Ushauri: Mbinu Za Kuuza Kitabu Kwa Mafanikio Makubwa


Unaendeleaje rafiki yangu. leo hii ninaenda kuwa najibu swali nililoulizwa na mmoja wetu ambaye anapitia kwenye changamoto baada ya kuwa amezindua kitabu chake na hakijafanya vizuri. Ebu kwanza tuone anachosema;

Habari yako kaka kwa mara nyingine!!!

Pole na hongera kwa kuendelea na wajibu ulokuleta duniani.

Ni takribani wiki 1 toka nitoe kitabu changu kiitwacho “THAMANI YA UHAI “. Nimejaribu kutangaza via WhatsApp na Facebook, ila sijapata hata mtu mmoja akihitaji kazi yangu.

Hiyo imepelekea kujihoji maswali kadhaa ambayo nimeamua kukushirikisha wewe. Maswali hayo ni kama haya :

  1. Hivi, mtu anatakiwa atafute soko la bidhaa au huduma yake ndipo aitoe au kuifanya au afanye ndipo atafute soko? Kipi kianze na kipi kifuatiwe?
  2. Hivi, watu huwa wanataka confirmation toka kwa watu wengine ili wanunue bidhaa au huduma ya mtu?
  3. Ni njia zipi zinatumika kutangaza bidhaa au huduma ili mtu apate wateja wengi na kupata faida anayoitarajia?
  4. Kuna watu ambao wanataka uwape chochote kitu ndipo wakusaidie kutangaza biashara yako. Je, ni sahihi kufanya hivyo? Ni kweli inaweza kumhakikishia mtu kupata atakacho?

Binadamu wengi ni vigeugeu, wanataka watumie vipaji vya wengine kujinufaisha wao. Hiyo ndio hofu yangu.

Mmh!!! Hayo ndio maswali yanayotawala kichwani mwangu bila ya kuwa na majawabu ya uhakika. Natumaini mrejesho mzuri toka kwako.

Ahsante sana na Mungu akubariki daima.

Habari yangu ni njema kabisa. Kwanza ningependa kukupongeza kwa hatua kubwa uliyochukua ya kuandika kitabu, kukihariri mpaka kukichapa. Hii ni hatua ambayo hiwezi kufanywa na watu wengi. wengi wameweza kuwa na ndoto kubwa za uandishi ila kwa miaka mingi sana hawajawahi kuandika hata sentensi moja. hivyo, kwa upande wangu nipende kukupongeza sana kwa hatua hiyo ambayo wewe mwenyewe umeweza kuifikia. Kitabu ni kitu ambacho kinadumu vizazi hata vizazi. Watoto wako na wajukuu wako watanufaika nacho na kwa hakika wataona kwamba wewe ulikuwa mtu unayejituma.

Shida ambayo unakumbana nayo wewe sasa hivi siyo kwamba upo peke yako. Wiki hii tu nimeongea na waandishi kama watatu na wote wanapitia kwenye changamoto kama hiyo hiyo ambayo wewe mwenyewe unapitia. Na hao ni wale tu ambao nimeongea nao. Na hiyo inaweza kukupa picha ni kwa namna gani ambavyo changamoto hizi zinawasumbua wengi.

Na. pengine kuna wengine ambao wapo kwenye hali mbaya zaidi.

Mitandao Ya Kijamii Inakuhadaa

Najua kwamba wengi wanapenda kuitumia mitandao ya kijamii  na kwa wengi mitandao hii ya kijamii ni sehemu ya kuonesha umaarufu wao au namna ambavyo wanavyokubalika. Iila kukubalika huku ambako kunaonekana kwenye mitandao ya kijamii siyo kukubalika halisi kwenye maisha ya kawaida. Wengi wanaokubali kazi zako mtandao wanazikubali tu bila hata kujua kama wamezikubali.

Ndio maana kuwa na wafuasi wengi kwenye hii mitandao siyo kigezo cha kuuza na wala kuwa na likes nyingi siyo kigezo cha kuuza zaidi. unaweza kuwa na wafuasi wengi ila bado ukawa huwezi kuuza bidhaa yako kwa watu wengi.

Sasa Je, Usiitumie Mitandao Ya Kijamii?

Hapana, endelea kuitumia mitandao ya kijamii. Ila sasa anza kuitumia kiusahihi kama ambavyo ninaenda kukuonesha muda siyo mrefu.

