Vitu viwili ambavyo hakuna MTU anapaswa kukuzidi


Rafiki yangu, SIKU ya leo ningependa kukwambia vitu viwili ambavyo hakuna MTU anapaswa kukuzidi kwenye kuvifanya. Vitu hivi ni

1. Kufanya kazi kwa bidii
Acha watu wakuzidi kwenye mambo mengine yote ila wasikuzidi kwenye kufanya kazi kwa bidii.

Kufanya kazi kwa bidii kupo ndani ya uwezo wako. Kwa hiyo kuanzia leo, acha watu wakuzidi kwenye vitu vingine Ila siyo kwenye kufanya kazi kwa bidii.

2. Kujifunza kwa bidii
Hiki Ni Kitu kingine ambacho hakuna mtu yeyote anapaswa kukuzidi kwenye kufanya. Hakikisha mara zote unazama kwenye kujifunza na kuelewa vitu kwa kiasi ambacho hakuna mtu mwingine mwenye elimu na uelewa mkubwa kukuzidi wewe.

Kila SIKU jifunze. Jifunze kwa kusoma vitabu, jifunze kwa kuhudhuria semina na maonesho, jifunze kwenye kozi na maeneo mengine.

Mara zote jifunze rafiki yangu. Hakuna mtu yeyote ambaye anapaswa kukuzidi kwenye kujifunza hata siku moja.

NB: Kwa kuanzia, hakikisha umepata audiobook zangu tatu ili uanze kuzisikiliza. Audiobook zenyewe ni

  1. JINSI YA KUIFIKIA NDOTO ZAKO
  2. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
  3. MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE

Kila audiobook Ni 20,000/- Ila Leo nakupa ofa. Lipia audiobook moja nikupe audiobook nyingine mbili bure.

Badala ya 60,000/- utaipia elfu 20,000 tu, nami nitakupa audiobook zote tatu.lipia Sasa kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Baada ya hapo, nitakutumia audiobook zako.

Umekuwa nami rafiki yako,
Godius Rweyongeza
0755848391

, ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X