Home


  • Namba Zetu Za Malipo

    Namba za malipo ya vitabu:

    Namba za lipa

    TIGO PESA: 19016638 Jina ni SONGAMBELE CONSULTANTS

    M-PESA: 5564517 jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

    Namba za kawaida

    AIRTEL MONEY: 0684408755
    TIGO PESA: 0655 848 392
    M-PESA: 0745 848 395

    Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    NB: Kama namba ya malipo anatumiwa mtu ambaye yuko nje ya nchi. Iandikwe Kwa kuanza na +255

    Kwa hiyo namba zinazotumwa nje ya nchi zitakuwa
    Airtel money: +255 684 408 755
    TIGO PESA: +255 655 848 392
    M-PESA: +255 745 848 395

    KOTE Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Kama malipo yatakuwa yanafanyika kupitia benki.

    Yafanyie kupitia

    1. CRDB BANK: 0150770710200
    2. NMB BANK: 22110047274

    Kote jina ni GODIUS GORDIAN RWEYONGEZA

  • Wasiliana na Godius Rweyongeza Sasa

    Habari yafuatayo ni mawasiliano Unayoweza kutumia kumpata GODIUS RWEYONGEZA

    Simu: +255 (0) 684408755

    Whatsap: +255 (0) 755848391

    Email: songambele.smb@gmail.com

    Kupata vitabu vyake wasiliana Moja kwa Moja na +255 (0) 684408755 (more…)

  • Ni nani anaruhusiwa kununua hisa na kwa Nini?

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy). Lipia kwa 0684408755

    Mwaka juzi nilikuwa naongea na ndugu mmoja kuhusiana na hali yake ya kiuchumi. Alikuwa katika hali mbaya kiuchumi.

    Nilimwuliza kama huwa ana tabia ya kuweka akiba. Akaniambia huwa anaweka akiba Ila huwa anaitumia siku chache mbeleni. Nikamwambia kuwa kwa Hali hiyo utapaswa kufungua akaunti benki ili uwe unaweka fedha zako huko. Lakini kikubwa zaidi nikamwambia anza kuwekeza pia kwenye soko la hisa kwa kununua hisa.

    Nikaanza kumweleza kuhusiana na hisa na namna zinavyofanya kazi.
    Nakwambia rafiki yangu, yule ndugu alinisikiliza kwa sababu Moja tu, kwa sababu muda ule tulikuwa tunatembea kwenda sehemu ili nimlipe kiasi fulani Cha fedha kwa kazi alivyokuwa amefanya.

    Ingekuwa siyo hiyo fedha, Nina uhakika siku hiyo asingenisikiliza….

    Baada ya kulazimika kunisikiliza katika mazingira Kama hayo, aliuliza swali kwa kusema. Hisa zenyewe zinauzwa bei kubwa…utakufa hisa moja inauzwa elfu sabini!

    Nilishangaa kuona anasema hivyo, lakini nikawa nimeendelea kumweleza kuwa kwa sasa kwenye soko la hisa la Dar Es Salaam hakuna hisa inayouzwa kwa bei kubwa hivyo.

    Sasa ambacho nimegundua watanzania wengi hawana elimu ya kutosha juu ya uwekezaji huu wa kwenye hisa.  Kama huamini toka nje sasa hivi uliza watu kumi tu kuwa wanajua Nini kuhusu uwekezaji kwenye hisa.
    Unaweza usipate hata mmoja wa kukupa jibu sahihi.

    Uwekezaji kwenye HISA ni uwekezaji ambao mtanzania yeyote anaruhusiwa kufanya. Ninaposema mtanzania yeyote namaanisha bila kujali Ni mtoto, kijana au mzee. Bila kujali Ni mrefu, mfupi, mwembamba au mnene. Bila kujali ni mhitimu wa darasa la saba, msomi wa chuo kikuu, dada wa nyumbani au ofisa anayefanya kazi ikulu.

    Wote tunayo haki ya kuwekeza kwenye soko la hisa kwa kununua hisa za kampuni yoyote tutakayoipenda

    Kwenye soko letu la hisa hata wageni wanaruhusiwa kuwekeza. Ila serikali yetu imetupendelea zaidi. Wageni (watu kutoka nje ya nchi) hawaruhusiwi kumiliki zaidi ya asilimia 60 ya hisa zote za kampuni iliyo kwenye soko la hisa.

    Serikali inafanya hivi ili kuwawezesha watanzania kuimiliki hisa, kumiliki uchumi na vitegauchumi.

    Rafiki yangu, changamka. Nenda kanunue hisa ili uanze kuimiliki kampuni na uchumi.