MAJIBU YA SWALI LA KWANZA:Hivi mtu anapaswa atafute soko la bidhaa au huduma yake

Zipo njia mbili za kuleta bidhaa au huduma sokoni ila njia nzuri ni kuleta bidhaa kulingana na kitu ambacho watu wanataka au wanapenda kulingana na changamoto walizonazo.

Hii inakuwa ni rahisi kwako kutangaza bidhaa yako maana moja kwa moja bidhaa yako au huduma yako inakuwa inagusa tatizo ambalo watu wanalo. Wewe ukienda kwa watu hutatumia nguvu kubwa kutangaza bidhaa yako. Badala yake utakachofanya ni kuongelea tatizo ambalo watu wanalo na namna ambavyo litatatatuliwa.  Hakuna mtu ambaye ana tatizo ambaye angependa tatizo lake liendelee kuwepo mara zote.

Watu wanapenda kupata huduma nzuri na za uhakika zinazotatua changamoto zao. Hii ni njia nzuri kuleta bidhaa sokoni na kuanza kuiuza siyo kwa kuuza bidhaa yenyewe bali suluhisho lililobebwa na bidhaa yako.

Kwa hiyo, kifupi wakati unatengeneza bidhaa au huduma zako anzia kwenye akili ya mteja. Jiulize mteja anataka nini? na hapa kama mwandishi haupaswi kukaa chini na kujiuliza swali la aina hiyo. la sivyo utapoteza muda mwingi nab ado hutapata kitu cha maana.

Ushauri wangu kwa waandishi wote ni huu:

  • Fungua blogu au tovuti. Na anza kuandika kwenye blog. Blg ni nzuri na haiwezi kulinganishwa na mtandao wowote ule wa kijamii. Haina ufanano wake.

Mfano mzuri tu wa blogu ni kwenyekutunza kumbukumbu. Mimi kwenye blogu yangu nikitafuta makala niliyoandika mwaka 2016, hainichukui hata dakika mbili. ila nikiingia facebook leo hii nitafuta makala niliyoandika mwaka 2016, nitakesha.

Lakini pia mitandao ya kijamii inapoteza vitu vingine baada ya muda. Leo hii mi

Sasa blogu inakusaidia kupangilia kazi zako kwa uhakika. Mitandao ya kijamii imewekwa kwenye mfumo wa kuonesha vitu vya vinavyojiri sasa hivi (breaking news) ili kuwafanya watu waendelee kuitumia. Hivyo, vitu vya nyuma hawana muda navyo.

Ila wewe kama mwandishi ukiandika kitu leo hii, kikasomwa na watu. kitu hicho hicho kinaweza kuwa na manufaa miaka mitano ijayo kwa watu wengine. Makala kama hii ninayoandika hapa, ikija kusomwa na mtu mwaka 2025 mwenye changamoto kama yako, bado itamfaa sana na bado atapata kitu cha kufanyia kazi. hivyo basi kama mwandishi kitu cha kwanza kabisa cha kukushauri. Toa uso wako facebook kwanza kwanza na utengeneze blogu. Blogu ni kitu kinachodumu. Siyo kitu cha siku moja tu.

  • Kitu cha pili, tengeneza email list. Hii ni orodha ya watu ambao wanakubali kazi zako kwa viwango vya juu kiasi kwamba wanwakuwa tayari kutoa baruapepe zao kwa ajili ya wewe kuwatumia mafunzo zaidi. hawa sasa ndio marafiki zako wa kweli ambao ukienda nao vizuri baadaye watakuwa tayari kukulipa kutokana na kazi zako unazofanya.

Hivyo, badala ya kukazana kukuza wafuasi kwenye mitandao ya kijamii, kazana kukuza email list yako. Kitu hiki watu wengi hawakipendi kwa sababu email list siyo kitu kinachoonekana kwa watu. ukiwa na watu 1000 wamesubscribe kwenye email yako. Hawawezi kuonekana kwa mtu moja kwa moja labda tu wewe uamue kuwaonesha watu, na watu wengi wanapenda kufanya vitu ambavyo vinaonekana kama kuwa na followers kwenye hii mitandao ya kijamii.

