana sahihi.

    97. Kuna watu wanavuta sigara wakidhani kuna watu wanawafurahia au kuwapenda kwa tabia hiyo. Mwandishi James anasema, huitaji tabia ya uvutaji wa sigara ili upendwe au uonekane kwenye jamii, kuna tabia nyingine nyingi nzuri na salama ambazo unaweza kuzitumia na zikakufanya kuwa maarufu na kupendwa.

    98. Kama unasumbuliwa na tabia ya uvutaji wa sigara, unachotakiwa kufanya ni kuifanya tabia hiyo kuwa mbaya na isiyo kuvutia kabisa. Hivyo tengeneza mazingira yote yawe magumu kwa uvutaji wa sigara, lakini pia ukitamani kuvuta sigara fanya tabia nyingine bora kuliko hiyo.

    99. Kuna muda mwingi sana tunatumia kupanga na kutamani vitu vifanyike kwa namna fulani, wakati mwingine tunasoma majarida au vitabu kupata taarifa ya kufanya jambo fulani tunalotamani; mwandishi anasema kuna upotevu mkubwa sana wa muda endapo hutachukua hatua haraka kutekeleza unayoyatamani.

    100. James Clear anasema, hakikisha unachukua hatua kutekeleza unayoyatamani, haina maana kupanga mambo mengi halafu huchukui hatua.

    101. Kama umeona tabia ya kufanya mazoezi ni muhimu kwa ajili ya afya yako usipoteze muda kuuliza uliza tena, unachotakiwa kufanya ni kutafuta vifaa vya kufanyia mazoezi na kuanza mazoezi mara moja.

    102. Kuna wengine wanajiandaa sana kiasi kwamba hamu ya kufanya jambo husika inaisha na kupotea.

    103. Kama umeona tabia ya kusoma vitabu ni muhimu sana kwenye maisha yako, usipoteze muda kujiandaa kwa hilo, ingia mara moja kwenye utekelezaji na uanze kusoma. Hii ni kwa wale wanaonunua vitabu vingi halafu hawavisomi.

    104. Njia nzuri ya kujifunza chochote ni kuchukua hatua, au kufanya mazoezi. Mwandishi James anasema kuna wakati mwingine maandalizi ni kama aina nyingine ya kughairisha jambo. Kama una jambo unalipenda kwenye maisha yako, kikubwa unachoweza kufanya ni kuchukua hatua na kuanza utekelezaji mara moja.

    105. Kama unataka kuchora hakikisha kila kitu unachohitaji kwa ajili ya uchoraji kipo mezani, kama vile penseli, karatasi, rangi, rula, ufutio nk. Vitu hivyo viwe karibu na ukifika mezani ni kuanza kuchora sio tena ukifika mezani unaanza kutafuta vitu vingine, weka mazingira yote yawe rahisi kwako ili uchore.

    106. Kama unataka kuanza kujenga tabia ya kufanya mazoezi kwa ajili ya afya ya mwili wako, weka vifaa vyote vya mazeozi sehemu inayoonekana, usivifiche mbali, na pia hakikisha una vifaa vyote unavyohitaji kwa ajili ya mazoezi kama vile viatu, nguo nk.

    107. Kama unataka kuboresha ulaji wako ili uwe ni wa afya, hakikisha vitu vyote unavyovihitaji kwa ajili ya mlo wako vipo, kama ni matunda, mboga mboga, maziwa, maji nk. Hakikisha vyote vinakuwepo. Pia usiweke karibu vyakula visivyojenga mwili kama vile soda, sukari, vilevi, chipsi nk vifanye vitu hivyo viwe vigumu kupatikana wala usivinunue na kuleta nyumbani kwako.

    108. Ifanya ratiba yako ya siku iwe rahisi sana kwako kuitekeleza, pia panga mambo yote unayoyaona yana umuhimu mkubwa kwenye maisha yako yawe rahisi kwako kuyafanya, na pia yafanye mambo yasiyo na tija kwenye maisha yako yawe ndio mambo magumu sana kwako kuyafanya.

    109. Kwa asili binadamu huwa tunapenda kufanya mambo rahisi yasiyotumia nguvu nyingi. Hivyo tengeneza mazingira ya kufanya mambo unayoyaona ni magumu lakini ni muhimu sana kwenye maisha yako yawe rahisi kwako kuyafanya.

    110. Ujenzi wa tabia unahitaji mazingira rahisi na yenye mvuto, kama unatumia nguvu kubwa, na upinzani ni mkubwa sana kujenga tabia mpya ni wazi kuwa huwezi kufurahia tabia hiyo, na pia ni rahisi kukata tamaa na kuendelea na tabia zako za awali.

    111. Unapojenga tabia mpya au kukuza tabia nzuri kwenye maisha yako, haitakiwi iwe kama ni changamoto. Ujenzi wa tabia unatakiwa kuwa wa mvuto mkubwa kwako, tabia zinatakiwa ziwe sehemu ya kukupa furaha na mafanikio. Hivyo fikiri tena kujenga tabia unayoipenda kwa kuweka mazingira rafiki kwa utekelezaji wa tabia hiyo.

    112. Kuna kanuni inaitwa kanuni ya dakika mbili; kanuni hii inasema unapoanza tabia mpya utekelezaji wake usizidi dakika mbili. Maana yake kama unaaza kesho kuishi tabia mpya jisemee nitatumia dakika mbili tu kuishi tabia hii mpya.

    113. Mwandishi James anasema, huwezi kuboresha kitu ambacho hujakianza, kama umeanza tabia mpya ni rahisi kuiboresha kadri siku zinavyokwenda ili iwe sehemu ya maisha yako.

