Vitengo Vitatu Ambavyo Vipo Kwenye Kila Biashara.Hata Kwenye Biashara Yako Vipo Hata Kama Hujui. Virasimishe Sasa


Kuna mambo 55 ya kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara, mambo haya yote yameelezwa kwenye hiki kitabu. Kupata nakala yako, wasiliana na +255 684 408 755
Hakikisha unajipatia nakala ya kitabu hiki. Tumia namba ya simu +255 684 408 755

Siku za nyuma nilikuwa najiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na ukomo. Hivi huwa inakuwaje kunakuwa na vitengo kwenye biashara au taasisi. Ni nini ambacho huwa kinafanyika mpaka watu wanajua kitengo fulani na fulani vinapaswa kuwa sehemu tofauti? Biashara inapaswa kuwa imefikia ngazi gani ili kuweza kuwa na hivyo vitengo vyote?

Siku ya leo ninaongelea vitengo vitatu muhimu kwenye biashara yako. Kama una biashara, hata kama ni ndogo, basi jua wazi kuwa kuna vitengo ambavyo huwezi kuviepuka. Hivi vitengo vipo, hata kama hujui vipo, ila ukweli ni kwamba hivi vitengo vipo kwenye biashara yako.

Inawezekana kwa sasa hivi kwenye biashara yako uko peke yako, ila ukweli ni kwamba siyo kwamba hivi vitengo havipo. Hivi vitengo kwa sasa hivi vipo, bila kujali ukubwa wa timu yako na kama uko peke yako maana yake majukumu yote ya kila kitengo kwenye biashara unayafanyia kazi wewe pekee. 

Kitendo cha wewe kufahamu hivi vitengo muhimu kwenye biashara yako siku ya leo ni kitu muhimu sana, 

Kwanza kitakusaidia kujua ni lini unafanya kazi kwenye kitengo gani.

Itakusaidia baadaye utakapohitaji kuajiri, kujua unamwajiri mtu kwenye kitengo gani na hata kuwa tayari umemwekea majukumu kamili anayotakiwa kuyafanyia kazi hatua kwa hatua kama ambavyo umekuwa ukiyatekeleza.

#kitengo cha kwanza ni kitengo cha uzalishaji. 

Biashara yoyote ile lazima ina kitengo cha uzalishaji. Uzalishaji ni kufanya bidhaa au huduma zinazohitajika kwenye biashara zipatikane. 

Mfano kama una duka, uzalishaji ni kitendo cha kununua bidhaa zinazohitajika dukani.

Kama kwa mfano unafanya uzalishaji wa sabuni, mambo yote yanayohusiana na uzalishaji wa sabuni, yanakaa kwenye kitengo cha uzalishaji. Hii ndiyo kusema kwamba mambo yote yanayohusisha kutafuta bidhaa zinazohitajika kwa ajili ya uzalishaji wa sabuni, mpaka pale sabuni inapokuwa tayari kwa ajili ya kuuza ndipo tunasema kwamba uzalishaji umekamilika.

kwa biashara ya huduma, uzalishaji ni unakuwa pale unapokuwa unaandaa hiyo huduma. Kama ni kozi, kitendo cha kuandaa hiyo kozi ndiyo uzalishaji wenyewe. 

sasa uzalishaji unapokuwa umekamilika, kazi inayofuata ni ya kitengo cha pili ambacho ninaenda kukieleza hapa chini. Kitengo cha uzalishaji mara zote huwa kinakuwa chini ya meneja wa uzalishaji, ambaye anahusika na kusimamia uzalishaji umefanyika kikamilifu kwenye biashara.

#kitengo cha masoko na mauzo.

Hiki ni kitengo muhimu sana ambacho kipo kwenye kila biashara. Inawezekana hujui kama unacho, ila ukweli ni kwamba kipo kwenye biasahara. Ni kitengo muhimu kwa sababu ndiyo kinafanya biashara iendelee kuwepo. Bila ya hiki kitengo maana yake hakuna biashara.

Hiki kitengo ndicho kinaleta hela au fedha kwenye biashara. Hiki ni kitengo ambacho kinafanya vitengo vingine viwepo. kitengo hiki kisipofanya vizuri, vitengo vingine vinaenda kufa, na hatimaye biashara kutoweka.

Masoko ni kuifanya biashara ijulikane kwa watu na

Mauzo ni pale mteja anapotoa fedha mfukoni, na kulipia bidhaa au huduma.

