JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA MTANDAONI-2


Umewahi kujiuliza ni kwa namna gani unaweza kutengeneza kipato kwa njia mtandao wa intaneti? Umewahi kujiuliza kitu kama hiki?

Kuna kipindi nilikuwa nikisikia stori za watu kama Millard Ayo, kwamba hawa watu wanatengeneza fedha kwa njia ya mtandao. Sasa wali langu lilikuwa hivi hawa watu wanawezaje kutengeneza fedha kwa njia ya mtandao? Wanawezaje, hilo swali tu mpaka sasa hivi limenifungulia  dunia na kunifanya niweze kuona vitu vingi sana ambavyo kiuhalisia nisingeweza kuviona bila ya kujiuliza swali la alina hiyo.

Najua kuna watu wengine wengi wanajiuliza swali la aina hii? Pengine na wewe utakuwa unajuliza swali la aina hii. Sasa swali langu kwako ni je, unawezaje kutengeneza fedha kwa njia ya mtandao? Unawezaje?

Kabla sijajibu hili swali, nataka kwanza tujue kwenye maisha watu wanatengenezaje fedha? Kwa mfano, wewe unatengezaje fedha? Kama umeajiriwa, maana yake unaenda kazini unafanya kazi na mwisho wa mwezi unalipwa, unatoa thamani kwanza ndipo unakuja kulipwa.

Kama unafanya biashara, maana yake unapaswa kuwa na bidhaa ambazo watu wanazihitaji, na unapaswa kuzileta bidhaa hizo kwa watu sahihi ili wakupe fedha. Bado tunarudi palepale kwamba unapaswa kutanguliza thamani kwanza.

Kwa chochote kile unachofanya na kinakuingizia fedha halali, ni wazi kuwa utakuwa unafanya kitu kwanza, kisha kitu hicho ndipo unakuja kulipwa.

Nimeona niliweke hili wazi, maana vijana wengi wanapofikiri kutengeneza fedha mtandaoni, basi kitu cha kwanza kabisa wanachofikiri ni kukaa bure bila kufanya kazi yoyote na kulipwa fedha ndefu. Hakuna kitu kama hicho.

Mtandao wa intaneti haumaanishi kwamba ulale na utengeneze fedha ya bure bila kufanya kitu chochote. Badala yake mtandao wa intaneti, upo kurahisisha huduma unauyoitoa au kuifanya bishara yako iweze kuwafikia watu wengi zaidi kwa haraka na kwa gharama kidogo.

Kiufupi kwenye ulimwengu wa leo kila mtu anapaswa kujitahidi kudandia teknolojia.

Kwa biashara au kitu chochote kile ambacho unafanya unapaswa kukiweka mtandaoni, ili kiweze kuonekana ka watu wengi zaidi. kitu ambacho kitakusaidia wewe kukutana na wateja sahihi wa biashara yako.

Kwa hiyo nifanyeje ili niweze kutengeneza fedha mtandaoni.

ANZA KWA KUTOA THAMANI

Ngoja nikwambie kitu, watu wanapenda fedha zao. Hakuna mtu ambaye ametafuta fedha kwa shida, atapenda kuona kwamba fedha alizozitafuta kwa shida zinapotea bila manufaa yoyote yale, badala yake kila mtu anapenda kuona kwamba fedha zake alizozitafuta kwa shida anazitumia vyema. Kwa hiyo, kitu cha kwanza kabisa unachopaswa kufahamu kama unataka kutengeneza fedha mtandaoni ni kwamba unapaswa kutoa thamani kwa watu.

Wasaidie watu kupata wanachotaka

USIINGIE MTANDAONI KWA KUFIKIRI KUTAPELI WATU

Kama nilivyokwambia ni kwamba watu wanapenda fedha zao, hivyo usije ukaingia mtandaoni kwa kufikiri kwamba unaweza kuwatapeli watu fedha zao na kutokomea. Hizo ni fikra za kimasikini sana na hicho kitu ndicho kimefanya vijana wengi washindwe kuendelea  wala kufanya kitu chochote kikubwa maishani.

Mara zote kuwa na fikra za namna gani ambavyo unaweza kuwasaidia watu kwanza. Watangulize watu mbele, maana watu wakinufaika na wewe ndio unakuwa unanufaika. Sijui unanielewa…

BADILI KITU UNACHOFANYA NA KUWA CHA KITEKNOLOJIA

Ukiangalia biashara kubwa za sasa hivi, hakuna kitu kikubwa ambacho wanafanya tofauti na kwamba biashara hizo nyingi zilikuwepo kwa miaka mingi sana iliyopita.

Biahsara ya kuuza vitabu ni biashara ambayo imekuwepo kwa miaka mingi sana, ila sasa kijana mmoja alifikiria kwamba badala ya kuwa tunazunguka na kutoka huku kwenda kule tukitafuta vitabu kwenye maduka ya vitabu, kwa nini vitabu visiwe vinauzwa mtandaoni na watu wanaweza kuvinunua mtandaoni, hapo ndipo ulipokuja mtandao wa Amazon.

Magari na usafiri wa taxi umekuwepo kwa siku nyingi sana. ila kilichofanyika kwenye ulimwengu wa leo ni kuweka vitu hivi kwenye mtandao wa intaneti. Kwa hiyo, unaweza kununua gari mtandaoni, unaweza kukodisha gari mtandaoni, unaweza kuwasiliana na boda akusafirishe kwa njia mtandao

Nakwambia hivi vitu ili ujue kwamba, unapozungumziwa mtandao, usianze kufikiria kitu cha ajabu cha kufanya kwa njia ya mtandao wa intaneti. Badala yake uanze kutumia vitu hivyo vhiyo ulivyonavyo sasa hivi na kuviweka mtandaoni.

Biashara hiyo hiyo uliyonayo sasa hivi, unapaswa kuiweka mtandaoni na kunufaika na uwepo wa mtandao

Kipaji chako hichicho ulichonacho, unapaswa kukiweka mtandaoni na kunufaika na uwepo wa intaneti.

Mgahawa wako huohuo, utengenezee ukurasa mtandaoni au hata tovuti, kisha sasa ndio uje kunufaika na uwepo wa mtandao.

Rafiki yangu, kwa kitu chochote na kwa vyovyote vile, hakikisha kwamba,

WEKA BIASHARA YAKO MTANDAONI

Kwa biashara yako yoyote ile ambayo unafanya, hakikisha kwamba biashara hii unaiweka mtandaoni. Hata kama ni kipaji chako.

Kuna njia nyingi za kuweka biashara yako mtandaoni kama kufungua tovuti au blog, kutengeneza ukurasa kwenye mitandao ya kijamii, kutengeneza

Anza kuwaonesha watu bidhaa zako, kama utahitaji kuwafundisha watu kuhusu bidhaa zako wafundishe ili waweze kuzielewa kiundani

Jibu maswali na maoni ya watu

Kusanya mawasilino ya watu wanaohitaji bidhaa zao na wasiliane nao

Wauzie bidhaa zako

Hakikisha pia umeangalia video hii hapa chini ambayo ina mafunzo ziaidi kuhusu namna unavyoweza kutengeneza fedha mtandani.

Umekuwa nami

Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE

kama umependa makala hii, nakuhakikishia kuwa utapenda na mafunzo yetu mengine tunayotoa kwa njia ya barua pepe. Jiunge na mafunzo hayo kwa kujaza taarifa zako hapa chini,


One response to “JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA MTANDAONI-2”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X