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Wekeza elfu tano tu, ujifunze uwekezaji kwenye hisa kwa kina. Kitabu Ni softcopy. Lipia kwa 0684408755

    Lakini kabla hujaenda kichwa kichwa kwenye kununua hisa, fanya hivi. Hakikisha umepata mwongozo wa kukusaidia kwenye uwekezaji kwenye HISA. Na mwongozo huu nimeandika kwenye kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Hiki ni kitabu ambacho unapaswa kutembea nacho popote pale utakapokuwa. Kitakusaidia sana kwenye uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Gharama ya kitabu hiki ni 5,000/-. Softcopy. Lipia kwa 0684308755 jina Ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Karibu sana

    Karibu ukipate

  • Mambo Muhimu ya KUZINGATIA kabla hujawekeza fedha Yako

    Kitabu hiki kinapatikana kwa 5,000/-. No softcopy

    Rafiki yangu mpendwa. Bila shaka unaendelea vizuri. Kila kunapokucha watu wanabuni njia mpya za kutaka kuondoka na kukaa na fedha zako. Watakuja kwako na maelezo mengimengi wakikushawishi uweze kuwapa fedha zako ambazo wewe mwenyewe umezitafuta kwa jasho na damu kubwa sana. Usipokuwa makini unaweza kujikuta unashawishika kutoa fedha zako kwa kila mtu anayekuja kwako kukwambia ana fursa nzuri ambayo ukiweka fedha utatajirika.

    Sasa ili kuepukana na Hilo, ningependa kwanza tujue vigezo muhimu vya kuzingatia kabla hujawekeza fedha zako. Chukulia tu mfano una milioni moja sasa hivi mkononi na unataka kuiwekeza. Utaiweka wapi? Je, utaiweka kweye hisa, hatifungani, vipande vya UTT, utanunua shamba au utanunua Kiwanja pembezoni mwa mji? Utawekeza kwenye kilimo,au utaenda Geita ununue gramu kadhaa za dhahabu? Utafanyaje ili fedha yako uiwekeze sehemu salama na ambayo itakupa mrejesho mzuri Bila kuharibu uwekezaji wako.

    Na kwa nini utawekeza huko?

    Vifuatavyo Ni vigezo muhimu unavyopaswa kuzingatia kabla ya kuwekeza fedha zako.

    (i) Mrejesho wa uwekezaji

    Kitu cha kwanza unachotakiwa kuangalia ni mrejesho gani utaupata kutokana na uwekezaji wako.  Hiki kigezo ambacho unapaswa kuangalia..

    Asilimia kubwa ya watu wanapowekeza huwa wanaangalia hiki kigezo peke yake. MTU anaambiwa weka laki moja tukupe laki tatu kesho kutwa, anakubali.

    Mrejesho wa uwekezaji Ni kigezo unachopaswa kuangalia,Ila kigezo hiki siyo mwanzo na mwisho. Kuna vigezo vingine vya kuangalia.

    Ni muhimu kama mwekezaji kupima iwapo uwekezaji anaouchagua utakuwa na matokeo yanayoridhisha na iwapo uwekezaji huo ni bora kuliko uwekezaji mwingine ambao unaweza kuufanya. Lakini hiki kisiwe kigezo peke yake Cha kuangalia.

    Kumbuka sehemu ambayo ina  mrejesho mkubwa na imekidhi vigezo vingine hapo chini  ni bora  kuliko sehemu yenye mrejesho  mdogo.

    (ii) Hatari za uwekezaji .

    Kama muwekezaji hauwezi kuangalia mrejesho wa uwekezaji tu bila kuangalia hatari za uwekezaji ambazo unazibeba pale ambapo unakuwa unawekeza katika uwekezaji wa aina fulani,

    Mfano kama kuna msitu ambao umeambiwa una dhahabu ambazo ukifika unaokota tu kama mawe ila ukaambiwa huo msitu ni hatari una kila aina ya wanyama ambao ukiingia tu wanakugawana ndani ya sekunde, kama mtu mwenye hekima utapima, ni kweli huu msitu una dhahabu tele ila uwezekano wa kutoka na dhahabu ni asilimia 0.0001%,uwezekano wa mimi kupoteza maisha katika huo msitu ni mkubwa kama bado unajali maisha yako  basi utaachana na  hiyo dili maana  ni dili la  moto !

