Vita Ya Maisha Anashinda Mtu Anayefikiri Anaweza


Tarehe 25/9/2016 niliandika makala hii inayoeleza Jinsi Ya Kuepuka Kujiua Mwenyewe Kiakili

Mwishoni nikahitimisha Kwa kusema kwamba vita vya maisha anashinda mtu ANAYEFIKIRI ANAWEZA.

Leo hii nimerudia kuisoma hii makala, nilichogundua ni kwamba hii makala Bado Ina nguvu Leo hii sawa na nilivyoandika takribani miaka 7 iliyopita.

Ukweli ni kuwa kile unachojaza kwenye akili Yako Ndicho unakuja kupata kwenye uhalisia.

Kile unachojiambia na kuaminisha ubongo wako, Ndicho kinatokea.

Miaka mingi iliyopita kuna wapiganaji walienda kupigana na jeshi kubwa. Jeshi ambalo lilikuwa limewazidi Kila kitu.
Wingi wa wanajeshi
Ubora wa vifaa

Na ukweli mwingine ni kuwa Hilo jeshi lilienda kupigana ugenini.

Kilichotokea. Kapteni wa jeshi baada ya wanajeshi kushuka Kutoka kwenye boti zao, aliamuru meli zote zichomwe moto. Halafu akatangaza mbele ya jeshi lake na kuwaambia, mnaona hizo meli zinavyoungua, hii ndiyo kusema kwamba, hatutoki hapa, labda tushinde

Kitendo hiki Cha kuchoma boti zote moto kiliamsha Ari wa kupambana miongoni mwa wanajeshi.

Kila mmoja akaanza kufikiri juu ya ushindi
Kila mmoja akaanza kuishi kiushindi.
Na jeshi lilipigana mpaka likashinda.

Ninachotaka ufahamu siku ya leo ni kwamba, ushindi wa kwanza kabisa tunaupata akilini. Halafu baada ya hapo ndipo tunakuja kupata ushindi kwenye uhalisia.

Mwandishi wa kitabu Cha the secret of the millionaires mind kwenye hili amesisitiza kitu kikubwa sana.

Anasema,
BE-DO-HAVE
KUWA-FANYA-PATA

Ili nisikuache hewani, nitaelekza hili Kwa undani kidogo

KUWA

Unajua hii maana yake nini? Yaani, kuwa unachotaka, Anza kufikiri katika Ile namna.

FANYA

Sasa baada ya kuwa umetengeneza fikra sahihi, kinachofuata ni wewe kuanza kuishi Kile ulichotengeneza kwenye fikra zako.

Kwa mfano, kama umetengeneza fikra ya kuwa bilionea. Kinachofuata ni wewe kuanza kuishi kama MABILIONEA wanavyoishi.

Ukitengeneza fikra ya ukurugenzi, Anza kuishi kama wakurugenzi wanavyoishi.

Fikra zako Sasa, zilete kwenye uhalisia.

Halafu mwisho Sasa ndiyo utakuja

ku PATA hicho kitu ambacho umekijengea fikra Kwa muda mrefu na kukifanyia kazi.

Kinachowakwamisha Wengi ni kwamba wanataka wapate kwanza, halafu ndiyo waje wawe na fikra chanya.

wewe kuwa tofauti kidogo, anza kwa kuhakikisha kwamba unakuwa na fikra chanya, kuwa na picha ya kule unapoelekea na jione kama mtu ambaye tayari amefikia hilo lengo, halafu baada ya hapo. Pambana sasa ili kufikia malengo na ndoto zako hizo kubwa.

SOMA ZAIDI

  1. Badili Fikra zako Ili Ubadili Maisha Yako
  2. Mbinu za kutimiza malengo yako

RAFIKI YANGU,Kwa leo inatosha. Tukutane kesho, kutakuwa na mwendelezo wa makala hiihii hapahapa.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 39

For Consultation only: +255 755 848 391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X