Tabia Saba (07) Zinazoleta Umasikini Na Jinsi Ya Kuziepuka Ili Kutengeneza Utajiri


Rafiki yangu, hongera sana kwa siku hii nyingine ya kipekee sana. Leo ikiwa ni februari 29 2020. siku zinazidi kusogea kwelikweli. Mwezi wa pili wa mwaka uliokuwa mpya, sasa unaelekea ukingoni. Siku chache zijazo tu utashangaa mwezi wa tatu huo umefika.
Nina hakika moja ya lengo lako kubwa maishani ni kutokomeza umasikini na kujenga utajiri utakokunufaisha wewe, familia yako, watoto mpaka wajukuu. Yaani tuseme kuondoa laana ambayo imekuwepo sasa kwenye familia yenu (umasikini).
Kuna tabia ambazo zitakuzuia kutengeneza utajiri ambao  umepanga. Na tabia hizi leo ndizo nataka uvunje moja kwa moja. Kama utaendelea na tabia hizi basi utaagana na utajiri maisha yako yote.
TABIA YA KWANZA NI TABIA YA KULALAMIKA
Hii ni tabia ambayo umekuwa nayo kwa siku sasa. Unalalamika juu ya hali ya hewa. unalalamika juu ya maisha ya watu wengine.
Unalalamika juu ya matatixo ambayo unakutana nayo kila siku kwenye maisha.
Hii hapa sio tabia ya matajiri hata kidogo. Matajiti wanajua kwamba kwenye maisha kuna vitu vya aina mbili.
kwanza ni vile ambavyo wanaweza kuvibadili, pili ni vile ambavyo vipo nje ya uwezo wao na hivyo hawawezi kuvibadili kabisa.
kwa hiyo matajiri wanachofanya ni kubadili vile wanavyoweza na kuachana na vile ambavyo hawawezi kubadili kabisa kwenye maisha yao.
Hivyo ambavyo wao hawawezi kubadili wanawaachia watu wengine ili nao wafanye kazi yao.
Na wewe ukiona kwamba kuna kuna kitu huwezi kubadili basi achana nacho, waachie wengine wanaoweza kubadili hicho kitu. Mwisho wa siku kama kila mtu atatimiza wajibu wake. Basi dunia itakuwa sehemu nzuri sana.
Kwa hiyo kitu cha kufanya siku ya leo. gawa vile vitu ambavyo umekuwa unalalamilia kwa siku sasa kwenye vipengele viwili. kipengele cha kwanza ni kile ambacho unaweza kubadili.
Na kipengele cha pili ni vile ambavyo huwezi kabisa kubadili.
Kwa vile vitu ambavyo huwezi kubadili, basi waachie wengine. Wewe kazana na vile tu ambavyo unaweza kubadili tu.
SOMA ZAIDI; MKitu Kimoja Kitakachotokea Endapo Utakuwa Mlalamikaji
TABIA YA PILI, NI KUWA NA MATUMIZI MAKUNWA ZAIDI YA KIPATO CHAKO
Hili ni kosa ambalo sidhani anahitajika nabii kukwambia ukweli huu. Ni wazi kwamba kama unatumia kiasi kikubwa zaidi ya kipato chako basi umasikini unakunyemelea kwa kasi kubwa.
kwa hiyo basi, napenda ufahamu kwamba kuanzia leo hii, kiasi cha fedha ambacho unatumia, hakikisha kinakuwa ni kidogo kuliko pesa unayoingiza.
 kama unaona kiasi cha fedha unachoingiza  ni kidogo basi fanya utaratibu kuanzia leo wa kuongeza kipato chako. Anzisha hata biashara ambayo inaweza kuanza kukuongezea kipato cha ziada.
Kamwe, kamwe,usitumie fedha zaidi ya kiasi unachoingiza.
TABIA YA TATU,USINUNUE VITU AMBAVYO HAVIONGIZI FEDHA
Kanuni muhimu ya fedha ni kwamba, unapaswa kuwa na rasilimali nyingi zinayoingiza fedha kuliko dhima (liabilitiy). rasilimali zinaingiza fedha zaidi na dhima zinatoa pesa mfukoni. kama una tabia ya kununua dhima zaidi ujue kwamba umasikini utakuwa unakunyemelea zaidi. wakati kama una tabia ya kununua rasilimali basi ujue kwamba utajiri utakuwa unakunyemelea pia. rafiki yangu nipende kukushauri kuwa unapaswa kujenga tabia ya kuwa na tabia ya kununua rasilimali zaidi ya unavyonunua dhima.
TABIA YA NNE NI KUNUNUA VITU BILA MPANGILIO
Hivi ushawahi kuona mtu akiwa na pesa ndio anawashwa kufanya matumizi kiasi kwamba anakuta kwamba pesa yote amenunua vitu ambavyo sio vya msingi. Ndio unakuta kwamba mtu ananunua  beseni, sinia au vitu vingie ambavyo vinaoenekana mbele ya macho yake bila mpangilio.
Kama wewe una tabia hii hapa basi niseme kwamba hii ni dalili ya umasikini. Yaani umasikini unakunyemelea kwa kasi. Jenga tabia moja muhimu sana ya kitajiri, tabia hii ni ya kukaa na pesa na kuituliza kwanza kila unapoishika mkononi mwako. Kwa  hiyo unapopata pesa usipoteze akili yako. Yaani ukawa kama umelogwa, ukawa hushikiki nyumbani, ukaanza kutumia kwa kisingizio kwamba unatumia kidogo tu.
Hapa ninaenda kukupa mbinu mbili ambazo zitakusaidia wewe hapo usiwe unatumia fedha zako hovyo hovyo.
Jenga utaratibu wa kuwa unaandika  vitu ambavyo unaenda kununua kila unapoamua kwenda kufanya manunuzi. Usiende kununua kwa sababu una fedha, utajikukuta kwamba umenunua na vitu vingine ambavyo sio. Utanunua vitu vingine kwa sababu tu umevipenda kwenye macho yako tu. ila baadae utakuja kugundua kwamba ulikuwa huvihitaji.
Pili, jenga utaratibu wa kufanya matumizi makubwa kwa wakati mmoja. Yaani yale matumizi ya muhimu unaweza kuyanunua kwa pamoja na kwa wingi. Kitu hiki hapa kitakusaidia wewe kutofanya matumizi ya hovyohovyo, lakini pia kitakufanya uwe unanunua vitu kwa bei ya kawaida sana.