    Katika uwekezaji vivyo hivyo hatuangalii tu mrejesho wa uwekezaji tunaangalia pia hatari za uwekezaji kama zinatufaa, nikuongezee kitu hapa kwa kadri unavyobeba hatari kubwa za uwekezaji basi na mrejesho wako uwe mkubwa ili kufidia hatari ambazo umezibeba, kwa hiyo kitu cha pili huwa tunagawanya uwekezaji kuendana na hatari za uwekezaji,

    kama unaona hatari za uwekezaji ni kubwa Sana kiasi kwamba utapoteza uwekezaji wako basi achana  na  huo uwekezaji. Hatari za uwekezaji ni ule uwezekano wa kuwa unachokitegemea kukipata kinaweza  kisitokee

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy) 0755848391

    (iii) Ukwasi  wa uwekezaji (liquidity)

    Sehemu hii nayo ni muhimu kwa muwekezaji makini. Ili kutengeneza fedha ni lazima uwe na uwezo wa kuuza uwekezaji wako pale unapohitaji kufanya hivyo.

    Ukwasi maana yake ni uwezo wa kubadilisha uwekezaji wako kuwa katika mfumo wa pesa . Uwekezaji unaoelezwa kuwa na ukwasi maana  yake ni uwekezaji ambao ni rahisi kuubadilisha kuwa fedha na uwekezaji unaoelezwa kuwa hauna ukwasi maana yake ni uwekezaji usio rahisi kubadilishwa kuwa fedha hasa pale inapotakiwa na mwekezaji.

    Kama ukwasi una shida maana yake siku ukitaka fedha zako kwa haraka unaweza kutoa macho kama mjusi kwani hutapata wa kumuuzia uwekezaji wako. Katika uwekezaji ambao nimetaja hapo juu kila uwekezaji una sifa yake katika sifa hizi nne je ni uwekezaji gani unaona unakufaa?

    Mfano uwekezaji kwenye ardhi ni mzuri ila ukwasi wake ni mdogo. Unaweza kuwa na kiwanja au nyumba, lakini mpaka uiuze upate fedha keshi, inakuwa na mlolongo mrefu na haupati fedha pale unapoihitaji.

    (iv) Usalama wa uwekezaji wako

    Hapa kuna watu wengi wamepoteza pesa kwa kuwekeza sehemu ambazo hazina usalama ila zinatoa ahadi ya mrejesho mkubwa.

      Kuna watu ambao hawana uelewa wa masuala ya kifedha au wanataka kupata utajiri wa haraka basi wanaingia kuwekeza kwenye biashara za upatu au biashara zisizo na uhakika wa mrejesho wa fedha na mwisho wa siku wanapoteza pesa.

    Usalama wa uwekezaji wako ni moja ya kigezo muhimu sana kama unataka kuwekeza, ni lazima sehemu ambayo unataka kuwekeza iwe na usalama wa pesa yako.  Waswahili wanasema ndege aliye mkononi ni bora kuliko ndege wawili walio porini, katika uwekezaji sheria namba moja ni kuwa usipoteze pesa yako kwa kuwekeza sehemu ambayo si salama.

    Na sheria ya pili Ni kuwa usisahau sheria ya kwanza.

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Wekeza 5,000 tu ujifunze maarifa muhimu kuhusu uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. 0755848391

    (v) Malengo yako 
    Kuwa na malengo katika kutimiza mipango yako ni muhimu. Katika uwekezaji ni muhimu kuwa na malengo. Malengo yanakupa mwongozo wa eneo gani uwekeze na wapi usiwekeze.

    Mfano mtu anayewekeza kwa akilenga kupata gawio la ambalo atatumia. Hawezi kuwekeza sawasawa na MTU ambaye anawekeza ili kuimiliki kampuni.

    Vi) Nani yupo nyuma ya uwekezaji huo?
    Ni muhimu sana kabla ya kuwekeza kujua nani Atakuwa nyuma ya fedha utakazoweka. Uongozi mzuri unaleta fedha zaidi kwa wawekezaji. Uongozi mbaya unaleta hasara.

    Vii) Mahali fedha itakapowekwa
    Unapaswa kujua kwa uhakika kuwa nikiweka fedha yangu hapa, hii fedha itawekezwa kwenye maeneo gani. Kama watu wanakushawishi uwekeze fedha kuwa utapata faida kubwa. Jiulize Ni biashara gani watakuwa wanafanya.

    Ni jukumu lako mwekezaji kujihakikishia kuwa eneo unapowekeza Ni eneo zuri na linalokufaa.

    Usihadaike tu kwa sababu uneambiwa utapata faida kubwa.

    Vii) Idadi watu wanaokimbilia kuwekeza
    Mara nyingi watu wa kawaida huwa wanaokimbilia kuwekeza kwenye miradi feki. Hii Ni kwa sababu huwa hawafuatilii na kujifunza kwa kina kuhusu uwekezaji.

