Leo nataka nikujulishe siri kuu ya mafanikio ambayo watu wengine wamekuwa hawakwambii.
Unaweza kufanya yote kuhusu mafanikio lakini kama utakosea, hili uje wazi kuwa utakuwa umekosea kweli. Na kitu hiki ni kurudia makosa ambayo watu ambao hawajafanikiwa wanafanya.
Ukiona mtu ambaye hajafanikiwa, ujue kuna kitu ambacho watu waliofanikiwa wanafanya ila yeye hafanyi. Hivyo, njia pekee ya wewe kujiondoa kwenye umaskini ni kuhakikisha kwamba unaepuka kufanya yote yanayofanywa na wale ambao hawajafanikiwa.
VItu wanavyofanya ndivyo vimewafanya wasifanikiwe. Siyo kwamba nakuwa mbaya kwenye hili, bali najitahidi kuhakikisha kwamba nakwambia ukweli kwenye hili. Lifahamu vyema, na ufahamu ukweli huu. Ufanyie kazi
Kama hutaki kuwa masikini, usifanye wanachofanya maskini.
Mfano wa kawaida, wakati wao wanakazana kutafuta hela yao na kuitumia yote mpaka inaisha. Wewe kazana kutafuta hela kisha wekeza. Unaona, ni kitu kidogo cha toafuti ambacho utakuwa umefanya lakini ambacho kitaleta tofauti kubwa kati yako wewe na wao.
Wakati wao wanalewa, wanakula bata wikendi nzima, wewe achana na ulevi na wala usiwe na uraibu na kitu chochote kile. Hela ambayo ungeitumia kwenya uraibu, itumie kwenye kuwekeza.
Wakati wao wanakimbizana kununua magazeti, weew nunua vitabu.
Wakati wao wanasilikiza redio, wewe sikiliza audio na mafunzo ya kuelimisha. Mengi ya hayo unaweza kuyapata hapa, tena bure kabisa.
Na mengine mengi
Kwa leo inatosha rafiki yangu. Tafadhali, anza kufanyia kazi haya uliyojifunza hapa
SOMA ZAIDI: Mambo Saba (07)Ambayo Watu Waliofanikiwa Huwa Wanaepuka Kufanya
Najua kuwa ungependa kupata ushauri wa karibu zaidi moja moja kwa moja kutoka kwangu. Nitafute tuone ni lini nitakuwa na muda, ili nikupangie ratiba ya kuongea na wewe. Utalipia.
Saa moja ni laki moja mazungumzo kwa njia ya mtandao.
SAA MOJA NI LAKI MBILI NA NUSU MAZUNGUMZO YA ANA KWA ANA. Malipo yanafanyika kwanza, kisha unapewa tarehe (appointment) tutakapoweza kuongea
Tumia namba ya simu +255 755 848 391 kuwasiliana nami.
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza ambaye anaishi Morogoro nchini Tanzania.
Unaweza kujifunza zaidi kutoka kwa Godius Rweyongeza kupitia youtube channel yake hapa
Kwa ushauri niandikie songambele.smb@gmail.com
Kupata vitabu ambavyo ameandika Godius Rweyongeza, wasiliana naye kwa +255 684 408 755 na orodha ya vitabu vyenyewe unaweza kuiona HAPA. Chagua unachopenda, kisha twanga, +255 684 408 755
Kujiunga na programu yetu ya uandishi. Wasiliana na +255 678 848 396
For Consultation only: +255 755 848 391 au godiusrweyongeza1@gmail.com