Kanuni Ya Miezi Sita Kwenye Biashara, Na Kwa Nini Kila MfanyaBiashara Anapaswa Kuifahamu


Kuna kanuni ya miezi sita kwenye biashara ambayo wafanyabiashara wengi hawaifahamu. Ni kanuni muhimu ambayo kama mfanyabiashara unapaswa kuifahamu. Kutoifahamu kanuni hii kutakuponza sana

Kanuni hii inasema kwamba, ukianza kufanya biashara, ndani ya miezi sita ya kuanza biashara kuna watu wengine wataanzisha biashara kama hiyo.

HII kanuni inafahamika kama kanuni ya copy cat.

ikimaanisha kwamba baada ya miezi sita kuna watu watakuwa wanafnaya biashara kama ya kwako uliyoanza kufanya baada ya miezi sita.

Kuna watu watazalisha bidhaa kama hizo miezi sita baada ya wewe kuwa umeanza kufanya uzalishaji.

Kwa hiyo hakuna kitu unachofanya kwenye biashara yako ambacho kipo salama ambacho watu hawatakuja kukifanya.

sasa ili kujiweka katika mazingira ambayo watu hawataweza kukutoa kwenye biashara unapaswa kuzingatia mambo sita yafuayo

  1. Ni ubunifu. Yaani mara zote kuwa mbunifu kwenye kila kitu unachofanya. kuwa mbunifu kiasi kwamba watu wengine wawe mara zote wanatafuta namna ya kuweza kuendana na kile unachofanya na kile unachobuni.
  2. Jifunze kila mara. kuwa mtu wa kujifunza mara zote, wengi watakuwa wanaiga kwako ila siyo watu wa kujifunza. wewe kuwa mtu kujifunza na hasa kwa kusoma vitabu, majarida yanayoelimisha na kuhududhuria semina na mfunzo muhimu sana.
  3. kuwa na mfumo ambao wengine hawawezi kuufanyia kazi. Inawezekana ni mfumo wa namna ya kuhudumia wateja kwa namna ya kipekee. Au inawezekana ni mfumo wa kuwa na wafanyakazi ambao ni bora kabisa kwenye biasahra yako. Hakikisha unakuwa na kitu ambacho hakuna mtu mwingine mwenye nacho na kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana bila ya kuacha hata kidogo.
  4. Kuwa mtu wa kupokea maoni kutoka kwa wateja wako. Kwa kuanzia nashauri, upokee hasa maoni kutoka kwa wateja wako. Hawa ni watu ambao wametumia bidhaa zako na hivyo wakikwambia kitu, ni uhakika kwamba wanakuwa wanamaanisha hicho wanachokisema.
  5. Hata hivyo, ukipokea maoni kutoka kwa wale watu ambao hata hawajatumia bidhaa zako maana yake ni kwamba utakuwa unapokea maoni kutoka kwa watu ambao hawajapata uhondo wa kile ambacho umetengeneza. na inawezekana wasije hata siku moja kununua kutoka kwako.
  6. Amua kufanya kitu ambacho utafahamika nacho kwacho. Ndiyo, najua kuna vitu ambavyo unaweza kufanya, lakini kwa kuanzia fanya kitu ambacho utafahamika nacho kwacho. Kifanye kwa ubora mkubwa sana

rafiki yangu, hayo ndiyo mambo matano ya msingi sana ambayo unapaswa kufanya, ambayo yatakufanya uwe mbele ya watu wengine mara zote. Badala ya mara zote kuendelea kuwa unaiga kwa wengine. Yatakufanya kuwa mbunifu mara zote na kuja na vitu vya tofauti.

Kuna mambo 55 ya kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara, mambo haya yote yameelezwa kwenye hiki kitabu. Kupata nakala yako, wasiliana na +255 684 408 755
Hakikisha unajipatia nakala ya kitabu hiki. Tumia namba ya simu +255 684 408 755

SOMA ZAIDI: Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Wakati wa Kuanzisha Biashara

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana na +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X