  • Kitu cha tatu, usitafute watu au wateja unapokuwa na njaa ya kuuza kitabu chako. Badala yake onesha kwamba unawajali na kuwathamini siyo tu kwa fedha zao bali kwa asili unawajali. Kila mara toa mafunzo na andika kiasi kwamba ujenge uaminifu kwa watu ili ikifika hatua ambapo utakuwa na bidhaa ambayo unayotaka kuiuza. Uweze kuiuza kwako kirahisi maana tayari wameshajenga uminifu kwako. hakuna mtu anapenda kuiachia fedha yake ambayo ameitafuta kwa hali ngumu kwa namna rahisi sana. hakuna.
  •  
  • Kila mtu anaipenda fedha yake. Kwa hiyo lazima wewe uwe ttayari umewadhihirishia kuwa wanaweza kutoa fedha zao kwako bila kupoteza kitu ndipo wafanye hivyo. Hapo sasa ndio unaweza kujiwekea utaratibu wa kuandika kwenye blogu yako kila mara ili watu waweze kuwa wanafuatilia mafuzno yako bila ukomo.

Sasa kadiri utakavyokuwa unaandika, kuna watu watakaojitokeza kuuliza maswali na kutokana na vitu ambavyo viwasummbua.  Haya ndiyo matatizo ambayo yanawakumba watu na hivyo vitabu au huduma unazoweza kutoa. Yaani, huhitaji kuumiza kichwa sana. Ukishaanza kuandika, maswali yanakuwa mengi. Na unaweza kuyajibu maswali haya kwa kuwaandikia watu vitbu maana maswali au changamoto nyingine zinajirudia mara kwa mara.

MAJIBU YA SWALI LA PILI: Hivi watu wanapenda konfirmationa kutoka kwa watu wengine ili wanunue  bidhaa au huduma.

Jibu ni ndio. TENA NDIO KUBWA. unavyoona Pepsi wanatangaza soda ya mkubwa wao akiwepo Diamond anakunywa mkubwa wao, siyo tu kwamba wanabahatisha. Hapo wanatumia umaarufu wake na kuwafanya watu wengine wakubali zaidi hiyo bidhaa.

Kiukweli ni kwamba, hata wewe, mtu unayemkubali akikwambia kwamba kanunue kitu fulani badala ya kitu fulani, ni wazi kuwa utawahi kwenda kukichukua. Sasa saikolojia ya watu ndivyo inafanya kazi hivyo.

Ukiweza kupata mtu wa kuwashawishi wengine wanunue bidhaa zako itakuwa vizuri. Ila kwa kuanzia fanya kama ambavyo nimekueleza. Tengeneza blogu, andika huko kwenye blogu yako, tengeneza email list ya watu ambao wanakubali kazi zako.

Kisha baada ya hapo toa thamani kwenye kazi ambazo unafanya. ili hawa watu wachache ambao wameanza kufuatilia kazi zako waweze kuzisambaza kwa watu wengine zaidi na zaidi. na hivyo ndivyo confirmation yako inavyoanza.

Hapa hauna excuse, ukitafuta njia ya mkato ya kuonekana maarufu mtandaoni, fanya hivyo. Ila ukiwa na ndoto kubwa na uandishi wako, basi utapaswa kufanya hivyo, miaka kadhaa ijayo hizi mbinu zitakuwa zimekusaidia wewe kusogea na kufika mbali sana.

Tumia njia ya shuhuda. Waombe watu wachache ambao wamesoma kitabu chako wakupe shuhuda. Zitumie hizi shuhuda kwenye kutangaza chako zaidi. onesha kwamba mtu alikuwa na hali fulani kabla ya kusoma kitabu chako na sasa baada ya kusoma kitabu chako amepata matokeo fulani.

Pia penda kuomba picha za watu wanaosoma vitabu. hii itawasaidia kuona watu wengine kuwa kitabu chako kimesambaa ila wao tu ndio hawajapata nakala ya kitabu chako. Hivyo, itakusaidia kuendelea kusogeza mauzo.

MAJIBU SWALI LA TATU: Ni njia zipi zinatumika kutangaza bidhaa au huduma ili mtu apate wateja wengi na faida anayotarajia.

Vitu vyote ambavyo nimekuwa nakueleza tangu mwanzo vilenga kukusaidia wewe kutangaza na kupata mafuriko ya wateja. Hivyo anza kwa kufanyia kazi hivyo kwanza.

