Mbinu Muhimu Ya Kujenga Mafanikio Katika Biashara


Wajasiriamali wana mchango katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu. Wajasiriamali ni chimbuko la vipato ambavyo husaidia kujenga uchumi wa watu kupitia biashara zao. Wajasiriamali wanatoa ajira kwa vijana wengi na hivyo kuwasaidia kupata kipato chao na kupata kitu cha kuweka mkono kinywani. Kuna mbinu mbalimbali ambazo wajasiliamali wanaweza kuzitumia ili kujenga mafanikio katika biashara zao.

  1. Fanya kile unapenda
Kama wewe ni mjasiliamali fanya kile unachokipenda.Usiingie katika ujasiliamali kwa kufanya tu kile ambacho umeona wengine wanafanya.Usifanye kwa kuiga au kufuata mkumbo.
 
Ikiwa wewe unafanya kazi katika hoteli na una kiu kubwa ya kuwa mjasiliamali,ni  vyema kufikria  katika  tasnia hiyo ya hoteli ni kitu gani unaweza kufanya wewe mwenyewe binafsi vizuri zaidi.
 
Mfano; Ikiwa katika tasnia hiyo ya hoteli unafanya kazi kama mpishi  kwa nini usifikirie kuanzisha kitu chako  ambacho una uzoefu nacho zaidi na kuona ni kwa jinsi gan badae unaweza kujitegemea.
 
Ikiwa wewe ni mjasiliamali basi ya kupasa wewe kujenga hali ya kile unachokipenda.
 
Baadhi ya wajasiliamali wamekata tamaa kwa kuona hawapati matokeo mazuri kwa yale wanayofanya labda wanataka wapate matokeo ya haraka,kumbuka ndugu mjasiliamali si suala l kulala na kuamka bali ni suala linalochukua mda na huitaji uvumilivu.Jifunze kwa wajasiliamali utagundua mafanikio yao yalichukua mda mrefu.
 
SOMA ZAIDI: AINA TATU ZA UJUZI UNAOHITAJI ILI KUONGEZA THAMANI YAKO NA KULA MEMA YA NCHI
 
2.Jenga upekee wa kile unachofanya.
 
Jaribu kuwa mbunifu kwa kile ulichoamua kufanya. Tafuta namna ya kujitofautisha na washindani wako ufahamike kwa namna yako.
 
Wajasiliamali wengi wanafanya mambo kwa kuona 
tu wengine wanafanya. wengi wameingia kwenye biashara kwa kuiga wengine wanachofanya.
 
Yafaa mjasiliamali kuwa mbunifu kwa kuacha kuiga kile unachokiona kwa mwenzako.
 
Ni vizuri kwa mjasiljamali kuwa na upekee wa bidhaa au huduma kwani ni njia nzuri ya kudhibiti soko.
 
Elewa biashara katika zana hizi zina ushindani mkubwa na changamoto nyingi
 
SOMA ZAIDI: HII NI HAZINA ILIYOLALA KWENYE KITABU HIKI KIMOJA
 
3.Jiulize unafanya nini ili kuwashika wateja wako.
 
Wateja ni msingi wa kuendelea na biashara kwa sababu bila wateja wa kuwauzia bidhaa hakuna biashara itakayoendelea.wateja ndo wanafanya shughuli unazozijua ziendelee.
 
Jijengee utamaduni kama mjasiliamali wa kuwashika wateja wako.
Hili unaweza kulifanya kwa kujenga uhusiano  mzuri na wateja wako,hakikisha wateja wanapata kile wanachokitaka kutoka kwako,kwa kuwa sehemu nzuri ya wateja na kuepuka lugha ya maudhi.
 
Jiulize katika biashara umewahi kufaya nini kuwatathimini wateja.
 

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

 
Tuishie hapo kwa leo 
Ni mimi rafiki na ndugu yako 
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane 
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Endelea kufuatilia blogu hii kwa makala zaidi za kuelimisha na kuhamasisha
 
 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X