Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Wakati wa Kuanzisha Biashara


Wakati hali mbaya kiuchumi na mshahara kidogo  kwa walioajiriwa vikipamba moto, wazo la kuanzisha biashara na kuwa bosi wako mwenyewe linaweza kuwa bora zaidi.
Hapa kuna mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara

Kuna mambo 55 ya kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara, mambo haya yote yameelezwa kwenye hiki kitabu. Kupata nakala yako, wasiliana na +255 684 408 755
Hakikisha unajipatia nakala ya kitabu hiki. Tumia namba ya simu +255 684 408 755

1.Wazo
Katika kila wazo zuri la biashara ulilo nalo kuna mamia ya watu wana wazo hilohilo.

  • Jambo muhimu la kuzingatia ni kama wazo lako lipo,au je kuna watu tayari  wanafanyia kazi wazo lako? Kama jibu ni ndio jiulize je,unaweza kupata wazo jingine au kufanya biashara hiyohiyo kwa kujitofautisha na watangulizi wako?
  • Jiulize maswali yafuatayo: Je,kuna mpango mzuri wa biashara? Je watu wengine wanaofanya biashara hiyohiyo wanatengeneza hela? Kama wanapata nini nifanye ili nifanikiwe na niingize hela zaidi yao?
  • Mwisho unahitaji kujua kama wazo lako kisheria linakubalika au la!

SOMA ZAIDI: K anuni ya iezi sita kwenye biashara na jinsi ya kuitumia kwenye biashara

2. Mpango wa biashara
 
Tengeneza mpango wa biahara . Watu wengi huwa wanaruka kipengele hiki na kuanza moja kwa moja biashara na hatimaye biashara zao huishia njiani.
 
Kutengeneza mpango wako utakusaidia kulinda mtazamo wako na mwelekeo wako kibiashara. Fikiria mpango wa biashara yako kama kitu muhimu sana.
 
Huwezi kuanza kujenga nyumba bila ramani.
 
3. Upekee wa biashara 
 
Amua biashara yako isimame kwa namna gani, lazima uwe na ushindani kwenye biashara yako utakao kutofautisha wewe na washindani wako. Ipe thamani biashara yako.
 
4.Nani yuko kwenye gari lako
 
Tambua kwamba wewe ndo dereva na gari ni kampuni au biashara yako na bado limesimama au halijaanza safari.Amua unaenda wapi? Amua unaenda na akina nani? Amua unataka kufika wapi?
 
Utaendesha biashara peke yako au unahaji watu wa kuajiri?
 
5.Umuhimu wa mteja.
 
Soko lako kuu ni lipi?
Kabla ya kupanga mbinu za kuuza unahitaji kujua soko lako lengwa ni lipi? Soko lengwa ni kikundi cha watu ambacho kampuni yako imetengeza bidhaa kwa ajili yake.
 
 
6. www.kampuniyako .com
 
Tengeneza tovuti au blogu maalumu kwa ajili ya biashara yako. Haijalishi utakuwa unatengeneza matofali au utakuwa ukilima; kuwa na  tovuti au blogu ni muhimu sana.
 
Blogu yako itakuweka mbele kuweza kuuza biashara yako mtandaoni.
Ni muhimu pia wewe  kuwa na email kwa ajili ya biashara yako.
 
SOMA ZAIDI: TOFAUTI KATI YA BLOGU NA TOVUTI
 
7.Mwonekano wako wa kwanza (first impression)
 
Una mbinu gani ya kwenda sokoni? Utawezaje kuwashawishi watu?
 
Elewa mambo gani ni muhimu ili kuliteka soko? Kuelewa mbinu gani ni muhimu sana hasa pale watu wanapokuwa hawajui kama bidhaa yako ipo? Wapi inapatikana? Na namna ya kuinunua?
 
8.Fahamu jinsi ya kuipiga tafu biashara.
 
Je hela ya kuanzisha na kuendesha biashara itatoka wapi? Hili linaweza kuwa jambo ambalo linasumbua ila fuatilia kujua wengine waliwezaje kufanya biashara zao. Je, utalipwaje? Kama ni tigo pesa mpesa au keshi ya mkononi.
 
 
9. Je una elimu ya kutosha?
 
Kitu cha kwanza tunasikia kutoka kwa wafanya biashara wanasema ningelijua. Hii inaonesha wazi huyu mtu hakufuatilia kwa umakini biashara yake kabla ya kuianza. Jiandae kukabiliana na changamoto yoyote itakayojitokeza na kuifanyia kazi.
 
 
10.Uko wapi mlango wa kutokea?
 
Mlango wa kuyokea ni muhimu sana.Kama biashara yako itakua (na lazima itakua).
 
Utataka kuiuza ili kutengeneza faida kubwa?Kama utakuja kuiuza biahara yako unapaswa kuanza biashara yako tangu siku ya kwanza ukijua ipo siku utakuja kuiuza. Kwa hiyo anza kuweka rekodi nzuri za mapato,matumizi,manunuzi pamoja na mauzo.
 
11.Soma. Soma. Soma.  
 
Ni muhimu sana kufuatilia biashara yako kwa kusoma makala na vitabu mbalimbali vinavyohusu biashara hiyo. Hii itakujengea msingi mzuri katika biashara lakini pia utaweza kujua mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye biashara usiku na mchana.
 
Hivyo nasisitiza tena endelea kusoma kila siku ili ujue ni mabadiliko gani yanatokea kwenye biashara yako. Endelea pia kufuatilia www.songambeleadress.blogspot.com kila siku.
 
SOMA ZAIDI: MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE. Zipuuze Zikukikimbie
MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA
Sababu 101 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Kipato Chako Mara Mbili Zaidi:
 

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com

 
Ni mimi ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane.
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante sana
songambeleadress.blogspot.com


One response to “Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Wakati wa Kuanzisha Biashara”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X