Vitabu Nane (08) Nilivyosoma Mwezi Wa Saba


tatizo si rasilimali zilizopotea
Hiki ni kitabu cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA


Kuanzia mwezi huu nimeanzisha utaratibu mpya ambao utakuwa unaniwezesha mimi kukushirikisha vitabu ambavyo nimesoma ndani ya mwezi uliotangulia. Kutoka kwenye orodha hiyo, nitakuwa nakuelekeza kitabu kimoja utapaswa kusoma

Hivyo leo hii ninaenda kukushirikisha vitabu NANE ambavyo nilisoma mwezi uliopita. Kila kitabu nitapata nafasi ya kukiongelea kidogo, na mwisho nitakushauri kitabu kimoja ambacho utapaswa kukisoma mara moja. karibu sana

1. A HAPPY POCKET FULL OF MONEY.


Hiki ni kitabu ambacho nilitoka nacho mwezi sita. yaani, nilianza kukisoma mwezi wa sita katikati nikaja kukimaliza tarehe moja mwezi wa saba.

Kitabu hiki hapa ni kizuri sana. kimeongelea kiundani sayansi ya fedha, na jinsi fedha inavyopatikana kwa kufuata sheria za asili. Ukiufuata kanuni zilizo kwenye kitabu hiki hapa, ni wazi kuwa unaenda kuachana na umasikini na badala yake unaenda kujenga urafiki wako mkubwa na UTAJIRI. Kurasa za kitabu hiki hapa zimesheheni mambo mbalimbali ambayo kwa sasa hivi unayachukulia poa, ila yana nguvu kubwa sana kwenye kutengeneza utajiri.

Kitu kikubwa kutoka kwenye kitabu hiki ni kuwa fikra zako ni chanzo cha utajiri wako au umasikini wako. Ukibadili fikra zako, basi utapata pia kubadili  maisha yako. Naam, utaweza kutengeneza utajiri.

Nashauri kila mtu ambaye yu hai akisome kitabu hiki hapa. unaweza ukawa unajuliza kwa nini wewe unashindwa kutengeneza fedha. Basi soma kitabu hiki hapa na utashangaa.

 

2. THE POWER OF SUBCONSIOUS MIND

Hiki ni kitabu kingine cha kipekee ambacho nilipata nafasi ya kukisoma kwa mwezi wa saba. Ni kitabu kizuri sana kuhusiana na NGUVU au UWEZO ulio nao wewe hapo wa kufanya mambo makubwa. Una uwezo wa kutenda miujiza, una uwezo wa kuvuta watu sahihi kwako kwa kutumia uwezo wa SUBCONSIOUS

MIND. Unaweza kuvuta fedha maishani mwako kwa kutumia SUBCONSIOUS

MIND. Unaweza kutibu magonjnwa yako, hata yale ambayo madkatari wamekwambia hayatibiki kwa kutumia SUBCONSIOUS MIND.

Lakini pia ukitumia vibaya uwezo huu, unaweza kujiiingiza kwenye umasikini, magonjwa, ajali na hata kusababisha kifo chako.

Hivyo, nashauri usome kitabu hiki hapa, maana, ukiweza kufahamu uwezo mkubwa ulio nao ndani yako. Ukifahamu pia kuwa wewe ndiye nahodha mkuu wa maisha na unaweza kuamua jambo likawa, basi ni wazi kuwa kwa kutumia hiyo nguvu unaweza kufanya mambo makubwa ambayo wengine hawajawahi kuona hapa duniani.

 

Kiufupi hiki ndio kitabu ambacho binafsi nakushauri ukisome kwa mwezi huu.