    Wanawekeza na walizwa. Ukiona watu wengi wanaokimbilia kwenye uwekezaji husika, ufuatilie kwa ukaribu zaidi kabla hujawekeza. Mara nyingi utakufa huo uwekezaji Ni feki.

    Ni Mara nyingi sana utasikia watu wakiwekeza kwenye Aina mbali mbali za uwekezaji na kulizwa. Lakini Ni Mara ngapi umesikia watu wanaongelea uwekezaji kwenye hisa zinazouzwa kwenye soko la hisa la Dar Es Salaam? Au vipande vya UTT?

    Soko la hisa la Dar limekuwepo kwa zaidi ya miaka 20 Sasa na mifuko ya uwekezaji wa pamoja ya UTT, imekuwepo kwa zaidi ya miaka 15. Watu wanawekeza huko kila mwaka, Ila Ni Mara ngapi umesikia watu wakiuongelea huu uwekezaji?

    Kaylinda je?

    Vii). Umri
    Hiki Ni kigezo kingine Cha kuangalia wakati unawekeza. Umri siyo namba tu, Bali una kitu Cha kutwamvia kuhusu uwekezaji.

    MTU anayestaafu au anayekarivia kustaafu, hawezi kuwekeza sawasawa na mwanafunzi wa kidato Cha nne.

    Ndio maana nataka nashauri kila mmoja ahakikishe amepata mwongozo wa kitabu cha uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande. Kinaitwa MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

    MWISHO: Haya masuala ya kuambiwa wekeza laki tukupe laki mbili baada ya siku mbili yaepuke sana. Hakuna biashara inayoweza kukupa uhakika wa kupata tu kwa asilimia 100. Kila biashara ina kiwango chake hatari.

    Unapokuwa unawekeza fuatilia, kila kitu unachohitaji kujua kuhusu biashara husika. Usiwekeze tu kwa mkumbo.

    Hakikisha una nakala ya kitabu Cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Kinauzwa 5,000/-. Softcopy. Nitakutumia kwa whatsap au baruapepe.

    Karibu sana.

  • Hivi vitu ndivyo vinavyotofautisha uwekezaji kwenye hisa na uwekezaji kwenye maeneo mengine kama nyumba, kilimo cha miti na vito vya thamani

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)

    Leo rafiki yangu nataka nikwambie vitu vinavyoafanya uwekezaji kwenye hisa kuwa ni uwekezaji wa kipekee kuliko uwekezaji wa maeneo mengine kama nyumba, kilimo Cha miti na vito vya thamani. Kinachotofautisha uwekezaji huu Ni:

    Moja, unaweza kuanza kuwekeza kwenye HISA kwa kiwango kidogo tu Cha fedha .
    Ili unielewe vizuri unapaswa kujua kuwa kiwango cha chini kabisa Cha uwekezaji kwenye hisa ni hisa 10.

    Hivyo, ukiwa na fedha ya kununua hisa kumi tu, unaweza kuanza uwekezaji wako kwenye hisa. Sasa swali la kujiuliza hapa ni kuwa Ni fedha kiasi gani inahitajika ili kumwezesha mtu kununua hisa kumi?
    Ukweli ni kuwa hakuna kiwango rasmi cha kukuwezesha kununua hisa kumi, ila kiasi Cha fedha kinategemea na bei ya hisa kwenye soko kwa wakati husika.
    Mfano, sasa hivi ninapoandika hapa.
    Bei ya chini kabisa ya hisa ya kampuni mojawapo kwenye soko la hisa ni shilingi 120. Hii ndio kusema kuwa kama unanunua hisa kumi za kampuni utatakiwa kuwa na shilingi 1200/- ukiongeza na gharama za madalali hii unaweza kufikia 2200/- hivi.

    Hivyo, kwa kiasi kidogo Cha 2200/- unaweza kuanza kumiliki hisa za kampuni hiyo.

    Na hisa zinazouzwa bei ya juu kwa sasa ninapoandika hapa zinauzwa kwa shilingi  16,200/-. Hii ndio kusema kuwa thamani ya hisa kumi itakuwa Ni sawa na 162,000/-. Tukiongeza gharama za madalali unaweza kutoa kiasi Cha 163,300/-.

    Kwa hiyo, kwa kiasi Cha 163,000/- unaweza kuanza kuimiliki hisa za kampuni hii.

    Ila jambo Kama hili haliwezekani kwenye uwekezaji mwingine. Hivi kweli rafiki yangu unaweza kumiliki nyumba kwa kuanza na shilingi 2200/- au 163,000/-.

