Rafiki yangu, najua mwanzoni mwaka huu watu wengi wameweka malengo mengi ambayo watakuwa wakiyafanyia kazi.
Ila leo hii nipo hapa kukwambia aina moja tu ya malengo ambayo watu wameweka na nina uhakika haya malengo hayatimia. Malengo haya ni yale malengo ambayo watu wameweka na hawajaanza kuchukua hatua kuyafanyia kazi
Sifa moja kubwa ya malengo ni kwamba ukishayaweka ni lazima uweze kuyafanyia kazi ili yaweze kuja kwenye uhalisia. Kama mwaka huu, umeweka malengo na bado hujachukua hatua kuhakikisha kwamba malengo yako hayo yanakuja kwenye uhalisia. Basi ujue kwamba malengo hayo hayatakaa yatimie, na hayo ndiyo malengo ambayo hayatafanikiwa kwa mwaka huu wa 2023.
Rafiki yangu, hakikisha kwamba unaanza kuyafanyia kazi malengo yako ambayo umejiwekea kwa ajili ya mwaka huu wa 2023.
Melngo makubwa+hatua kubwa=mafanikio
SOMA ZAIDI: Mwongozo Sahihi Wa Kufikia Malengo Na Ndoto Zako
Kila la kheri.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.
Godius Rweyongeza ni mwandishi wa vitabu zaidi zaidi ya 20. Na ni mwendeshaji wa mtandao wa Songambele. Amekuwa akiandika kwenye huu mtandao huu tangu mwaka 2016. Kitabu chake cha Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni kimekuwa #1Best Seller kwa muda sasa kwenye mtandao wa GETVALUE
Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.
Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.
Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA
One response to “Hii ndiyo aina pekee ya malengo ambayo hayatafanikiwa ndani ya mwaka 2023”
Asante