Pia nimeandaa audio yenye inayoeleza MBINU 23 ZA KUUZA. Na hii ni maalumu kwa ajili ya waandishi tu. naomba upate muda wako usikikilize hapa.

Tatu. Usitangaze mara moja

Kwa mbinu ambazo utazisikiliza hapo juu, usitangaze bidhaa yako mara moja au mara mbili. endelea kuitangaza mara kwa mara.

Tafiti nyingi zinaoesha kwambna mtu anaposikia tangazo au kitu mara ya kwanza anakuwa hajali. Ila anapokisia kuanzia mara saba ndio anakuwa tayari kuchukua hatua.

Pia andika kitabu kingine. kama mwandishi usiwe na kitabu kimoja. Ukiuza kitabu kimoja na mteja akanunua kwako, baada ya hapo unampoteza maana unakuwa hauna kitu kingine cha kumuuzia. Ila sasa ukiwa na vitabu hata viwili au vitatu maana yake mtu akinunua cha kwanza utaweza kumshawishi anunue na cha pili au ajiunge na huduma fulani au apate kozi fulani n.k.

Kwa njia hiyo sasa ndio unakuwa unaanza kupata faida yako.

Mambomengine nimeyaeleza kwenye audio hii hapa. ifuatilie vizuri ina mazuri kwa ajili yako.

MAJIBU SWALI LA NNE: Kuna wAtu wanataka uwape chochote kitu   ndipo wakusaidie kuytangaza biashara yako. Je, ni sahihi kufanya hivyo, ni kweli inaweza kumhakikishia mtu kupata anachokitaka.

Hapa nashauri kwanza uangalie na watu alionao mtu husika. Kama ana watu wanaoendana na wale uliowalenga ni sahihi kumlipa ili akutangazie bidhaa yako. Khayo ni matangazo ambayo unapaswa kufanya pia.

Na hii ni njia n yingine ya confirmation pia. Mtu akisikia kutoka kwa yule anayefuatilia kuwa amesoma kitabu chako na kimemfaa basi atakuwa tayari nay eye kutoa fedha ili akipate. Ila kuwa makini, hakikisha kweli huyu mtu anao wafuasi na watu ambao wanaendana na bidhaa zangu. kisha mpe hela akutangazie. Ni vizuri ukianza kidogo ili uone mrejesho.

Kuna vitu hapa ninataka uvijue pia

Kwanza, watu wanaokwambia toa kitabu tutanunua mara nyingi huwa hawanunui

Kuna watu wanaweza kukwambia kuwa tupo nyuma yako. Toa kitabu tutakisoma. Ila ukishatoa kitabu wanaingia mitini. Hiki kitu kisikukatishe tamaa, wewe weka nguvu na weka kazi. hakuna kazi ambayo huwa inapotea bure hata kidogo. unaweza usione matokeo kwa muda mfupi ila kwa muda mfupi matokeo yataonekana tu. endelea kupambana.

Pili kuna vitabu vingi ambavyo havikufanya vizuri hapo mwanzoni ila sasa baadaye vikafanya kazi vizuri. Historia za waandishi wa aina hiyo ni nyingi tu. hivyo, na wewe endelea kukizania kitabu chako.

Tatu, Tangaza kitabu kama chako kama vile hakuna maisha nje ya kitabu chako. Yaani, iwe kama vile kitabu ni tiketi ya kwenda mbinguni.

Nne, jifunze copywriting. Huu ni ujuzi muhimu ambao utakusaidia sana kama mwandishi. Kama kuna kitabu kimoja cha copywriting utakachopaswa kusoma basi kiwe ni Cha How To Write A Copy That Sells Cha Ray Edwards

MUHIMU SANA: Hakikisha umepata kitabu (ebook) cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 kwa elfu tano tu leo hii. Kitabu hiki kina mengi ya kukusaidia wewe. Rusha elfu tano sasa 0755848391 jina Ni GODIUS RWEYONGEZA. Baada ya hapo utatunitumia baruapepe yako au namba yako ya WhatsApp ili nikutumie kitabu.

Karibu


4 responses to “Ushauri: Mbinu Za Kuuza Kitabu Kwa Mafanikio Makubwa”

  1. Nimesoma nimeelewa, mimi kama mwandishi naahidi kufanyia kazi yote yaliyoandikwa hapo. Asante sanà.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X