    HAIWEZEKANI.

    Pili, hisa zinatoa mwanya wa kununua kidogokidogo. Unaweza kununua hisa kumi leo. Kesho hisa hamsini. Siku nyingine hisa kumi na tano na kuendelea. Ila huwezi kuwekeza kwenye NYUMBA kwa kuanza kununua chumba leo, baada ya wiki ukanunua sebule, halafu siku nyingine ukanunua choo😂😂.
    Ni au ununue kitu chote kizima au la umekikosa…

    Nakushauri rafiki yangu uchangamkie uwekezaji kwenye hisa kwa kupata elimu sahihi ambayo utaanza kuitumia kuanzia Leo hii. Pata kitabu changu Cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Kwenye hiki kitabu utajifunza mengi kuhusu uwekezaji huu wa kipekee kwenye maeneo haya ya hisa, hatifungani na vipande.

    Fanya uwekezaji wa shilingi 5,000/-tu siku ya leo. Ili uweze kupata kitabu hiki. Lipia kitabu hiki kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

    Kumbuka kitabu hiki kinapatikana kwa njia ya mtandao (Kama ebook au softcopy). Na gharama yake ni 5,000/- tu. Ukilipia elfu tano, utatumiwa kitabu hiki kwa baruapepe au WhatsApp. Lipia Sasa. Namba ya malipo ni 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA..

    Umekuwa nami
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Hili ndilo kosa moja kubwa wanalofanya watu kuhusu kuwekeza

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)

    Hili ndilo kosa moja kubwa wanalofanya watu kuhusu kuwekeza

    Rafiki yangu jamii yetu imejuwa haiewi vizuri uwekezaji. Kitu hiki kimewafanya watu wajihusishe na miradi feki na ambayo haieleweki na hata wakati mwingine kutapeliwa.

    Moja ya kosa ambalo watu wamekuwa wanafanya kuhusu uwekezaji Ni kusubiri mpaka watakapokuwa na fedha ili waanze kuwekeza.

    Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu. Usisubiri mpaka uwe na pesa ili uanze kuwekeza. Anza na kile ulichonacho

    Kwenye makala yangu ya jana, nilikueleza ni kwa namna gani unaweza kuanza kuwekeza kwenye hisa kwa kununua walau hisa kumi tu. Hisa kumi zinagharimu fedha ya kawaida ambayo ukichagua vizuri unaweza kuimudu.

    Ubora wa wewe kuanza kuwekeza sasa hivi Ni kuwa kadiri uwekezaji wako utakavyokuwa unakua, wewe pia utakuwa unaongeza maarifa yako zaidi na zaidi. Na hivyo, kuendelea kubobea na kufanya maamuzi sahihi zaidi.

    Nikwambie kitu rafiki yangu, usisubiri mpaka uwe na kila kitu ili uanze kuwekeza. Anza kuwekeza hata kwa kutumia kiasi hicho kidogo ulichonacho sasa.

    Nakushauri, upate kitabu changu Cha Maajabu ya kuwekeza kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Kitabu hiki kitakufaa sana na KItakupa mwongozo unaouhitaji ili uanze kuwekeza.

    Usisubiri mpaka uwe na kila kitu ili uanze kuwekeza.
    Imeandikwa nami rafiki yako
    Godius Rweyongeza
    0755848391
    Morogoro-Tz

  • Kitu kimoja ambacho watu hawajui kuhusu uwekezaji

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)

    Rafiki yangu, najua Kuna aina mbalimbali za uwekezaji. Uwekezaji kwenye ardhi na NYUMBA (real estate), mali zisizo hamishika, uwekezaji kwenye kilimo cha miti, hisa, hatifungani na vipande  na uwekezaji mwingine.

    Hata hivyo kitu kimoja ambacho watu hawajui Ni kuwa, uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande ni uwekezaji ambao unaweza kuanza kuifanya hata kama huna mtaji mkubwa.

    Kwa mfano, ili uwe mwekezaji kwenye ardhi na nyumba tena ukiwa mjini, unakuta inakugharim mpaka milioni 50 na zaidi.

