UBUNIFU UNABORESHA BIASHARA YAKO
Kama wewe umekuwa mtumiaji wa muda mrefu kidogo wa mtandao wa WhatsApp utagundua kuwa mtandao huu umekuwa unafanyiwa marekebisho ya hapa na pale kila mara.
Kuna kipindi haya mambo ya status au WhatsApp business hayakuwepo.
Nakumbuka suala zima la kubold, italicize, underline na strikethrough na yenyewe hayakuwepo.
- Watu 60 Walioshindwa Karibia Kwenye Kila Kitu Na Bado Wakashinda Kwa Kishindo
- Penye Changamoto Pana Fursa.
- Maisha ni wajibu wako, ukishinda ni juu yako, ukishindwa ni juu yako pia
- Kwa Nini KUWEKA akiba ni Muhimu Hata Kama Hujui Lini Utakufa
- MAMBO MUHIMU KUHUSU KUWEKA AKIBA
Ila kadiri siku zilivyoendelea yamewekwa. Hayo ni machache tu kati ya marekebisho mengi ambayo wamefanya.
Ninachotaka kukwambia ni kwamba kwenye biashara yako, ni vizuri kuwa mtu wa kufiria nje ya boksi na kufikiria zaidi ya hapo ilipo kwa sasa.
Ubunifu utaitofautisha sana biashara yako na biashara za watu wengine. Maana hata ukisema ufanye biashara ambayo haijawahi kufanywa hapa duniani. Ndani ya miezi sita tu, kuna watu watakuona ukiifanya na wenyewe wataanza kuifanya. Kumbe basi, kitu pekee ambacho kinaenda kukutofautisha wewe na wengine ni ubunifu.
UBUNIFU SIYO MPAKA UWE NA WAZO AMBALO HALIJAWAHI KUWEPO
Wengi wanapofikiria ubunifu basi wanadhani, mbunifu yeyote anapaswa kuja na wazo la kipekee sana na wazo ambalo halijawahi kuonekana. Unaweza kuja na wazo la kawaida, ila kwenye biashara yako likawa linaleta mapinduzi.
Inashauriwa walau kila siku uwe unafikiria mawazo ya kawaida kumi tu na kati ya hayo utoe moja au mawili ambayo utayafanyia kazi. Ukiwa mtu wa kufikiria hivi ni uhakika kuwa mwaka mmoja baadaye, kama ni biashara, lazima tu utakuwa umeisukuma mbali.
UBUNIFU SIYO MPAKA UWE PROFESA
Ubunifu ni kitu tunazaliwa nacho. Ndiyo maana utagundua kwamba kila mtoto huwa anapenda kuumba vitu mbalimbali kwa kutumia udongo, mchanga au malighafi zozote anazoona zinamfaa.
Kwa hiyo hiki kiwe kiashiria kwako kuwa UBUNIFU ni kitu tunacho, tumezaliwa nacho na tunaenda nacho popote. Kadiri ambavyo utautumia ubunifu kwenye kazi, biashara au eneo lolote, ndivyo utakavyoimarika zaidi na zaidi.
Ungependa kujifunza zaidi kuhusu UBUNIFU?
Nakushauri upate nakala ya kitabu changu cha JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO.
kwenye kitabu hiki nimeongelea tu kuhusu suala zima la UBUNIFU, mwanzo mpaka mwisho.
Kukipata rusha elfu Saba tu (7,000/-) kwa 0755848391 au 0684 408 755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Unaweza pia kubonyeza hapa ili ukipate mara moja.
NB. Kwa Sasa kitabu kinapatikana kwenye mfumo wa nakala laini(ebook).
Umekuwa nami,
GODIUS RWEYONGEZA
Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri