Salaam Za Kheri Ya Mwaka Mpya 2024 Kutoka Kwa Godius Rweyongeza


Rafiki yangu mpendwa, salaam. Nichukue nafasi hii kukutakia kheri ya mwaka mpya 2024. Ule mwaka uliokuwa umeusubiri sasa ndiyo huu hapa umefika. Yale mambo yote uliyokuwa umesema kwamba utayafanya ndani ya huu mwaka, sasa ndiyo muda muafaka wa kuyafanya.

Biashara uliyokuwa umesema kwamba utaanzisha mwaka 2024, hakikisha sasa unaianzisha. Akiba uliyokuwa umesema utaweka. Iweke.

Kiufupi lengo lako kuu la mwaka huu hakikisha kwamba unalifanyia kazi bila ya kuacha.

mwaka huu ufanye kuwa Baraka kwako. Na utaufanya hivyo kwa kufanyia kazi vile ulivyoopanga kufanya kuliko tu kuishia kusema kwamba utafanya.

 

Tumezoea kwamba watu huwa wanasherehekea sikukuu nyingi ambazo hawajasbabisha wao. Sikukuu ambazo huwa zinatokana na kalenda. Sikukuu hizi ni pamoja na mwaka mpya huu ambao unasherehehekea leo, siku za iddi, pasaka, sikukuu zote za kiserikali, krismasi na yinginezo. Mwaka huu usiishie tu kusherehehea sikukuu zinazotokana na kalenda. Sherehekea matokeo uliyopata kutokana na kufanyia kazi malengo na ndoto zako.

 

Kazi ya kufanya leo. Andika malengo yako makubwa ambayo utayafanyia kazi ndani ya mwaka 2024. Kila la kheri

Soma zaidi:Kheri ya mwaka mpya 2022 

Kheri Ya Mwaka Mpya Na Mambo 12 Unayopaswa Kufanya Kuanzia Leo


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X