    Lakini kwa upande mwingine, uwekezaji kwenye hisa Ni tofauti. Ili uwekeze kwenye hisa, kiwango Cha chini Cha kuwekeza kwenye HISA Ni hisa kumi tu.
    Ambapo kiasi konachohitajika kwa pamoja kitategemea na Bei ya hisa kwa wakati husika.
    Mfano, Leo hii ninapoandika hapa. Mojawapo ya kampuni kwenye soko la hisa Bei yake ni 120. Hii ndio kusema kuwa Kama unanunua hisa kumi unatakiwa kuwa na shilingi 1200/-. Ukiongeza gharama nyingine za madalali maana yake inafika karibia 2300/-

    Kwa hiyo, ukiwa na 2300/- unaanza kuwa mwekezaji. Na bado unaweza kuendelea kuwekeza zaidi kadiri siku zinavyoendelea.

    Hakuna uwekezaji kwenye ardhi unaoweza kuufanya kwa  2300/-

    Na hata ukiangalia ukiangalia hisa zenye Bei kubwa. Nikiangalia Bei za mwisho Jana wakati soko la hisa linafanyika . Hisa za Bei ya juu zilikuwa ziliuzwa kwa 16,200/-
    Ili ununue hisa kumi maana yake unapaswa kuwa na 162,000/- ambapo ukiongeza na gharama nyingine za madalali inafikia 163,100/-

    Bado kwenye ardhi hiki kiwango Ni kidogo Sana kukufanya ufanye uwekezaji wa maana. Ila kwenye hisa, inawezekana.

    Rafiki yangu, ninachotaka kukwambia Leo Ni kuwa, Ni rahisi sana kuwekeza kwenye HISA kuliko ilivyo kuwekeza kwenye eneo jingine. Maana kiwango Cha kawaida Cha pesa ndicho kinahitajika kuanza nacho unapowekeza

    Chukua hatua uanze kuwekeza kuanzia leo. Kwa kuanzia nashauri upate nakala ya kitabu changu Cha Maajabu ya kuwekeza kwenye HISA HATIFUNGANI NA VIPANDE.

    KItakupa mwongozo na kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Kupata nakala ya kitabu hiki utapaswa kulipia 5,000/- kwa ajili ya softcopy ya kitabu hiki.

    Lipia Sasa kwa AIRTEL MONEY:  0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA
    Au tuwasiliane kwa 0755848391.

    Karibu sana

    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
    Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)

  • Kitu Hiki Ndicho Kinawafanya wengi washindwe kufanya makubwa

    Habari ya leo rafiki yangu, bila shaka unaendelea vyema kabisa.

    Leo ningependa nikwambie kitu ambacho kimekuwa kinawakwamisha watu wengi na kuwafanya washindwe kufanikisha makubwa . Kitu Hiki siyo kingine bali ni kukosa malengo makubwa ambayo wanayafanyia kazi kwenye maisha yao.

    Ili uweze kunielewa vizuri hapa naomba nianze kwa kukupa mfano wa kawaida tu, unaweza kukuta MTU anadaiwa hela.
    Anapambana kwa nguvu zake zote kutafuta pesa ili alipe deni lake.

    Na kweli pesa anapata na deni analilipa, Ila akishamaliza kulipa deni anakosa msukumo wa kuendelea kupambana na kutafuta pesa zaidi ili kununua Uhuru wake wa Kifedha.

    Au unaweza kukuta mtu anatembea kinyonge. Lakini inapotokea hatari ya ghafla, MTU huyo anaruka na kukimbia Kama vile siyo yeye.

    Huu uwezo tulionao siyo TU tuitumie wakati wa hatari peke yake, bali tuitumie pia muda mwingine ambao siyo wa hatari pia. Kwa ajili ya kufanya makubwa

    Kinachowafanya wengi washindwe kuutumia huu uwezo mkubwa Ni kwa sababu hawana malengo. Unapokuwa hauna malengo, maana yake unashindwa kujisukuma maana hauna kitu chochote cha kukusukuma.

    Rafiki yangu Mara zote kuwa na melengo ambayo unayafanyia kazi. Malengo yawe makubwa na yakusukume muda wote kujituma na kufanya kazi kwa bidii.

    Kama hauna malengo basi kaa chini Uweke malengo sasa.

    Malengo ni Moto wa kukusukuma wewe kufanya Yale ambayo wengine wanaona kama hayawezekani.

    Tenga muda leo hii ukae chini Uweke malengo. Muda huu ni uwekezaji ambao unaufanya. Kwa ajili ya kesho yako.

    Nataka tu ufahamu kuwa bila ya kuwa na malengo, hutajisukuma kufanya kitu Cha maana.

  • Jinsi ya kupata mafunzo yenye hadhi ya chuo

    Brian Tracy anasema kuwa muda ambao tunautumia kwa siku tukisafiri na Kutembea kutoka eneo moja kwenda jingine, ukiuunganisha baada ya mwaka mmoja Ni sawa na semester moja ya chuo!

