Kosa kubwa unalofanya unapokuwa unaongea na watu


Sasa tukiwa bado hapo kwenye kuongea na kuzungumza na watu, siku ya leo ningependa tu kukwambia makosa ambayo watu huwa wanafanya wakiwa na watu, na jinsi ya kuyaepuka haya makosa ili uweze kuwa mtu mwenye ushawishi zaidi.

Kosa la kwanza kabisa ambalo watu huwa wanafanya ni kutumia simu wanapokutana na watu. Rafiki yangu katika ulimwengu wa leo, simu ni dhana muhimu sana ambayo tunaitumia. Nadhani na wewe utakuwa unaitumia sana, sana simu. Pamoja na raha nyingi za kuwa na simu, pamoja na mambo mengi ambayo simu inaweza kutusaidia kufanya, kuna kitu kimoja ambacho naona bado watu hawajaweza kukitambua. Na kitu hiki ni kwamba unapokutana na mtu kwa ajili ya mazungumzo, tafadhali usitumie simu.

Simu unayo muda wote. Yaani, wewe unashinda na simu na ulala nayo na pengine kitu uachoangalia kikiwa cha kwanza asubuhi ni simu.

Sasa pamoja na kuwa unakuwa na muda mwingi wa kutumia simu kiasi hicho ni kuwa unapokutana na mtu bado unataka kutumia simu tu. hivi hili ni kweli? Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu, watu wanapenda sana kuonekana wanathaminiwa, na njia ya watu kuonekana kwamba wanathaminiwa ni wewe kuwapa umakini wote pale unapokuwa unaongea hao watu. Hivyo basi, unapokutana na mtu yeyote, hakikisha kwamba hautumii simu.

Weka umakini na nguvu zako zote kwenye mazungumzo yako na huyo mtu. Achana na vitu vyote au kitu kingine ambacho hakiendani na mazungumzo.

Utakuwa na muda wa kutosha wa kutumia simu yako hapo baadaye, hivyo, kwa sasa achana kabisa na simu yako. Weka nguvu zako zote kwenye mazungumzo. Hiki kitu kitakusaidia kutogawa umakini wako. Hiki kitakusaidia kumsikiliza mtu kwa umakini. Hiki kitu kitakusaidia wewe kupata ushawishi zaidi wa watu.

Inashangaza sana kuona kwamba watu wanaalikana ili wapige stori halafu badala ya kupiga stori, wanaanza kuongea na simu, wanaanza kuchati na kutuma jumbe.

Ukiamua kwamba unaenda kukutana na mtu, usitumie simu.Na kama kutakuwa na ulazima wa wewe kutumia simu. Basi mwombe huyo mtu ambaye umekutana naye kwamba ungependa kuongea na mtu fulani mara moja au ungependa kumtumia mtu fulani ujumbe mara moja kisha unaendela na mazungumzo.

Siyo unaongea na mtu halafu unatumia simu yako, hiyo ni dharau. Yaani, mtu ameacha majukumu yake yote, amekuja kukutana na wewe. Halafu, wewe unatumia simu muda wote. Huo ni ukosefu wa nidhamu aisee.

Achana nao.

Kosa la pili amablo watu wanafanya ni kutoangalia watu kwenye uso. Naam, unapooongea na watu unapaswa kuwaangalia watu kwenye uso. Hiki kitu kitaonesha kwamba uko makini kwenye mazungumzo ambayo yanaendela, lakini pia kitakusaidia wewe kuweza kumfuatilia mhusika kwa ukaribu na kuona namna anavyowasilisha mada kwako. Sambamba na hilo kumwangalia mtu usoni kunaonesha kwamba uko makini sana na unajali.

Sasa kuanzia leo hii usiongee tu na watu. ukiongea na mtu yeyote yule hakikisha kwamba unaongea na ukiwa umemwangalia usoni. Mara zote, mwangalie huyo mtu usoni. Hiki kitu kitakupa maksi kubwa sana.

Juzi juzi wakati napita mtandaoni nilikutana na nukuu ya

Anasema kwamba kama unaangalia simu kuliko unavyoangalia watu usoni, jua kwamba kuna kitu kikubwa unakosea.

Kumbuka hii ni nukuu ya mkurugenzi wa kampuni kubwa ya APPLE inayozalisha simu. Lakini bado anasisitiza wewe kuwaangaliwa watu usoni kuliko unavyoangalia simu yako. Na leo hii kwenye hii makala, bado naendelea kukusisitiza wewe kuendelea kuwaangalia watu usoni hasa pale unapokuwa unaongea nao.

FANYA HIVYO MARA ZOTE,

Kwa upande mwingine inawezekana hiki kitu hujakizoea. Kama hujazoea hiki kitu, kuna kitu kimoja tu unaweza kufanya kuanzia sasa hivi. Na kitu hiki siyo kingine bali ni kuhakikisha kwamba unaanza kujenga utaratibu wa kuangaia watu usoni pale unapokuwa aunaongea nao. Fanya hivyo kuanzia siku ya leo.

Nakutakia kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X