Kwaheri 2023: Mambo 12 Ambayo Mwaka 2023 Umenifunza


Mwaka 2023 sasa unaisha.

Umekuwa ni mwaka bora sana kwangu, na umekuwani mwaka ambao nimeweza kufanya mengi, kuna mengi ambayo naweza kuandika kuhusu mwaka 2023 ila kwa leo nitaandika haya ambayo mwaka 2023 umenifundisha.

 1. mwaka 2023 umenifundisha kuwa kuwa mtandao wa intaneti una mkono mrefu. Najua wengi tumezoea kusikia kwamba serikali ina mkono mrefu. Lakini mwaka 2023 umenifundisha pia kuwa mtandao wa intaneti una mkono mrefu. Kuna makala nimekuwa naandika kwenye hii blogu tangu mwaka 2016 mpaka leo. Baadhi ya hizo makala hazikusomwa sana mwanzoni, ila kadiri siku zinavyokwenda watu wanazidi kuzisoma na kunufaika nazo. Japo nilishaandika hizi makala kwa muda mrefu ila mpaka leo hii kuna watu wanazidi kunufaika na hizo makala, na hii ni kwa sababu tu zipo mtandaoni. zingekuwa sehemu nyingine wasingeziona. Na ndio maana nimekuwa nashauri watu wengi wawe na blogu badala tu ya wewe kuwa unaandika vitu vyako vizuri na kuviweka whatsap ambapo baadaye vinapotea. Kama hauna blogu, mwaka 2024 hakikisha kwamba unaliweka hilo kama lengo lako la kuhakikisha unakuwa na blogu na hasa kama unashirikisha maarifa kwa njia ya mtandao. CHochote kile unachoandika hata kama ni kidogo, kiweke kwenye blogu, kuna siku kitakuwa na manufaa kwa watu wengine.
 2. Mwaka 2023 umenifundisha kuwa kufanya kazi kwa bidii kunalipa japo unaweza usione matokeo ya kwa muda  mfupi muda mwingine. lakini unapaswa kuwa tayari kuwekeza  kwenye kufanya kazi kwa bidii kama ambavyo wakimbiaji wa Marathoni huwa wapo tayari kuwekeza kwenye kufanya mazoezi kwa miaka minne kabla ya KUKIMBIA marathoni ya dakika kadhaa.
 3. mwaka 2023 umenifundisha kuwa tatizo la ajira nchini Tanzania ni kubwa, lakini pia vijana hawapendi kufanya kazi. Hili nimeligundua baada ya kuanza kuajiri. Mwanzoni nilifikiria kupata watu sahihi ni rahisi sana maana vijana wengi hawana ajira, ila kilichotokea ni tofauti. Vijana wengi kweli hawana ajira, ila pia hawako tayari kufanya kazi. Wanapenda pesa ila hawataki kazi.
 4. Mwaka 2023 umenifundisha kuwa kuchukua hatua ya kwanza ni muhimu sana. Lakini pia sambamba na hili mwaka huu umenifundisha kwamba unapopanga kufanya kitu kifanye. Mwaka huu tulipanga kufanya semina; kutokana na sababu kadha wa kadha kuna watu walidhani haitawezekana kufanyika. na wengine walisema huwezi kufanya semina bila ya kuwa na udhamini wa taasisi kubwa kama benki n.k. na hata wengine waliokuwa wameonesha nia ya kuhudhuria semina hawakufanya hivyo. Ila kwa kuwa tulikuwa tumepanga kufanya semina. Hatukurudi nyuma. Mwezi wa sita tarehe 24 tuliweza kufanya semina moja nzuri sana hapa Mjini Morogoro, ilihudhuriwa na watu wasiozidi 12, ila ilikuwa ni moja ya semina bora sana za mwaka 2023. Na hiki kimetupa mwanya wa kufanya semina nyingine zinazofuata, mfano mwaka 2024 mwezi wa sita tarehe 29 tutafanya semina ya ana kwa ana maeneo ya ubungo Dar. Unaweza kujiandikisha mapema, ada yake itakuwa ni laki moja kwa kila mshiriki. kujiandikisha tuma ujumbe kwenda namba ya simu 0755848391 sasa.
 5. Mwaka 2023 umenifundisha kwamba haupaswi kutegemea kitu kimoja au namba moja. Kama ni simu na unaitumia kwa kazi, usiitegemee moja. Kama ni kompyuta na unaitumia kwa kazi, usiitegemee moja, kuna siku hiyo unayoitegemea inaweza kugoma. Kama ni wafanyakazi usimtegemee mmoja, siku akiacha kazi utapasuka moyo, nadhani labda mwenza tu ndiyo unapaswa kuwa naye mmoja, ila vingine tafuta namna ya kuwa na ziada ili ikitokea moja imepata shida au dharula nyingine unaweza kuendelea mbele.
 6. Mwaka 2023 umenifundisha kuwa ukiajiri, lipa watu wako kwa wakati hata kama malipo unayowapa ni kidogo. Kamwe usimcheleweshee mfanyakazi wako mshahara wake..Hili somo nimejifunza kwa taabu sana baada ya kumcheleweshea mmoja wa wafanyakazi wangu maokoto yake, akaacha kazi na alikuwa ni mtu wa muhimu sana. Kwa lugha ya sasa hivi ni kwamba sikuzingatia maokoto. MWAKA 2024 ZINGATIA MAOKOTO.
 7. Mwaka 2023 umenifundisha kwamba, unapaswa kutangaza bidhaa au biashara yako au kitu chochote unachofanya kwa njia zote unazoweza kutumia. Mitandao, redio, runinga, viperushi kutaja ila vichache, mwaka huu kila njia niliyotumia kwenye kutangaza kwa namna moja au nyingine imeniletea wateja.
 8. Mwaka 2023 umenifundisha kuwa popote unapokuwa, itangaze biashara au bidhaa yako. Nilikuwa nasafiri kwenda Dar, kwenye gari nilisimama kwa ajili ya kuongea na wasafiri kuhusu umuhimu wa kusoma vitabu. Huwezi amini, miongoni mwa wale waliosikia kile nilichosema kuhusu usomaji wa vitabu, walihamasika, na sasa kuna watu wawili ambao wamekuwa wasomaji wazuri wa vitabu. Hii yote ni kutokana na mazungumzo yangu mafupi siku hiyo kwenye basi wakati tunatoka Morogoro kwenda Dar.
 9. Mwaka 2023, umenifundisha kuwa uwekezaji unanipa ridhiko la moyo sawa na kuandika kunavyonipa ridhiko la moyo. Huu umekuwa ni mwaka ambao nimekuwa nikifanya uwekezaji kwa nguvu zote, na mara zote ambazo nimekuwa nafanya uwekezaji, nimekuwa najisikia vizuri.
 10. Mwaka 2023 umenifundisha kuwa unapofanya kazi, unapaswa kuifanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Maana hiyo kazi itadumu, lakini pia itawafikia wengi. Kuna baadhi ya vitabu nimeandika zaidi ya miaka sita iliyopita. Ila watu wamevisoma mwaka huu na vimekuwa vitabu vyenye msaada mkubwa kwao. Laiti ningekuwa nimeviandika hovyo visingeweza kuwa vyenye msaada kihivyo. Vitabu hivyo ni pamoja na kitabu cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA ambacho ndani ya huu mwaka kimepata mpaka nafasi ya kuongelewa kwenye bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hii ilikuwa ni baada ya mbunge, mh. Shamsi Vuai Nahodha kuwa amekisoma na kukipenda. Kitu hiki kilifanya watu wengi wapende kujipatia nakala zao, na kweli kila aliyepata nakala alitaka na rafiki yake aipate. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu, niliandika kitabu hiki vizuri mwaka 2018, na sasa watu ndiyo wanatambua uwepo wake na wanakisoma kwa nguvu zao zote. Na wewe pia usisite kujipatia nakala ya kitabu hiki cha TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA: tatizo ni rasilimali watu tunaowapoteza. Kupata nakala yako wasiliana na 0684408755 sasa.
 11. Mwaka 2023 umenifundisha kukaa na watu sahihi. Nikijaribu kuangalia mambo yote makubwa ambayo nimeyafanya mwaka 2023 ni kwa sababu nyuma yangu nilikuwa na watu sahihi walionizunguka, la sivyo mengi yasingewezekana.
 12. Mwaka 2023 umenifundisha kuwa hakuna elimu au kitu chochote unachojifunza kinachopotea. Unaposoma kitabu siyo kwamba unapoteza, na kama kuna baadhi ya vitu ambavyo hujatumia siyo kwamba ndiyo umepoteza. Ila kuna siku, saa na dakika kitu hicho utakitumia na kitakuwa chenye manufaa kwako.