    Hii ndio kusema Kuwa ukiutumia vizuri huu muda, kujifunza. Baada ya mwaka utakuwa umepata kozi yenye hadhi ya semester ya chuo.

    Nataka hili likutafakatishe uanze kuona Ni kwa namna gani umekuwa unapoteza muda mwingi ambao huutumii wakati wa safari na wakati unatembea. Muda ambao kwako ungeweza kuwa muda wa kujifunza na kupata mafunzo yenye hadhi ya kozi ya chuo.

    Na nitafurahi ukianza kuutumia vizuri huu muda.

    Kwa kulifahamu hili, Ni nimekuandalia vitabu vyangu kwa mfumo wa sauti (Audiobook) ili uweze kuutumia muda wako wa safari kusikiliza Audiobook hizi.

    Na hiki ndicho kitu ambacho nataka tufanye siku ya leo.

    Pata Audiobook zangu tatu kwa kulipia Audiobook moja tu.

    Kwa kawaida Audiobook moja huwa naiuza kwa shilingi 20,000/- kwa hiyo Audiobook tatu ni sawa 60,000/-

    Ila Leo hii nataka ulipie Audiobook moja.nikupe nyingine mbili bure kabisa

    Audiobook zilizopo Ni pamoja na

    1. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

    2. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO

    3. MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE

    Lipia Audiobook moja siku ya leo. Upate nyingine mbili bure.

    Karibu

    Namba ya malipo ni 0755848391

    Jina ni GODIUS RWEYONGEZA

    Karibu.

  • Leo ni siku ya waandishi duniani: Mambo mawii unayopaswa kufahamu

    Habari ya siku ya hii ya kipekee sana rafiki yangu. leo ni siku ya waandishi duniani. Mimi ni kiwa mmoja wa waandishi, hii siku inanihusu sana. lakini pia inakusu wewe, maana hakuna mwandishi bila msomaji. Hivyo, siku ya leo ni siku yetu sote. Kwa hiyo, nitakuwa sijakosea kusema kwamba kheri ya siku ya waandishi kwako!

    Sasa kwenye siku hii ya waandishi kuna mambo yafuatayo ambayo ningependa uweze kuyafahamu.

    Kwanza, ni kuwa tumia saa chache zilizobaki, kuhakikisha kuwa unaandika ujumbe mfupi kwa mwandishi umpendaye. Mtumie ujumbe wa kumpongeza ili kumtia moyo kwa kazi yake nzuri anayofanya.

    Pili, kujinyakulia kitabu cha jinsi ya kuwa mwandishi mbobevu. Mwakani ningependa kuona kitabu chako ili wakati tunasherehekea waandishi mwaka 2023. Na wewe uwe kwenye hiyo orodha.

    Ndiyo maana nataka na wewe ujinyakulie ofa ya kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU. Gharama ya kitabu hiki ni 5,000/- ila kwa leo tarehe 1 na kesho tarehe 2, utakipiata kwa 4,000/.

    Lengo langu nataka mwakani, wewe uwe miongoni mwa waandishi tutakaosherehekea sikukuu yao.

    Tuma 4,000/- tu kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA ili niweze kukutumia kitabu hiki. Usichelewe maana muda wa ofa ni mchache sana, na ofa hii haitajirudia tena.

  • Usipokata tamaa…

    Mwisho wa siku usipokata tamaa, ukiendelea kuweka juhudi na kujituma bila kurudi nyuma, matokeo utayaona.

    Kwa hiyo ujumbe wangu kwako siku ya leo Ni kuwa endelea kuweka juhudi zaidi kwenye Kazi. Yajayo yanafurahisha.

  • Vitu viwili ambavyo huwafanya watu washindwe kupiga hatuaRafiki yangu, bila shaka unaendelea vyema.

    Rafiki yangu, bila shaka unaendelea vyema. Mimi hapa nilipo, niko sawa kabisa. Kuna vitu viwili kwenye maisha ambavyo huwafanya watu washindwe kufanikisha malengo na ndoto zao.

    Lengo la mimi kukwambia vitu hivi ni kuwa wewe unapaswa kuvifahamu hivi vitu viwili na kuviepuka, la sivyo utaishi maisha ya kawaida Kama ambavyo watu wengine wanaishi.

