Kuna mtu mwaka 2010 alikuwa analalamika kuwa hana mtaji, mwaka 2015 alikuwa bado analalamika kwamba hana mtaji, mwaka 2020 bado analalamika kwamba hana mtaji. Na cha kushangaza zaidi ni kwamba mwaka 2025 atakuwa bado analalamika kwamba hana mtaji.
Hivi ni kweli kwamba huyu hana mtaji au hayuko makini?
Leo ninachotaka kuongea na wewe ni kwamba usikubali kubaki hivyohiyo. Usikubali kabisaa..
Dunia yenyewe tunamoishi huwa haibaki hivyohivyo. Muda wote inakuwa inajizungusha yenyewe kwenye mhimili wake…
Wewe pia uwe kwenye mwendo
Kama leo hii huna mtaji, basi anza kufanya utaratibu wakupata mtaji pesa kesho..
Kama leo hii huwezi kuwekeza laki moja kwa wiki.. wekeza elfu tano kwa wiki..
Kama huwezi kupata muda wa kutosha wa kutimiza ndoto yako ya kuandika kitabu, tumia dakika kumi tu kwa siku. Kamwe, kamwe usikubaili kubaki hivyo hivyo, ulivyo kila siku.
Badala yake ni kwamba kila siku endelea kuweka juhudi na nguvu zaidi kwenye kufanyia kazi malengo yako hata kama ni kwa udogo.
Nakubaliana na Marin Luther King Jr ambaye alisema kwamba kama huwezi kupaa, basi kimbia
Kama huwezi kukimbia, tembea.
Kama huwezi kutembea tambaa,
Ila kwa vyovyote vile hakikisha mara zote hupo kwenye mwendo.
Kwa hiyo, basi usikubali kukaa ukiwa umetulia bila ya kufanya chochote. Kuwa kwenye mwendo mara zote.
SOMA ZAIDI: MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA
NB: Ile ofa ile, ya idi ile ya mtu mmoja kujiunga na kozi yangu ya uandishi, imeshachukuliwa. Pole sana, kama ulikuwa unaihitaji, basi ndio hivyo haipo tena.
Unachoweza zaidi kufanya ni kujiweka kwenye listi ya watu watakaofuata baada ya kozi hii kuisha. Kama ungepennda kuwa miongoni mwa wale watakaoshiriki kozi hii siku za mbeleni. Nitumie ujumbe wenye neno UANDISHI 2022. Ili nafasi zikiwepo tukwambie. Nitumie ujumbe kwa namba 0755848391
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz
One response to “Usikubali Kuendelea Kubaki Hivyo hivyo”
[…] SOMA ZAIDI: Usikubali Kuendelea Kubaki Hivyo hivyo […]