Vitu Vitano Ambavyo Bosi/ Mwajiri Wako Hawezi Kukwambia


siku ya leo nimeona nikueleze vitu vitano ambavyo bosi wako hawezi kukwambia. na vitu hivi hakuna mtu mwingine atakuja kukwambia isipokuwa mimi tu ndio nimeona inafaa nikwambie vitu hivi. sasa ni juu yako kuvifanyia kazi ili utengeneze maisha ya tofauti au la uendelee kama ulivyokuwa unafanya siku zote.

1.Bosi wako hawezi kukwambia fedha iliyoanzisha biashara ya kampuni unayofanyia kazi ni sawa na fedha uliyotumia kununua gari lako. Pengine fedha hiyo ilikuwa kidogo kiasi cha kulingana na fedha ya smartphone yako. Alichofanya alitumia huo mtaji kidogo na kuukuza mpaka ikawa biashara kubwa unayofanyia kazi sasa.halafu eti wewe unajikuta huwezi kubanduka kwenye hiyo kazi kwa sababu huna mtaji. Rafiki hiki kitu bosi wako hawezi kukwambia isipkuwa mimi tu.

  

2.Bosi wako hawezi kukwambia anzisha biashara ukiwa ukiwa hapa umeajiriwa

Bosi wako hatakwambia kuwa kwa siku una saa 24. Hivyo, Jenga utaratibu wa kuamka asubuhi na mapema na kufanyia kazi biashara yako na baadaye ukitoka kazini wahi usimamie biashara yako. Bosi wako hatakwambia punguza kuangalia runinga na kuchati unapotoka kazini ili ukasimamie biashara yako.

Bosi wako hatakwambia usiingie kwenye mitandao ya kijamii ili ushughulike na biashara yako Ni mimi tu mwenye ujasiri wa kukwambia hivyo.

3. Bosi wako hatakwambia acha kazi ukajiajiri labda tu kama utendakazi wako hauridhishi.

4. Bosi wako hatakwambia kuwa kipaji chako ni hazina kubwa ambayo hupaswi kuizika.

5. Bosi wako hatakwambia kuwa ukiendelea kunmaamikia,usitegemee kufanikiwa.

Unaweza kuwa mtu wa kulalamika kwa mambo mengi ambayo hupati kutoka kwa bosi wako. Unaweza kuendelea kulalamika kuhusu mshahara wako ambao hautoshi, Ila kiufupi ukiendelea kumlalamikia bosi wako usitegemee kufanikiwa.



Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

, , ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X