    114. Kama unataka kuvunja tabia usizozipenda kwenye maisha yako, unatakiwa kuweka upinzani mkubwa sana kwenye utekelezaji wa tabia hiyo. Ifanye tabia hiyo iwe ngumu na isiyovutia kabisa kuitekeleza.

    115. Unaweza kutumia fursa za teknolojia zilizopo ili kuboresha tabia unayoipenda. Mfano kuna wengine wanapenda kufanya mazoezi ya mwili akiwa wanasikiliza musiki, au wengine wakivaa vifaa vya masikioni vinawafanya waongeze umakini kwenye majukumu yao.

    116. Kama kuna namna unapata raha unapofanya tabia fulani, ubongo wetu huwa una tabia ya kutukumbusha mara kwa mara kuhusu raha zilizopo katika kufanya tabia fulani. Hivyo unaweza kuhusianisha ujenzi wa tabia mpya na raha ya kitu fulani ili ikusaidie kukuza tabia mpya.

    117. Hisia chanya zinasaidia sana kukuza tabia mpya, lakini pia hisia hasi zinaua sana tabia mpya. Siku zote tunapenda kufanya na kurudia vitu ambavyo tunajua tukivifanya tutapewa au tutapata zawadi.

    118. Unaweza kujenga mfumo wa ufuatiliaji wa tabia yako, hii itasaidia ili muda wote uwe kwenye ujenzi wa tabia yako. Unaweza kutengeneza form malumu ya kujaza tabia unazoziishi na kama unazitekeleza.

    119. Sisi binadamu huwa tunajali sana maoni ya watu juu yetu, hivyo basi unaweza kumpa mtu jukumu la kukusimamia ili uweze kuishi tabia unazozipenda. Kwasababu hatupendi watu watuchukulie vibaya hii itatupa nguvu ya kuitekeleza tabia unayoipenda.

    120. Unaweza kutengeneza mkataba wa tabia, mkataba uweke wazi kabisa aina ya tabia unazotaka kuzijenga kwenye maisha yako, utazitekeleza siku gani, kuanzia saa ngapi na kwa muda gani? Pia mkataba huo uweke wazi faini au adhabu ambazo utazipata endapo utakiuka masharti ulivyoonyesha kwenye mkataba, njia hii itakusaidia kujenga tabia na kuziishi kwa mafanikio.

    121. Fanya kile unachokipenda kwenye maisha yako, soma kile unachokipenda, na jenga na ishi tabia unazozipenda. Usijenge wala kuishi tabia ambazo huzihitaji kwa kuogopa watu watakuonaje. Chagua tabia sahihi kwako zijenge na ziishi kila siku.

    122. Njia nyingine bora ya kuwa na tabia nzuri ya kudumu muda mrefu ni kuchagua kujenga tabia ambazo zinaendana na ujuzi wako, haiba yako, utalaamu wako na jinsi ulivyo. Kwa kufanya hivyo itakusaidia kuwa na utekelezaji mwepesi wa tabia unazotaka kuzijenga.

    123. Uchaguzi mbaya wa tabia unaleta utekelezaji mgumu, uchaguzi sahihi wa tabia unaleta utekelezaji rahisi. Chagua tabia kuendana na uwezo wako wa kipekee uliozaliwa nao. Chagua tabia zinazoendana na wewe. Mfano kama uwezo wako wa kipekee ni kuandika, unaweza kujenga tabia za kuandika kila siku na ikawa rahisi kwako kutekeleza.

    124. Cheza mchezo unaoendana na uwezo wako. Kama hakuna mchezo sahihi unaondana na uwezo wako, tengeneza mchezo wako mwenyewe kwa kujenga tabia mpya itakayokufanya ucheze mchezo huo.

    125. Chagua tabia ambayo utaifanya kila siku, usichague tabia za msimu, tabia za mafanikio zafaa sana kuwa tabia za maisha. Tabia ambazo utazifanya bila kujali unajisikiaje au upo kwenye hali gani, tabia za muda wote na sio za misimu fulani fulani tu.

    126. Hata kama zitatokea nyakati utakuwa chini na upo boadi sana, mwandishi anasema ifike mahali upende tu hali za kuboreka, maana hazikwepeki, zipende na zitumie kufanya makubwa. Tuwe na uwezo wa kufaidika na nyakati zote zinazokuja kwenye maisha yetu, hata kama ni ngumu kiasi gani.

    127. Kila mtu anaweza kufanya kazi kwa bidii kunapokuwa na hamasa na mazingira ni mazuri. Mwandishi anasema, mafanikio kwenye maisha yanadai matumizi ya nyakati ambazo hatuna hamasa kabisa ya kufanya chohote. Mafanikio na ukuaji mkubwa umefichwa kwenye nyakati ngumu, nyakati za giza, nyakati ambazo hatutamani tena kufanya chochote.

    128. Mafanikio sio lengo unalohitaji kufikia au msitari wa mwisho unaotakiwa kuuvuka, bali ni mfumo unaohitajika kuboreshwa na ni mchakato unaotakiwa kuimarishwa kila mara.

    129. Kama unapata tabu sana kubadili tabia zako, tatizo sio wewe, tatizo ni mfumo wako wa maisha, mfumo unafanya tabia uliyonayo ijiendeshe yenyewe hata bila wewe kujua. Ukibadili mfumo wako wa maisha ni rahisi kwa tabia kubadilika pia.

    130. Until you work as hard as those you admire, don’t explain away their success as luck.

    Mwisho; Kitabu hiki ni chepesi sana kusoma, na kina mambo mengi sana mazuri kuhusu kujenga tabia, kuvunja tabia usizozipenda na kujenga nyingine bora kabisa. Nashauri kila mtu akisome kitabu hiki.

    @Hillary Mrosso_13.11.2022

    /

X