kuna mengi ambayo mwaka 2023 umenifundisha, ila kwa leo itoshe tu kusema kwamba hayo ndiyo masomo makubwa ambayo binafsi nimejifunza 2023.

Wwewe mwaka 2023 umekufunza kitu gani? Mjadala huu unaendelea kwenye kundi la whatsap, hapa

Au kwa email ambapo unaweza kunijibu kwa kunitumia ujumbe kwenda godiusrweyongeza1@gmail.com

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye ni kocha, mjasiriamali na mkufunzi. Unaweza kujifunza zaidi kwake kwa kujiunga na mafunzo ambayo huwa anatoa kwa njia ya barua pepe hapa.

Kupata makala maalum ambazo huwa anaandika kwa watu maalum. Bonyeza hapa

KUMBUKA:

Ofa ya msimu wa sikukuu inaelekea kuisha. Mwisho ni tarehe 1.1.2024 saa sita usiku

*Ofa ya kwanza*
*Unapata vitabu 6 (softcopy kwa 20,000/- au vitatu kwa 10,000/-* 🤭

Chagua hapa, nipe taarifa👇🏿

1: JINSI YA KUTENGENEZA MSHAHARA NJE YA MSHAHARA
2: NGUVU YA WAZO
3: NGUVU YA KUWEKA MALENGO
4: MWONGOZO WA WAPAMBANAJI
5: MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA
6: VYANZO VINGI VYA KIPATO

Lipia 10,000 upate vitabu VITATU, LIPIA 20000 Upate vyote SITA. ( Softcopy)

Namba ya MALIPO ni. 0684408755 GODIUS RWEYONGEZA

*Ofa ya pili*

Unapata audiobook 6 kwa 15,000/- TU. Audiobooks zenyewe ni.

1. NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
2. JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO
3. MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE
4. JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO
5. MAAJABU YA KUWEKA AKIBA
6. KIPAJI NI DHAHABU

Gharama ya hizi audiobooks ni zaidi ya ~100,000/~ ila kwa Sasa lipia 15,000/- TU upate zote sita.

Namba ya malipo ni 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

*Hii ndiyo Ile ofa ushindwe mwenyewe*

Wewe ofa Yako msimu huu ni ipi?


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X