Jinsi ya kuwakomesha watu wanaokukatisha tamaa kistaraabu kabisa (Ila Utakuwa Umewakomesha)


Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu. Kama hujawahi kukutana na watu ambao wanakukatisha tamaa, inawezekana hujawahi kuthubutu kufanya kitu cha tofauti na vile vilivyozoeleka kwenye jamii au hufikirii kwa ukubwa kabisa. Ni hivyo tu.

Ila kama unafanya vitu vya tofauti, ni wazi kuwa watu wataanza kukukatisha tamaa kwenye kile unachofanya.

Inawezekana watu wakakukatisha tamaa moja kwa moja kwa kauli zao. Mfano ni Kauli Hizi Tatu (03) za Kukatisha Tamaa ambazo nimezieleza kwenye hii makala, na ubora ni kwamba nimekueleza namna ya kuziepuka pia

Lakini habari njema ni kwamba, njia nyingine ya kuwanyamazisha watu wanaokukatisha tamaa, ni kwa wewe kufanyia kazi kile unachotaka kufanyia kazi bila ya kuacha, haurudi nyuma na wala hukwamishwi na kitu chochote.

Maneno yao yanakuwa  kama moto wa kuchochoea zaidi kile unachofanya. Hivyo, kitendo cha wewe kusikia kile wanachosema, unaamua kuongeza juhudi zaidil ili uweze kupata matokeo ambayo ni bora zaidi.

Hawa wanaokukatisha tamaa, wewe unapaswa kuwashangaza kwa kuwaonesha kwa vitendo kwamba umeweza kufanya na hicho kitu kimekuja kwenye uhalisia.

Kamwe rafiki yangu, usikubali kukata tamaa wala kurudi nyuma. MARA ZOTE SONGA MBELE

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X