Njia Tano Za Kutengeneza Utajiri Na Moja Kuu Inayokufaa


Utajiri ni asili ya mwanadamu yeyote. Ni kitu muhimu kwake kuwa nacho. Kamusi ya kiswahili sanifu inasema kuwa utajiri ni hali ya kuwa na Mali nyingi. Hata hivyo, leo hapa tunaenda kuona kuwa utajiri ni zaidi ya kuwa na mali nyingi. Maana kuna utajiri wa aina tatu.

Kwanza, kuna utajiri mali na vitu vingine vizuri ambavyo dunia inaweza kutoa (ambavyo vinapatikana duniani). Kiufupi huu ni utajiri muhimu sana unaopaswa kuwa nao. Mali, fedha, magari, nyumba nzuri kutaja ila vichache. Unastahili kuwa na vitu vya aina hii na ni haki yako ya kuzaliwa kabisa.

Aina ya pili ya utajiri ni utajiri wa afya. Afya yako ni muhimu,ukizingatia kuwa aina nyinginezo za utajiri zinategemea kama wewe una afya ya mwili.

Kwa hiyo jitahidi sana kuilinda sana hii afya yako, maana ndiyo inakuoelekea wewekupata utajiri mwingine.

Utajiri wa kiroho. Huu pia utajiri muhimu kuwa nao na ambao unafanya mlinganyo wa utajiri ukamilike. 

 

 

Sasa hapa chini ninaenda kukueleza njia tano za kupata utajiri. Na utajiri ninaoongelea hapa ni utajiri wa fedha.

Mwisho kati ya hizi njia tano, nitakuelekeza njia moja kubwa unayoweza kutumia kupata utajiri wako na hii ni njia isiyoshindwa mara zote.

1. UNAWEZA KUPATA UTAJIRI KWA KURITHI

Huu Ni utajiri unaopata baada ya watu wengine kuwa wamefanya kazi na wewe unapokea mali tu.

Japo najua unaweza kuupenda utajiri huu ila tafiti nyingi zimeonesha kuwa watu ambao hupokea utajiri kwa njia hii huupoteza ndani ya miezi au miaka michache na kurudia kuwa masikini. Hivyo, utajiri wa kurithi hauna historia ya kutengeneza matajiri wa kudumu kwa wingi. Ni wachache sana walioweza kuutunza utajiri huu na wale walioweza kuutunza utajiri huu ni wale ambao walikuwa wamepewa elimu ya fedha kabla ya kurithi mali hizo. Ila wale ambao hawakupata elimu hii ya fedha waliishia kupoteza mali zote.

2. UTAJIRI KWA KUBAHATISHA

Huu ni utajiri ambao unaweza kuupata kwa kucheza michezo ya bahati nasibu. Kwanza, hii si njia nzuri ya kuufikia utajiri. Lakini pia tafiti kwa upande huu zinaonesha pia watu ambao huwa wanapata utajiri wa aina hi,i nao huishia kuupoteza. Na sio tu kwamba wanapoteza huo utajiri pekee, bali pia wanaishia kuwa masikini zaidi ya walivyokuwa hata pale mwanzoni. Yaani, wanaingia mpaka kwenye madeni na hata wanajikuta kwamba wanauza mali walizokuwa nazo hapo awali.

Hivyo, hii sio njia ya kutengeneza utajiri ambayo naweza kukushauri wewe hapo uitumie. Na ukiachana na hilo ni  ukweli kwamba kubahatisha kutakufanya upoteze fedha zako nyingi ambazo ungeweza kuziwekeza na zikakusaidia kwenye maeneo mengine.

3. UTAJIRI KWA KUUZA THAMANI YAKO

Huu ni utajiri ambao unapata kwa kuuza utu wako kwa ajili ya fedha. Sidhani kama hapa unahitajika muujiza wa kukwambia kwamba aina hii ya utajiri si mzuri. Hivyo, kiufup ni kwamba aina hii ya utajiri haikufai hata kidogo. Unachotakiwa kufanya ni kuweka misingi muhimu ambayo utaisimamia maishani mwako. Na kwenye misingi hii hakikisha kwamba wewe hapo hauuzi utu wako kwa sababu ya fedha.

4. UTAJIRI KWA KUIBA/KUTAPELI/UFISADI

Aina hii ya utajiri inaenda kabisa kinyume na sheria za nchi na dunia nzima kiujumla. Kibaya zaidi ni kwamba hata ukupata utajiri huu, muda wote utakuwa unahofu na kuona kama vile watu wamejua siri yako ya kuupata utajiri. Hata mtu akikohoa tu wewe kwa upande wako ndio unaenda kuona kwamba tayari huyu mtu amenichora! Hii si aina ya utajiri ambayo unapaswa kuifikiria hata kidogo.

5. UTAJIRI KWA KUTOA THAMANI 

Hii ndiyo aina ya utajiri ambayo mabilionea, mamilionea wengi wameitumia. Na hii ndiyo njia ambayo naweza kukushauri ufuate, maana kwa njia hii unatengeneza utajiri wa kudumu na hata ikitokea kwamba umeupoteza utajiri huu hapa bado unakuwa na nafasi kubwa ya kuweza kuurudisha utajiri huu kwako.

Kwa njia hii ya utajiri unatoa thamani kwa watu wengine na kutatua matatizo au vikwazo na changamoto walizonazo. Hii ni aina ya utajiri unayoipata kwa kufanya maisha ya watu wengine kuwa bora zaidi. Na kadiri wewe unavyokuwa unafanya maisha ya watu wengine kuwa bora zaidi basi ya kwako yanazidi kuwa bora zaidi.

Kitu muhimu unachoweza kufanya siku hii ya leo ni kuamua kuwa tajiri. Na njia ya kuwa tajiri unayopaswa kuchagua ni kuwa tajiri kwa kutoa thamani kwa watu wengine.

Nikushukuru sana kwa wakati wako rafiki yangu. 

 

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

, ,

One response to “Njia Tano Za Kutengeneza Utajiri Na Moja Kuu Inayokufaa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X