KITABU: MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE


 

Hivi umewahi kuona wazungu wanavyokuja hapa nchini na kuzunguka huku na kule. Na hata kutembelea vivutio ambavyo vipo karibu yako wakati wewe ukiwa hujawahi kuvitembelea. Huwa wanawezaje kukaa hapa nchini kwa mwezi au zaidi? Je, huwa hawana kazi huko kwao?

Moja ya kitu ambacho huwa wanahakikisha wanakuwanacho ni fedha inayowafanyia kazi. Ubora siyo tu kwamba wao peke yao ndio wenye uwezo wa kuifanya fedha iwafanyie kazi, bali na wewe unaweza pia. Na njia nzuri kabisa ambayo wewe unaweza kuanza kuitumia ili kuifanya fedha ikufanyie kazi ni kwa kuwekeza kwenye hisa.

Kwenye kitabu hiki hapa tunaenda kujifunza kila kitu ambacho unahitaji kujua kuhusu hisa na jinsi ambavyo unaweza kutengeneza uhuru wa kifedha au utajiri kupitia hisa, hatifungani na vipande.

Kitabu hiki kimeeleza vitu vigumu ambavyo watu wengi wanashindwa kung’amua kwa lugha rahisi ambayo kila mtu anaweza kuilewa. Na lengo lake kubwa ni kukukuwezesha wewe uweze kukisoma, kukielewa na kuchukua hatua kwa kuanza kuwekeza kwenye soko la hisa.


3 responses to “KITABU: MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X