Mauzo yanakuwa hayajakamilika pale unapokuwa hujapokea fedha, na kamwe hupaswi kuhesabu umeuza kama hujapokea fedha. Hata kama mteja amechukua bidhaa

SOMA ZAIDI: Huu Ndiyo Muda Mzuri Wa Kusema Kwamba Umefanya Mauzo Kwenye Biashara Yako

#kitengo cha tatu ni kitengo cha fedha

Hiki ni kitengo kinchosimamia mzunguko wa fedha kwenye biashara, yaani, fedha zinazoingia na kutoka kwenye biashara. Kitengo hiki huwa kinakuwa chini ya meneja wa fedha na mipango.

Kitengo hiki kinahakikisha hesabu zote zimetunzwa vizuri kwa ajili ya kumbukumbu za sasa na baadaye.

Kitengo hiki kinaenda kukusaidia wewe mfanyabiashara mchanga kutenganisha fedha zako binafsi na fedha za biashara. Maana wengi huwa wanachanga kwenye hili. Unakuta mtu anachanganya fedha zake binafsi na fedha. Sikiliza uhusiano mkubwa uliopo kati yako wewe na biashara yako ni kwamba wewe ni mmiliki wa biashara, lakini fedha za biashara haupaswi kujimilikisha na kuzifanya kuwa za kwako. Fedha za biashara ni za biashara. wewe unapaswa kupata pesa kutoka kwenye biashara yako kwa njia mbili tu.

Njia ya kwanza ni kama mshahara au kamisheni, wewe kama mfanyakazi kwenye biashara yako basi unastahili kupata mshahara au kamisheni na njia ya pili ya wewe kupata pesa kutoka kwenye biashara yako ni gawio au faida.

HAKIKISHA UMESOMA HII: Jinsi Ya Kujilipa Mshahara Kutoka Kwenye Biashara Yako. Njia Mbili Zilizothibitishwa 

Hivyo, ndivyo vitengo vitatu muhimu sana kwenye biashara yako.

Kama kwa sasa hivi unafanya kazi kwenye kila kitengo, kazi yako kubwa ambayo unapaswa kujipatia leo hii ni kuanza kuweka vitengo kwenye biashara na wewe kujua unafanya kazi kwenye kitengo gani. Tena kama umeajiri, wagawe watu walio kwenye biashara yako kwenye vitengo. 

Muhimu, hakikisha kwamba kila kitengo kinakuwa na kiongozi, mtu ambaye atawajibika kwa kufanya au kutofanya jambo fulani.

MUHIMU: Naomba ifahamike kwamba hivi vitengo siyo mwanzo na mwisho. Unaweza kuwa na vitengo zaidi ya hivi, ila hivi vitatu ni vya kuanzia. Kaidiri biashara inavyokua unaweza kuwa na vitengo vingine zaidi. Mfano kitengo cha masoko na mauzo bado unaweza kuvitenganisha na kuwa kitengo cha MASOKO peke yake na kitengo cha MAUZO peke yake pia.

Aidha unaweza kuwa na vitengo cha utafiti pia, na vitengo vingine kulingana na jinsi biashara inavyokua.

Una swali la ziada kuhusu hii mada ya leo. Kama lipo inawezekana swali lako limejibiwa kwenye kitabu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA. Hakikisha umepata kitabu hiki kizuri sana kwa kuwasiliana na +255 684 408 755. Fanya hivyo sasa hivi ili uweze kupata nakala yako,

La sivyo, mimi nakushukuru sana kwa muda wako siku ya leo. HAKIKISHA UMEJIUNGA NA WATU WANAOPOKEA MAKALA MAALUM KUTOKA KWANGU kila siku. Kujiunga, jaza taarifa zako hapa chini

Kazi ya kufanya siku ya leo. 

  1. ainisha majukumu yote yanayofanyika kwenye biashara yako.
  2. yagawe majukumu yako kwenye vitengo vitatu vikuu vya kwenye biashara yako.
  3. ukiwa unafanya jukumu kuanzia leo, jiulize hili ni jukumu la kitengo gani?
  4. Hakikisha umepata kitabu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA  (Tumia namba ya simu +255 684 408 755)
  5. Nitafute kwa ushauri zaidi kuhusu hili ili niweze kukusaidia kwa undani. Hapa kutakuwa na gharama za consultation. Laki moja kwa saa moja kwa njia ya simu au mtandao, laki mbili na nusu kama tutaonana ana kwa ana.

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia. 

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya simu au mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

NB: Wakati naandika makala hii mara ya kwanza, karibia na kumaliza, makala ilifutika yote, kwa vile nilishaamua kuandika makala hii kwa mara nyingine. Na ndiyo maana mnaiona hapa.

Kwenye makala ya kesho, nitaeleza hili kwa kina na hatua ninazochukua kuhakikisha kwamba changamoto kama hizi hazijitokezi mbeleni. Na jinsi wewe unavyoweza kufanya ili usije ukakumbana na changamoto kama hizi. Hakikisha kesho unakuwa hapa hapa.

SOMA ZAIDI: 

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X