TABIA YA TANO NI KILA MMOJA KUJUA KWAMBA UNA PESA
Hii ni tabia moja mbaya ambayo ukiendelea nayo basi itakukwamisha kwelikweli.  Hakuna mtu anapaswa kujua ni lini umeingiza kiasi kikubwa cha pesa au  lini haukuwa na pesa kabisa. usiwe unabadilika kulingana na pale unapopata pesa au unapokosa pesa. Tabia zako zinapaswa kuwa ni zilezile muda wote.
Moja ya hasara kubwa ya wewe kujionesha kwa watu kwamba una pesa ni kwamba utakauwa unapata marafiki “feki”ambao wananuia kutumia pesa zako tu. lakini pesa zako zinapoisha na wao wanapotea.
Na mchezo huu unaweza ukawa unaendelea miaka nenda, miaka rudi bila ya wewe kujua. Unaweza kufikia hatua ya kujiuliza, kwanini huwa ninapata marafiki ambao huwa wanakuja na kupotea? Jibu ni kwamba wanaona pesa wanakuja. Ukifulia tu, na wao wanaenda sehemu nyingine.
Kuanzia leo hii, mtu yeyote asijue kwamba una pesa au hauna pesa. ishi maisha yaleyale bila kujali kwamba kwa sasa upo kwenye hali gani.
TABIA YA SITA,  KUGAWA PESA BILA MPANGILIO
Najua utakuwa na marafki, ndugu, na watu wengine ambao huwa wanakuomba pesa ya kula au pesa ya kutatua tatizo fulani ambalo limewakumba. Watu hawa wanajenga utaratibu kwamba upo muda wote. Hivyo wakipatwa na tatizo, muda wowote tu wanakimbilia kwako kuomba pesa. hata kama tatizo ni dogo na wao wanaweza kulitatua lakini bado wanakimbilia kwako ili uwasaidie pesa. kuanzia leo anza kujenga utaratibu wa tofauti. Watu wanapokuomba pesa wape ushauri wa namna wanavyoweza kutatua matatizo yao wenyewe.  Kiufupi ni kwamba usijenge utaratibu wa kuwapa watu samaki. Wakati unaweza kuwafundisha kumiliki bwawa la samaki. Hivyo wafundishe namna ya kumiliki bwawa la samaki badala ya kuwa unawapa samaki kila siku.
Wafundishe kutatua matatizo yao ya kipesa wenyewe.
TABIA YA SABA, KUKOPA NA KUKOPESHA
Kama una tabia ya kukopa, basi leo iwe mwisho. Usikope teana. Kukopa ni tabia ya kimasikini ambayo watu masikini wanayo na wanaibeba kwenye maisha yao ya kila siku. Madeni sio kitu kizuri ambacho unawezakujizoeza. Badala ya kuiweka akili yako kwenye kuomba mikopo basi
Pia usikopeshe fedha yako. Nadhani umewahi kusikia watu wanasema kwamba kukopa harusi kulipa matanga. Huu usemi sio kwamba ni wa kubahatisha. Ni wa ukweli. na asilimia kubwa ya watu ambao utawakopesha hawatajitokeza kulipa kwa muda walipanga. Na hata wakilipa watakulipa kwa kuchelewa nap engine baada ya mikwaruzano mingi sana. Sasa kwa nini ujiingize kwenye shida zote hizo.
Kuna watu wanafanya  biashara ya kukopesha. Kama wewe hufanyi hii biashara basi usikopeshe.
Rafiki yangu, nimeona kwamba nikwambiae vitu hivi vya kipekee sana leo ili uweze kuvijua. 

Ni mimi anayejali mafanikio yako,
GODIUS RWEYONGEZA

KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA

, ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X