Ufanyeje pale bidii yako inapotumika kama mtaji kwa watu wengine


Siku moja kuna rafiki yangu aliniuliza swali, alitaka kujua kuwa unafanyaje pale ambapo unakuwa na bidii na watu wanajua kuwa una bidii ila wanataka wakutumie.

Leo ningependa kujibu swali hili kwako wewe ambaye unaona kwamba una bidii na watu wanaitumia hovyo. Kwanza ningependa kwa kuanza kusema kwamba unapaswa kuwa na bidii kwenye kazi zako. hakikisha kazi yako yoyote ile unayogusa unaifanya kwa bidii, na siyo tu unaifanya kw abidii, bali unaifanya kwa ubora wa hali ya juu sana.

Kama wewe unaona kwamba lazima bosi wako awepo ili ufanye kazi. HUFAI.

Kama unaona kwamba bosi wako akitoka unapumua kwa nguvu kwa vile ametoke. Jua kwamba hufai.

Kama muda wa kazi unachati, unaongea umbea na unajificha kwenye migongo ya watu wngine. Hufai pia.

Rafiki yangu, wewe unapaswa kuwa mchapakazi wa hali ya juu sana. chapa kazi mara zote na sehemu zote, chapa kazi kwelikweli kiasi kwamba asipo mtu ambaye anapaswa kukuzidi kwenye kuchapa kazi.

Na kwenye hii dunia kuna vitu viwili ambavyo haupaswi kuruhusu mtu yeyote akuzidi kwenye kuvifanya, vitu hivi ni kufanya kazi kwa bidii na kujituma.

Kama kuna watu wanakuzidi kwenye hivyo vitu viwili. Basi funguka sasa hivi.

SASA baada ya kuwa nimesema hayo yote kuhusiana na kuchapa kazi kwa bidii. Inawezekana kuna watu watataka kukutumia wewe kwa manufaa yao zaidi kwa vile wanaona unachapa kazi kw abidii.

Na kama unasema watu wanakutumia, kwa lugha nyingine unamaanisha kwamba unafanya kazi kwa viwango vikubwa ukilinganisha na malipo ambayo unapata. Hivyo, unalipwa kiasi kidogo ukilinganisha na vile anavyopaswa kuwa analipwa.

Laiti ungekuwa unalipwa vizuri usingesema hivyo.

Kwa hiyo, kama unaona kwamba haulipwi kama vile unavyostahili unaweza kufanya yafuatayo.

Kwanza, unaweza kuamua kuacha kazi ili uweze kuweka juhudi zako sehemu nyingine ambayo itakulipa kulingana na kazi yako. Huu ni ukweli ambao pengine hukuutegemea lakini unapaswa kuubeba na kuufanyia kazi bila yakuchelewa.

Pili, kama unaona hiyo ni ngumu, basi unapaswa kuonana na bosi wako na kumwambia kuwa anapaswa kukuongeza malipo ili yaendane na viwango vya kazi unayoweka. Hapa nenda na vielelezo vyote ambavyo utahitaji kuonesha kwa bosi wako ili kuthibitisha hilo

Na tatu na mwisho, ni kwenda kwa bosi mwingine ambaye anaweza kukulipa kiwango unachoona unastahili.

Hayo ndiyo mambo matatu ambayo utahitaji kufanyia kazi rafiki yangu,ili kuhakikisha kwamba u

KITU Kikubwa zaidi ni kwamba haupaswi kuja kuzama kwenye kukazania kulipwa na bosi wako na wakati huohuo thamani na ufanisi wako ukapungua. Muda wote huo, ufanisi wako unapaswa kuwa unaongezeka.

Na hata wachezaji wa mpira huwa wanapandishwa viwango vya malipo kutokana na vile wanavyokuwa wanazidi kuwa bora zaidi kwenye kazi zao. Hivyo, kwa msingi huo basi, unapaswa kuongeza uchapaji wa kazi, ufanisi na ubora wa kazi bila kuacha ili kuendelea kupanda viwango

Kila la kheri

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X