BONYEZA HAPA ILI KUKIPATA

 

3. MAKE YOUR DREAMS BIGGER THAN YOUR MEMORY CHA Terri Savellefoy

Nilisoma kitabu hiki hapa kama sehemu ya utafiti kwenye uandishi wa kitabu changu changu kinachohusiana nan NDOTO. Hivyo, katika kutafuta vitabu ambavyo ninaweza kupata mambo mazuri kuhusiana na ndoto nilikutana na kitabu hiki hapa. kitabu hiki hapa ni kizuri sana, kusoma hasa kwa wewe ambaye umemezwa na mambo ya nyuma kuliko ambavyo ndoto zako zimekumeza. Kama unafikiria zaidi mambo yaliyotokea kama, ugonjwa ambao umewahi kukukuta siku za nyuma, au ajali, au kuachwa au kitu chochote kile cha nyuma. Kama kitu hiki hakikupi amani na hivyo muda wote unakirejea na kuona una hatia. Au kuona kuwa kitu hicho cha nyuma kimekunyima fursa ya wewe kusonga mbele. Basi mwandishi wa kitabu hiki hapa anaingilia katikati na kusema kwamba unapaswa kutengeneza ndoto zako kuwa kubwa zaidi kuliko kumbukumbu zako za mambo ya zamani.

Ukiwa na ndoto kubwa, utajikita kwenye hizo na utashau mambo yote ya kizamani ambayo yatakuwa hayakupia nguvu.

Kuna njia nyingi mwandishi ameshirikisha kwenye hicho kitabu, kuanzia namna ya kuondokana na msongo unaotokana na kumbukumbu za nyuma mpaka jinsi ya kufikia ndoto zako.

Kitabu hiki kimeandikwa kwa misingi ya dini ya kikristo, hata hivyo, bila kujali upo kwenye dini gani, basi kisome kitabu hiki hapa utapata kujifunza mengi kwelikweli kuhusu ndoto. Binafsi sijakimaliza, nimebakiza vitu viachache kwenye kitabu hiki hapa vya kumalizia.

 

4. EINSTEIN: His Life and universe cha Walter Isaacson.

Binafsi napenda sana kusoma vitabu vya biografia. Na karibia kila mwezi tutakuwa tunapata kitabu kimoja cha aina hii. Wakati naendela n utafiti kwenye uandishi wa kitabu changu hicho kinachohusiana na NDOTO. Niliamua pia kuchukua kitabu hiki hapa kinachohusina na ALBERT EINSTEIN.

Kwanza nilipata kujua juu ya uwepo wa kitabu hiki hapa wakati nasoma biografia ya STEVE JOBS, ambayo imeandikwa na mwandishi huyuhuyu wa kitabu hiki. Na baadae mwezi juni kwenye kitabu cha MASTERY ndio niliona kilikuwa miongoni mwa vitabu vilivyosomwa na Robert Greene. Hivyo, wakati naendelea kusoma kitabu cha MASTERY niliandika pembeni kitabu hiki ili nije nikisome siku za mbeleni.

Albert Einstein ni mmoja wa wanasayansi wakubwa wa karne ya 20. Kuna vitu vingi amefanya kwenye uwanja wa fizikia ambavyo mpaka leo hii vinatumika kwenye masomo haya ya fizikia. Nadharia yake ya GENERAL RELATIVITY ni moja nadharia muhimu sana kwenye uwanja wa fizikia. Lakini pia mliganyo wake E=MC2 ni mlinganyo maarufu sana hapa duniani. Pengine unaweza kuwa ni mlinganyo ambao unafahamika kwa wasomi mpaka wasio wasomi hata kwa kuutaja tu.

Kuna mengi ya kujifunza ndani ya kitabu hiki hapa. kama ilivyo kawaida, mwandishi Wlater Isaaacson atakuvuta taratibu kwenye maandishi yake mpaka utajikuta kwamba umezama ndani ya kusoma huku ukiwa hutaki kukiachia kitabu hiki hapa.


