Njia Bora Na Ya Uhakika Ya Kunufaika Elimu Na Elimu Yako Ya Chuo


Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana ambao wanahitimu chuo huku wakiwa bado wakiwa hawana mwelekeo. na ambacho kimekuwa kinatokea ni kwamba hawa vijana ambao wamesoma  chuo na kufaulu vizuri, baadaye wanaingia mtaani, wanakutana na maisha ya huku kitaani, yanawapiga, wanaishia kufanya kazi ambazo hata wao wenyewe walikuwa hawapendi.

SIKU YA LEO nipo hapa kukuonesha namna unavyoweza kunufaika na elimu yako ya chuoni.

KAMA BADO UKO CHUONI: Fuatilia masomo yako vizuri. Hudhuria masomo yale ambayo ni ya lazima uwepo na usipokuwepo hutaweza kuelewa vizuri.

Usipoelewa uliza.

Kama kuna mazoezi yakufanya yafanye.

Halafu angalia kati ya hayo yote unayojifunza, ni kitu gani ambacho unapenda zaidi. Ukifuatilia kozi zako vizuri kuanzia mwaka wa kwanza mpaka unapomaliza mwaka wa tatu, wa nne au wa tano. Utagundua kwamba kuna kozi moja au mbili ambazo unazipenda zaidi na unaweza kuzitumia kwenye maisha yako ya kila siku.

Amua kuzichagua hizi kozi na kuzitumia kwenye maisha yako ya kila siku. Angalia ni kwa namna gani unaweza kupata pesa kutokana na hizo kozi ambazo umejifunza.

Angalia ni mambo gani ambayo watu wana uhitaji nayo na namna ambavyo wewe unaweza kutatua hayo mahitaji. Kisha tatua hizo changamoto kwa kuwaletea suluhisho.

Kwa namna hiyo, utajikuta kwamba unawasaidia watu huku wewe mwenyewe ukiwa unazidi kufnaya kitu unachopenda na unapata pesa.

KAMA UMESHAHITIMU: Najua unaijua hiyo kozi ambayo uliilewa sna, kozi ambayo ulikuwa unaipensa sana wakati ukiwa chuoni.

Hiyo kozi moja ambayo leo hii, hata ukiamshwa tu usingizini unaweza kuileza hata kwa bibi yako akakuelewa vyema kabisa.

ANZA kuangalia ni kwa namna gani ambavyo hii kozi sasa unaweza kuileta kwenye uhalisia wa maisha yako ya kila siku. Anza kuangalia ni kwa namna gani unaweza kuifanyia kazi hiyo kozi na watu wakawa tayari kutoa pesa zao mfukoni na kukulipa.

Kisha fanyia kazi kile utakachokuwa umepata.

Ukweli ni kuwa kwa fikra hizi sitegemi kwamba baada ya hapa uendelee tu kukaa nyumbani ukiwa unasema kwamba hauna kitu cha kufanya.

BADALA yake unapaswa kuanza kupambania lengo lako kubwa na ndoto zako kubwa za sasa hivi ambazo ni kuwasaidia kupiti kile unachojua.

Nimeandika kitabu kizuri sana, kinaitwa, TENGENEZA FEDHA KWA KUUZA KILE UNACHOJUA. Ni moja ya kitabu bora sana kabisa ambacho kila mwanachuo anapaswa kuhakikisha kwamba amesoma. Kimeeleza kwa undani kuhusu dhana nzima ya kutumia unachojua (ujuzi, maarifa, konekisheni, au chochote unachojua).

Kupata nakala ya kitabu hiki ni rahisi sana.

Wasiliana nasi kwa +255 684 408 755 sasa ili uweze kupata nakala yako. Utaletewa popote pale ulipo duniani.

SOMA ZAIDI:

Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu.

Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia kiasi kidogo tu.

Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.

SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea.

Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.

Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa

Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com

Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga,  +255 684 408 755

Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396

For Consultation only: +255 755 848 391  au godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X