Mambo Saba (07) Ya Kufanya Pale Unapokuwa Hauna Cha Kufanya


Huwa inatokea kwa watu wengi mara nyingi, ambapo wanajikuta kwamba hawana kitu cha kufanya. Kitu hiki huwa kinawafanya watu wengi kuanza kuzunguka huku na kule wakisema kwamba wanapoteza muda. Sasa siku ya leo napenda nikwambie vitu vitano ambavyo utapaswa kufaya pale ambapo utakuwa unaona kwamba hauna kitu cha kufanya.
KWANZA, SOMA KITABU
Ukijikkuta katika mazingira ambayo unaona kwamba hauna kitu cha kufanya, basi chukua kitabu na anza kusoma. Akili yako yote iweke kwenye kitabu hicho ambacho umeamua kusoma. Tena hakikisha kwamba una daftari na karatasi ambapo utapata kuandika vitu vya kipekee sana kutoka kwenye kitabu hicho.
Kwa kufanya hivi utakuwa umeutumia muda wako vizuri badala ya kusema kwamba, uzunguke huku na kule UKIPOTEZA MUDA
PILI, PITIA MALENGO YAKO
Mara nyingi ukiona kwamba mtu anasema kwamba anapoteza muda, basi ujue kwamba hiyo ni ishara tosha ya kwamba hajapangilia vizuri malengo yake. Hivyo ukijiona kwamba upo kwenye hali kama hii ambayo huelewi ni kitu gani ambacho unapaswa kufanya basi chukua malengo yako na uyapitie. Kitu hiki hapa kitakusaidia kujua ni kitu gani haswa unapaswa kufanya. Kitu hiki pia kitakusaidia kuweka nguvu yako kubwa kwenye kutimiza malengo yako ambayo yako mkononi mwako.
ANGALIA SOMO HILI YOUTUBE:  Jinsi Ya Kutengeneza Fedha Mtandaoni
TATU, ITUMIE NAFASI HII KUONGEZA WATEJA WAWILI KWENYE BIASHARA YAKO
Ukiona kwamba hauna kitu cha kufanya basi utumie muda huu kwa ajili ya kutafuta wateja wawili wa biashara yako au huduma yako ambayo unatoa. Hivyo unaweza kutumia muda  huu kuwapigia watu ambao wanaweza kununua bidhaa zako au unaweza kwenda ofisi/ nyumba zao ili uongee nao kuhusu biashara yako au huduma yako. Kwa kufanya hivi utakuwa umeutumia vizuri muda wako kwa kuhakikisha kwamba umeongeza wateja na mauzo kwenye bidhaa yako.
Kama hauna biashara basi unaweza kuutumia muda huu kuangalia ni biashara gani unaweza kuanza kufanya mara moja.
NNE, UTUMIE MUDA HUU KUMSHUKKURU  MTU MMOJA
Kila siku kwako inakuwa ni nafasi yako wewe hapo kukutana na watu wengine. Sasa unapokutana na watu, kuna wale watu ambao mnabadilishana namba, kuna wale ambao wanakusaidia kufanya na kutimiza kazi fulani, kuna wale ambao wanashiriki kuinua kipaji au ndoto yako. Hivyo utumie muda huu katika kuandika ujumbe mfupi wa kumshukuru mtu wa aina hii. Au kupiga simu na pengine kuandika barua kwa ajili ya mtu huyu. Mshukuru kwa kitu cha kipekee ambacho amekufanyia.
Haya ni matumizi mazuri ya muda wako  ambao unao siku ya leo.
TANO, SIKILIZA VITABU VILIVYOSOMWA
Kama wewe unapenda kuzunguka na hupendi kukaa eneo moja, basi cha kufanya hakikisha kwamba unakuwa na vitabu vilivyosomwa. Unaweza kusikiliza vitabu hivi hapa ukiwa unatembea. Unaweza kusikiliza vitabu hivi hapa ukiwa umekaa chini. Lakini pia unaweza kusikiliza vitabu hivi hapa ukiwa unaendelea na shughuli nyingine kama hii hapa tunayoenda kuona kwenye namba sita chini.
SITA, TENGENEZA CHAKULA AMBACHO UMEKUWA UNAPENDA KWA SIKU SASA
Inawezekana kuna aina ya chakula umekuwa unapenda kula kwa siku sasa, ila kutokana na kwamba hukuwa na muda wa kukitengeneza basi ulikwama kwenye kufanya hiki kitu. Hivyo, kwa muda huu ambao unaona kwamba hauna kitu cha kufanya unaweza kuutumia kutengeneza chakula cha kipekee ambacho kwa siku umekuwa unapenda kula.
Au kinywaji cha kipekee ambacho umekuwa unapenda kunywa kwa siku sasa hivi.
Haya yatakuwa ni matumizi mazuri ya muda wako katika kujenga afya yako.
SABA, ONGEA NA WATOTO WAKO KUHUSU MAMBO MBALIMBALI YA KISHULE NA MAISHA
Unaweza ukawa ni mtu ambaye umekuwa unabanwa sana na kazi za hapa na pale, kiasi kwamba watoto wako hawapati nafasi ya kuwa karibu na wewe. Na pengine hata mwenza wako hapati muda mzuri wa kuwa karibu na wewe. Unaweza kuutumia muda huu kukaa na familia na kuongea mambo mbalimbali.
Unaweza kuutumia muda huu kufuatilia maendeleo ya watoto wako shuleni. Lakini pia unaweza kuutumia muda huu kuwasaidia watoto wako kufanya kazi za shuleni.
Rafiki yangu haya ndio mambo saba ya kufanya pale unapojiona kwamba hauna kitu cha kufanya. Nina hakika sana kwamba mambo haya yatakusaidia sana pale utakapojikukta kwenye hali hii hapa.
Kitu hiki kitakufanya usiwe mtu wa kusema kwamba ninapoteza muda tu hapa. badala yake utakuwa na kila kitu ambacho kimepangiliwa  vizuri sana.
Nashukuru sana nikutakie kila la kheri
Ni mimi anayejali mafanikio yako
GODIUS RWEYONGEZA

KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA

, ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X