    Vitu hivyo viwili Ni

    Moja KUTOKUWA NA MALENGO AU NDOTO KUBWA
    Wengi wanaamka kila siku na kwenda kufanya kazi. Ila hawana malengo na ndoto Kubwa zinazowasukuma. Hiki Ni kitu kibaya, maana bila malengo na ndoto Kubwa ambazo zinakusukuma, utakosa motisha ya kufanya makubwa. Na hivyo, hutaweza kufika mbali kwenye maisha. Rafiki, yangu, Kama hauna malengo, Basi Leo hii, kaa chini na uweke malengo ambayo utaanza kuyafanyia kazi.

    Kwenye maisha yako, rafiki yangu, hakikisha Mara zote una malengo au ndoto kubwa unazozifanyia kazi. Malengo ni ramani ya kule unapotaka kuelekea. Kwenye maisha hakuna ambaye huwa anapanga kushindwa , Bali watu hushindwa kupanga. Nakuomba kitu kimoja tu rafiki yangu, usishindwe kupanga

    Pili, ni KUTOKUWA TAYARI KULIPA GHARAMA
    Siku hizi watu wengi wanapenda Ssna njia za mkato ili kupata mafanikio ya haraka . Rafiki yangu, njia ya mafanikio inakuhitaji ulipe gharama.
    Na zipo gharama sita ambazo utapaswa kulipa kama ambavyo nimezianisha kwenye kitabu changu Cha jinsi ya kufikia ndoto zako.
    Kitu kikubwa unachohitaji kujua ni gharama kiasi gani upo tayari kulipa ili kufikia mafanikio unayotaka. Kama hauko tayari kulipa gharama ujur hutaweza kufikia ndoto na malengo makubwa.

    Unaweza kupata Audiobook ya kitabu Cha Jinsi ya kufikia NDOTO ZAKO leo hii kwa kulipia 20,000/- tu. Nitakutumia Audiobook hii pamoja na Audiobook nyingine mbili bure kabisa
    Audiobook nyingine mbili nitakazotumia bure Ni
    1. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
    3. Maisha Ni FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE

    Rafiki yangu, lipia Audiobook moja upate mbili bure

    Vitu viwili ambavyo huwafanya watu washindwe kupiga hatua

    Rafiki yangu, bila shaka unaendelea vyema. Mimi hapa nilipo, niko sawa kabisa. Kuna vitu viwili kwenye maisha ambavyo huwafanya watu washindwe kufanikisha malengo na ndoto zao.

    Lengo la mimi kukwambia vitu hivi ni kuwa wewe unapaswa kuvifahamu hivi vitu viwili na kuviepuka, la sivyo utaishi maisha ya kawaida Kama ambavyo watu wengine wanaishi.

    Vitu hivyo viwili Ni

    Moja KUTOKUWA NA MALENGO AU NDOTO KUBWA
    Wengi wanaamka kila siku na kwenda kufanya kazi. Ila hawana malengo na ndoto Kubwa zinazowasukuma. Hiki Ni kitu kibaya, maana bila malengo na ndoto Kubwa ambazo zinakusukuma, utakosa motisha ya kufanya makubwa. Na hivyo, hutaweza kufika mbali kwenye maisha. Rafiki, yangu, Kama hauna malengo, Basi Leo hii, kaa chini na uweke malengo ambayo utaanza kuyafanyia kazi.

    Kwenye maisha yako, rafiki yangu, hakikisha Mara zote una malengo au ndoto kubwa unazozifanyia kazi. Malengo ni ramani ya kule unapotaka kuelekea. Kwenye maisha hakuna ambaye huwa anapanga kushindwa , Bali watu hushindwa kupanga. Nakuomba kitu kimoja tu rafiki yangu, usishindwe kupanga

    Pili, ni KUTOKUWA TAYARI KULIPA GHARAMA
    Siku hizi watu wengi wanapenda Ssna njia za mkato ili kupata mafanikio ya haraka . Rafiki yangu, njia ya mafanikio inakuhitaji ulipe gharama.
    Na zipo gharama sita ambazo utapaswa kulipa kama ambavyo nimezianisha kwenye kitabu changu Cha jinsi ya kufikia ndoto zako.
    Kitu kikubwa unachohitaji kujua ni gharama kiasi gani upo tayari kulipa ili kufikia mafanikio unayotaka. Kama hauko tayari kulipa gharama ujur hutaweza kufikia ndoto na malengo makubwa.

    Unaweza kupata Audiobook ya kitabu Cha Jinsi ya kufikia NDOTO ZAKO leo hii kwa kulipia 20,000/- tu. Nitakutumia Audiobook hii pamoja na Audiobook nyingine mbili bure kabisa
    Audiobook nyingine mbili nitakazotumia bure Ni

    1. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
    2. Maisha Ni FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE

    Rafiki yangu, lipia Audiobook moja upate mbili bure

X