Malengo Yako Ya Mwaka 2024 Usimwachie Mungu


Ni mwaka wa tatu sasa tarehe kama ya leo naandika makala  inayosisitiza kuhusu malengo na kwa nini haupaswi kumwachia malengo yako mungu. Mwaka juzi niliandika makala hii hapa. 

Makala hiyo hapo juu ina swali zuri sana ambalo nimekuwa napenda kuendelea kuwauliza watu kila mara.

Na hata juzi nilituma ujumbe kwa watu wa nguvu kupitia whatsap. Ujumbe huu ulikuwa na swali lililokuwa linauliza, umejiandaaje kwa ajili ya mwaka 2024? Lengo lako la mwaka 2024 ni lipi au unamwachia Mungu?

Cha kushangaza ni kwamba asilimia kubwa ya watu walisema kwamba wanamwachia Mungu. Kwa sababu ni mweza yote,

Ni alpha na omega.

anajua kesho yako

anachopanga yeye mwanadamu hawezi kupangua

na mengine mengi.

Ukweli ni kuwa malengo yako haupaswi kumwachia Mungu, japo ana sifa hizo ambazo watu wamekuwa wanatoa, ila ukweli ni kuwa Mungu mwenyewe anakuangalia wewe unavyofanya.

Mungu hawezi kukubariki ukiwa umebweteka, huna malengo, huna mwelekeo wowote, upo tu hapo. Kitendo cha wewe kukaa chini na kuweka malengo ni sawa na sala ya kumwambia Mungu kwamba sasa naomba baraka zako uzielekeze hapa.

Kitamfanya aachilie baraka zake kuelekea kwenye lengo lako, kuliko pale unapokuwa hauna lengo wala ndoto yoyote ile unayoifanyia kazi.

Umekuwa unaishi kwa miaka mingi bila ya kuwa lengo lolote. mwaka huu fuata mwongozo huu hapa kuweka malengo. Hata kama hujawahi kuweka malengo, ebu ufanye mwaka huu kuwa mwaka wako wa kwanza wa kuishi kwa kufuata malengo.

Kamwe usije kusema kwamba nimechelewa kuweka malengo. Muda bado, ndiyo kwanza kumekucha ndani ya 2024! Na kama unajua biashara mara zote ni asubuhi. Huu ndiyo muda wenyewe wa wwe kuutumia muda wako vizuri sasa.

Ukiwa na malengo, utakuwa na kusudi, utakuwa unajuwa wapi unaelekea na nini ufanye ili uweze kufika huko.

SOMA ZAIDI: Hatua Muhimu Katika Kuweka Malengo

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X