SOMA ZAIDI: Mafunzo saba  (07) kutoka kwa wajasiliamali saba waliofanikiwa zaidi kwenye karne ya 19


 

5. UNDERSTANDING YOUR POTENTIAL cha Myles Munroe.

Hiki ni kitabu kingine muhimu sna ambacho kinazunguzmia juu ya uwezo ulio nao ndani yako. Wazo kubwa la kitabu hiki ni kuwa wewe una uwezo wa kufanya makubwa, ila usipoutumia uwezo huo utaendelea kukaa humo ndani yako, huku ukiunyima uliwengu huu uhondo ambao ungetokana na malengo na ndoto zako.

Na uwezo wako haupimwi kwa kile ambacho unaweza kufanya, bali kwa kile ambacho hujafanya.

 

6. PRINCIPLES AND POWER OF VISION

Hiki nikitabu kingine kizuri kuhusu nguvu ya maono ambacho nilisoma kutoka kwa Dr. Myles Munroe.

Kuna kanuni ambazo ukizifuata inakuwa ni rahisi kwako kufikia ndoto zako, ila ukizivunja kanuni hizi hapa, basi unakuwa unajikwamisha kufikia malenngo na ndoto zako.

Kitafute kitabu hiki hapa na ukisome.

 

7. THE PROPHET cha Khalil Gibran

Hiki ni kitabu kifupi sana ila kizuri sana. kinaeleza mtu ambaye alikuwa anakaa kwenye nchi ya ugeni, sasa ulipofika wakati wake wa kuondoka watu wakawa wanamwomba aseme kitu kuhusu baadhi ya vitu. Ndipo walimwomba aseme kuhusu MAHUSIANO, NDOA, NYUMBA, WATOTO n.k.

Kuna mengi ya kujifunza kwenye kurasa za hiki kitabu

 

 

8. LIFE 3.0: How to Be Human In The Age Of Artificial Intelligence

Hivi ukisikia kuhusu Aritificial Intelligence (A.I) unaelewa nini? Ni nini maoni yako kuhusiana na hii mada ambayo imekuwa inajadiliwa na watu mbalimbali kwenye zma hizi?

Kadiri ugunduzi unavyoendelea kwenye hii dunia, binadamu wanaelekea kuwa kama miungu. Yaani, wanafikia hatua ambapo wanaweza kutengeneza vitu vyenye uwezo wa kufikiria kuzidi wao.

Wapo watu ambao wana hofu kuwa binadamu anaweza kufikia hatua akatengeneza kitu chenye akili kuliko yeye. Na pengine kitu hiki kikatumika kuwaua binadamu wote.

Ila wengine wanaona kwamba hiyo shida, binadamu akitengeneza kitu chenye akili kuliko yeye litakuwa ni jambo la busara sana, maana kitakuwa kinafanya kazi ya kufikiri kwa kina na kuja na suluhisho la vitu ambavyo hapo awali hatukuwahi kufikiria.

Wapo watafiti wanaosema kwamba binadamu anaweza kutengeneza A.I kufikia mwaka 2055.  Huku wengine wakisema kitu kama hiki hakitawezekana ndani ya miaka 100 ijayo.

Kitabu hiki kimejibu maswali mengi ambayo watu wanayo kuhusiana na hiki kitu. Kimeenda mbali zaidi na kueleza kuhusiana na safari ya binadamu kuishi miaka elfu kumi ijayo mpaka bilioni ijayo na jinsi binadamu anaweza kutawala ulimwengu kwa kusafiri kutoka sayari moja kwenda nyingine endapo kutakuwepo na na A.I.

Lakini pia kimetahadharisha, mambo mabaya ambayo yanaweza kujitokeza endapo hatutakuwa makini kwenye utengezaji wa A.I.

 

Rafiki yangu hivyo ndivy ovitabu ambavyo nilisoma kwa mwezi wa saba.

Kitabu cha THE POWER OF SUBCONSIOUS MIND ndicho ambachoningependa, wewe ukisome kiundani zaidi. Kina mambo mengi mazuri kwa ajili yako,

 

 

 

, ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X