Ninavyotunza Kumbukumbu Zangu Za Kiuandishi Zisipotee. Na Jinsi Wewe Unavyoweza Kufanya Pia


Rafiki yangu, juzi nilikuwa naandika makala nzuri sana, nilipokuwa nakaribia kuimaliza kabisa nilibonyeza sehemu ile makala ikapotea yote.

Kama unajua zoezi la uandishi lilivyo, utakubaliana nami kwamba kupoteza kazi ambayo umeandika kwa zaidi ya saa moja na zaidi ni kupoteza sana. Nilichofanya, sikukata tamaa, ilibidi nirudie kuiandika ile makala upya. Ninaposema, upya, namaanisha upya kabisa.

Ila kwa kawaida huwa nachukua tahadhari sana kuhakikisha kwamba sipotezi kazi zangu ninazoandika. Na hata hii juzi nilikuwa nimechukua hizi tahadhari, japo nilishindwa kufahamu ni kitu gani kilitokea moja kwa moja.

Nachukua tahadhari sana kwa sababu, nilishawahi kupoteza kazi nyingi zaidi ya hii ya juzi siku za nyuma. Nikajifunza, na ndiyo maana sasa hivi, sitaki kurudia makosa yale yale ambayo niliwahi kufanya siku za nyuma.

na pia unapopoteza kazi moja, mara nyingi unajikuta kwamba unatulia kwanza na kukosa ile hamu ya kuendelea mbele na uandishi. Binafsi ninawajua waandishi wengi ambao waliandika na kupoteza kazi (kitabu) yao moja, baada ya hapo wakashindwa kuendelea kuandika zaidi na zaidi.

Baada ya kosa la juzi nimeongeza umakini zaidi. Na hapa ninaenda kukueleza njia ambazo natumia kuhakikisha kwamba sipotezi kazi yangu yoyote ambayo nimeamua kufanya hata kama ni kidogo. Kama ungependa kusoma makala iliyofutika na kurudiwa kuandika ni HII HAPA

Kwanza, nahakikisha kwamba naandika nikiwa mtandaoni.

Moja ya kitu ninachofanya siku hizi ni kuhakikisha kwamba ninaandika nikiwa mtandaoni. Maana yake kazi inakuwa inajisevu yenyewe automatically kwa njia ya mtandao. Mara nyingi umeme ukikatika, mfano kama nipo ofisini na ninatumia desktop ya mezani, ninahakikisha kwamba ninaandika nikiwa mtandaoni. maana sina undugu na TANESCO.

Wanaweza kukata umeme wao muda wowote, na pengine kwa bahati mbaya, nikawa sijasevu kazi hiyo, na pengine nimeshafanya kazi hiyo kwa saa kadhaa bila kusevu. Na kama sijasevu kwa muda wote huo ndiyo kusema kwamba kazi hiyo ninaenda kuipoteza.

Lakini kama nimesevu kwa njia ya mtandao, maana yake hata ikitokea changamoto kama hiyo, bado ninaendelea kuwa na uhakika wa kutosha kwamba kazi yangu ipo, na ipo salama mtandaoni.

Na ninaweza kuchukua, kompyuta au simu nyingine kwa ajili ya kuendeleza ile kazi.

#makala zikae kwenye blogu na vitabu vikae google

Nikiandika makala,  basi naiandikia kwenye blogu moja kwa moja. Hili linanisaidia nikimaliza, kuhariri na kuiruhusu iende hewani.

Nilikuwa na changamoto ya kuandika makala na kuzisambaza whatsapp tu. Lakini siziweki kwenye blogu, changamoto ya makala hizi ni kwamba baada ya muda zinapotea na whatsap kunakuwa hakuna mtiririko mzuri wa maudhui ambayo mwandishi unaweka.

Inakuwa ni ngumu kwa mtu kufuatilia maandiko yako kwa wakati wa baadaye kwa utulivu. Hivyo, njia pekee ya kufanya hivyo ni kupitia blogu.

Kitu kizuri kuhusu blogu ni kwamba, haipotezi kile unachoweka. Labda wewe uamue kufuta kile ulichoweka. Lakini la sivyo kila kitu kinakaa sawa bila ya kupoteza. Kwenye hii blogu, kuna makala ambazo nimeweka humu tangu mwaka 2016. Lakini makala nilizoweka whatsap mwaka 2016, leo hii wewe mwenyewe huwezi kuziona.

Lakini makala za hapa bloguni zote zipo. Hata kama mwaka 2016, ulikuwa bado hujaanza kufuatiliaa kazi zangu.

Mfano mmojawapo ni makala hii Ifahamu Tofauti Kati Yako na Huyu.

na makala nyingine nyingi zilizo kwenye hii blogu ambazo niliandika mwaka siku za nyuma.

Hivyo kwangu, whatsap nitaendelea kuitumia kushirikisha maudhui pamoja na mitandao mingine ya kijamii. Ila sehemu kuu ambapo maudhui yatapatikana kwa uhakika ni hapa kwenye blogu hii ya SONGAMBELE. Na hata yale maudhui machache ambayo nilikuwa sijayahamishia hapa, nitafanya utaratibu yahamie hapa mara moja.

Aidha kwa upande mwingine vitabu vyote vinapaswa kukaa google. Hata kama nitaandikia maeneo mengine, lakini nitapaswa kuvihamishia google mara moja ili vikae huko.

Usikubali ufe na ndoto yako ya kuwa Mwandishi mkubwa.

Sehemu nyingine ninazotumia kutunza vile ninavyoandika ni

  • keep notes ya google
  • simplenote (japo hii siku hizi siitumii sana)
  • Telegram; kutokana na uwezo wake wa kutunza kumbukumbu bila kuzipoteza, bado telegram inaweza kutegemea kiaina kuliko whatsap. Huku nina kumbukumbu za tangu mwaka 2016, lakini whatsap hata kumbukumbu za mwanzoni mwaka jana tu sina.
  • dropbox

wewe kumbukumbu zako unatunza wapi?


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X